BREAKING NEWS

Tuesday, September 6, 2011

MKUU wa Wilaya ya Simanjiro,Mkoani Manyara,Khalid Mandia amesema atawachukulia hatua kali kwa kuwaweka ndani wazee wa jamii ya kifugaji wa kimasai watakaowaoa wasichana wadogo ambao wanaosoma shule. Mandia aliyasema hayo jana wakati akikabidhi cheti cha ardhi cha kijiji cha Emboreet ambacho kimekuwa kijiji cha pili,kati ya vijiji 52 vya wilayani hiyo kupatiwa cheti hicho. Alisema hivi sasa jamii ya kifugaji imeweka kipaumbele kikubwa kwenye elimu kuliko miaka iliyopita,walipokuwa wanathamini mifugo hivyo wakitia fursa hiyo wasichana wa jamii hiyo wanatakiwa kupatiwa elimu. “Kama kuna mzee wa kimasai bado anatabia ya kuoa wasichana wadogo wanaosomoa shule nitamweka ndani ili iwe funzo kwa wengine wenye tabia hiyo iliyopitwa na wakati,” alisema Mandia. Ofisa mtendaji wa kata hiyo,Charles Msangya alisema,kupitia kampuni ya utalii ya Kikoti Safari Camp,kijiji hicho kimenufaika kimapato,kielimu na kuinua uchumi wa kina mama na kila mwaka wanasomesha watoto 10 wanaotoka katika familia duni. “Pia kupitia fedha tunazolipwa na kampuni ya Kikoti tumeweza kuchangia mfuko wa kina mama kwa kuwapa sh3 milioni kila mwaka,kupata ajira tano na baiskeli tano zilizotolewa na Kikoti kwa vijana wetu,” alisema Msangya. Naye,Ofisa ardhi wa wilaya ya Simanjiro Baltazar Suke,alisema cheti hicho kinawapa wananchi mamlaka ya kutambua mipaka yake na hadi hivi sasa watu 25 wa kijiji hicho wamepatiwa hati miliki ya kimila baada ya kupata cheti hicho. “Zamani Mwenyekiti na Ofisa mtendaji wa kijiji waliweza kuuza ardhi ya kijiji bila kushirikisha wananchi lakini hivi sasa hawawezi kufanya hivyo bila ruhusa yenu,” alisema Suke.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates