Watu wawili wamefariki dunia katika matukio tofauti likiwemo la mtu mmoja kuwawa na mwenzake kwa ajili ya mapenzi.
Mtu mmoja aliyejulikana kwa jinala Sombetini Lakitoni (25) Muarusha na nimkazi wa Sinoni wilayani Monduli mkoani hapa amefariki dunia mara baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali sehemu za shingoni na tumboni.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoani Arusha (ACP) Akili Mpwapwa alisema kuwa tukio hilo lilitokea September 22 mwaka huu majira ya saa nne kamili usiku katika mtaa wa Sinoni uliopo wilayani Monduli.
Alisema kuwa awali warehemu alikuwa na ungovi wa kimapenzi baina yake na mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Mbaruku Hassan Malugu (30) mgogo na ni mkazi wa mtaa wa Sinoni wilayani Monduli.
"unajua hawa watu wawili walikuwa na ugomvi wa kimapenzi yaani walikuwa wanamgombania mwanamke mmoja ambaye ajajulikana jina hivyo katika kugombana kule uyu Mbaruku Hassani akamchoma mwenzake na kitu chenye ncha kali katika sehemu ya shingoni pamoja na tumboni na kumsababishia umauti kumkuta papo hapo"alisema Mpwapwa.
Aidha Mpwapwa alisema kuwa mara baada ya mtuhumiwa kufanya kosa hilo alikimbia na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta na pindi atakapo kamatwa atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo.
Aliongengeza kuwa mwili wa marehemu umeifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Monduli .
Katika tukio lingine gari aina ya Scania lenye namba za usajili T 646 AGB lililokuwa na tela lenye namba za usajili T 284 AGB ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina la Jabu Shabani (45)msambaa na nimkazi wa Arusha limemgonga mtembea kwa miguu aliyejulikana kwa jina la Mamaa Moita (89) Muarusha na nimkazi wa Olerieni nakusababishia kifo papo hapo.
Akiongelea tukio hilo kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa alisemakuwa tukio hilo lilitokea september 22 mwaka huu majira ya saa 12:00 jioni katika barabara ya Nairobi -Ngaramtoni wilayani Arumeru.
Alisema kuwa gari hilo ambalo lilikuwa linatokea Namanga kuelekea mjini Arusha lilimgonga mtembea kwa miguu huyo wakati alipokuwa akivuka barabara kutoka upande mmoja wa barabara kwenda upande wa pili wa barabara.
Alibainisha kuwa dereva wa gari hilo amekamatwa na atafikishwa mahakamani mara tu uchunguzi wa tukio hilo kukamilika na mwili wamarehemu umeifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya Mounti Meru.
Mpwapwa aliwasihi wananchi kuwa makini sana wakati wanavuka barabara