BREAKING NEWS

Thursday, September 29, 2011

WAKILI MAARUFU AJITOLEA KUTATUA TATIZO LA MAJI

WAKILI maarufu wa kujitegemea hapa nchini,Nyaga Mawalla amejitolea kutatua tatizo sugu la maji linaloikabili shule maalumu ya msingi ya Arusha yenye mchepuo wa kingereza ambayo iko chini ya serikali kwa kuijengea kisima kirefu cha maji kitakachogharimu zaidi ya sh,50 milioni.

Akitoa taarifa mbele ya waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi juzi aliyefanya ziara ya kutembelea shuleni hapo mkuu wa shule hiyo,Angelina Kitwiga alisema kuwa wakili huyo ameamua kuikwamua shule hiyo na tatizo la maji ambalo limedumu kwa muda mrefu.

Alisema ya kuwa wakili huyo ambaye amepitia shuleni hapo ameamua kujitolea kusaidia kero ya maji mara baada ya kuguswa na tatizo hilo ambapo pia atasaidia kuboresha mfumo wa mabomba yatakayokuwa yakitoa maji kupitia kwenye kisima hicho kupitia mikondo ya maji ya chini ya ardhi.

Kitwiga, alisema kuwa kero ya maji shuleni hapo imedumu kwa muda mrefu hali inayopelekea mara nyingine shule yao kukosa maji kwa wiki moja mfululizo na wanafunzi kulazimika kutoka nje shule hiyo kusaka huduma ya maji kitendo ambacho kinahatarisha usalama wao .

Hatahivyo,alibainisha ya kuwa tayari serikali imeshatuma barua ya kuridhia uchimbaji wa kisima hicho na kuitaka ihakikishe inawasaidia kukabilina na changamoto nyingine kama uhawa wa nyumba za watumishi shuleni hapo .

Naye,waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi ,Dk Shukuru Kawambwa mbali na kupongeza jitihada za wakili huyo pia alisema ya kuwa serikali imetenga jumla ya kiasi cha sh,140 milioni kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu mbalimbali shuleni hapo.

“Tunampongeza huyu mwanafunzi wa zamani kwa kuajitolea kuchimba kisima kirefu cha maji shuleni hapa huu ni uzalendo wa kweli lakini pia serikali itajitahidi kuchangia juhudi hizi kwani tayari tumeshatoa sh,140 milioni”alisema waziri huyo

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates