WANACHAMA WA YANGA WAUTAKA UONGOZI KUTAFUTA SULUHU



WANACHAMA wa timu ya Yanga, tawi la Arusha, wameutaka uongozi wa timu hiyo kutafuta suluhu itakayoiletea maendeleo timu hiyo na kufanya vizuri katika michezo yake ya ligi kuu ya Vodacom, inayoendelea na hatimae kutwaa tena ubingwa wa tanzania msimu huu .

Mwenyekiti wa tawi la Yanga, Arusha, Haji Hamisi Haji au Mzee Hajihaji, ameyasema hayo leo mjini Arusha,alipokuwa akielezea kutoridhishwa kwake na mwenendo wa timu hiyo ambayo haijafanya vizuri katika ligi kuu ya vodaom na kuonekana kuwa inasua sua .

Haji haji, amesema kufanya vibaya kwa timu hiyo kunatokana na mgogoro ulioibuka hivi karibuni ndani ya timu hiyo kati ya baadhi ya viongozi kutokuelewa pamoja na kesi ambazo zimepelekwa hadi mahakamani na hivyo kukwamisha mafanikio ya timu hiyo na matokeo yake ni timu kufungwa fungwa hovyo kitendoambacho kinawakasirisha na kuwakera ukizingatia kuwa timu hiyo ni kubwa nchini na katika ukanda wa Afrika mashariki.

Amewataka viongozi wa timu hiyo kuyashirikisha matawi yote ya timu hiyo nchini, na kuacha kuwabagua na kuwatenga, wanachama walioko kwenye matawi bali watambue kuwa matawi yana mchango mkubwa katika maendeleo na mafanikio ya timu hiyo na matawi ni sehemu ya timu hiyo.


Hajihaji,amesema tawi la Arusha, linapata taabu kufungwa fungwa kwa timu hiyo ambayo imeopoteza michezo miwili sasa ya ligi kuu ya Voda com kwa kufungwa na timu ndogo hivyo akautaka uongozi wa timu hiyo kukaa pamoja na matawi na kuelekeza nguvu zao katika mashindano hayo ya ligi ya Vodacom.

Amesema kuwa kama viongozi wa timu wameshindwa tawi la Arusha liko tayari kuipokea timu hiyo na kuihudumia hadi mwiosho wa ligi hiyo kama ambavyo waliwahi kuichukua timu hiyo miaka 1990 wakati vuiongozi walipokuwa wakigombana.

Kuhusu usajili ,Hajihaji, ameishauri timu hiyo kutokusajili wachezajhi kila mwaka na badala yake isajili kila baada ya miaka miwili ili kuiwezesha timu kujengeka vizuri na kuwa ya kutishaio na fedha za usajili zielekezwa katika ujenzi wa uwanja wa timu hiyo uliopo jijini Dar es Salaam.

Amesema timu hiyo sio mbaya tatizo ni mgogoro wa baadhi ya viongozi mgogoro ambao umetumbukia hadi kwa wachezaji ambao wamekuwa hawafanyi vizuri katika michezo ya ligi kuu ya vodacom inayoendelea.

Amesema kuwa tawi hilo lina ucchungu mkubwa sana kuona timu haifanyi vizuri inafungwa fungwa mara kwa mara na kusababisha kebehi na matusi kutokakwa wanachama wa Simba ambao wamekuwa wakiwashambulia kwa maneno na kuwabeza kuwa timu hiyo ni mbovu jambo ambalo sio kweli hata kidogo.

Ameutaka uongozi kushirikisha wajumbe wa kamati za ufundi kutoka kila tawi nchini badala ya kamati ya Dar peke ambayo imeonekana imezidiwa uwezo hivyo matawi yako tayari kutoa msaada wa wajumbe kuisaidia timu hiyo ifanye vizuri

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post