BREAKING NEWS

Sunday, September 18, 2011

UMEME UMETUHATHIRI ADI WANAFUNZI


wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya Fikira kwanza wakiwa wanaingia ukumbini


WAHITIMU wa kidato cha Nne mkoani hapa wameitaka serikali kushughulikia haraka suala la upatikanaji wa umeme wa uhakika kutokana na umuhimu wake kijamii na kiuchumi.

Wakizungumza katika lisala yao wakati wa mahafali ya kumaliza kidato cha Nne, wahitimu kutoka shule ya Fikiria Kwanza walisema kuwa swala la umeme limekuwa tatizo kubwa sana kwani limewaadhiri katika masomo yao .

Mmoja wa wahitimu Anna Estomi,alisema kuwa wamekuwa wakipata wakati mgumu sana wakati wanataka kusoma usiku kutokana na kukosa umeme pia walibainisha kuwa wamekuwa wakitumia mishumaa kusomea ambapo inamathara makubwa hapo badae.


Alisema kuwa mbali na wao wanafunzi kupata tabu kutokana na swala hili pia ukosekanaji wa umeme umesabisha uchumi wa nchi kushuka kwa kiasi kikubwa .

“Unajua swala hili la umeme limewaadhiri watu wengi mbali na sisi wanafunzi pia wafanyabiashara ambao ni wadogo wadogo ambao wanategemea umeme wamekuwa wanapata shida sana kwani wamekuwa wanashindwa kufanya kazi kwa wakati kutokana na kukosa umeme”alisema mmoja wa mwanafunzi aliyejulikana kwa jina la Anna Estomi.


Aliongeza kuwa pia tatizo hili la umeme limekuwa limewaadhiri pia vijana wengi ambao walikuwa wanafanya kazi katika makampuni yanayofanya kazi zake kwa kutegemea umeme pamoja na wale wa viwandani kwani wengi wao wameondolewa kazini kutokana na kutokuwepo na kazi.

Afisa Elimu Taaluma kwa shule za sekondari katika Halmashauri ya Meru, Dainesi Mosha aliwapongeza wanafunzi hao pia pamoja na walimu kwa jinsi walivyoweza kushirikiana hadi hapo walipofika.

Aliitaka serekali kuwaangaliwa walimu sana kwani bila walimu hamna kitu ambacho kingefanyika huku akisema kuwa serekali ainabudi kuwahudumia walimu vizuri na kuwadhamini kwana wanafanya kazi kubwa sana ya kuwaondoa watu ujinga.

Pia aliwataka waajiri wa shule mbalimbali kuajiri walimu ambao wanataaluma ya kutosha katika fani na sio kuwachukuwa walimu wa mitaani ambao hawana elimu ya kutosha ya kufundisha.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates