BREAKING NEWS

Friday, August 12, 2011

SIMBA WAZURU MACHINJIO YA N'GOMBE ARUSHA



wachezaji wa simba wakifuatilia kwa makini jinsi ngombeanavyo chunwa



Timu ya simba ya jijini Dar es salaam imeahidi kuwapa ushirikiano timu ya Arusha meet katika maswala yote ya michezo na yaligi kwa ujumla yanayotarajiwa kuanza hivi karibuni.



Hayo yalisemwa na mwenyekiti wa timu ya Arusha Meet Fc Avelin John Meshili wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya timu ya Simba iliyokuwa imeweka kambi yake jijini Arusha kumaliza ziara yake ya kutembelea kiwanda hicho cha nyama.



Alisema kuwa wamefurahia sana kwa kitendo cha timu hiyo ya simba kukubali uwaliko ambao waliwapa wa kutembelea katika machinjio yao na kusema pia wamefurahia kwa kitendo cha uongozi wa simba kuwahaiidi kuwapa ushirikiano wa kutosha katika kipindi chote ambacho wanaanza ligi ya wilaya na hata kufikia katika ligi kuu.



“sisi tunashukuru sana kwa kitendo cha viongozi wa simba kukubali kutupa ushirikiano na wametuambia kwa sasa wana timu ya U-20 na kutuahidi iwapo tutakuwa tunaitaji wachezaji au sehemu yeyoyote tukiona tumepungukiwa na wachezaji wakati wowote watakuwa tayari kutusaidia kwa kutupa wachezaji wa timu hiyo”alisema Meshili.



Aidha alisema kuwa timu ya simba imehaidi kucheza nao mechi moja ya kirafiki ambapo alisema kuwa wataicheza mara baada ya mechi ya simba na Jkt oljoro kumalizika.





Kwa upande wake meneja mkuu wa kampuni ya Arusha meet Joachim Mmassy alisema kuwa wamefurahi kwa uongozi wa timu ya simba kuona kuwa wanafaa kwakuwapa ushirikiano na kusema kuwa watajitaidi kushirikiana nao bega kwa bega ili kuweza kuendeleza soka hapa nchini.



Alisema kuwa kwa sasa timu yao ya Arusha meet imeanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na ligi ya wilaya na amewaaidi wapenzi wa soka wa mkoa wa Arusha kukaa kitako kuisubiri timu yao ambayo ilikuwa inavuma na ilisimama kimichezo kutokana na uongozi wa chama cha mpira wa miguu wilaya ya Arusha kutofanya vyema.



“unajua pia tumealika timu ya simba kutokana na kuwa timu hii ni nzuri na nimaarufu sana hivyo tumetumia nafasi hii kujitangaza kwani iwapo wataenda makwao watasema kuwa tulitembelea kampuni ya Arusha Meet na sisi apo tutakuwa tumeshajitangaza”alisema Mmassy



Kwa upande wake msemaji wa timu ya wekundu wa msimbazi Simba Ezekiel Kamuya walisema kuwa wanashukuru wa kupokelewa na timu hiyo na wameahidi kuwa nao bega kwa bega .



Wakati huo huo Timu timu hii ya simba ambayo imeweka kambi mkoani hapa imesema kuwa inaalika timu kubwa na zenye uwezo za nje ya nchi ili kuweza kujiimarisha vizuri kwa ajili ya ligi kuu ambayo inaanza hivi karibuni.



Hayo yalisemwa na msemaji wa timu ya wekundu wa msimbazi (simba) Ezekiel Kamuya wakati alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maandalizi ya mechi baina yao na timu ya Fc leopard ya nchini Kenya.



Alisema kuwa wao kama wanasimba wamekuwa wakialika timu kubwa kucheza nao ili kuwez akubaini makosa ambayo wanayo na pindi wanapo yagundua huyafanyia kazi kabla ya ligi kuu kuanza.



Alisema kuwa katika mechi iliyopita ambayo walicheza na timu ya Victors ya nchini Uganda walicheza na kubaini makosa yao na kwa sasa wamejiandaa vyema kwani wamerekebisha makosa ambayo waliyafanya katika mechi iliyopita.



Alikiri kuwa timu ya Victors ni nzuri na iliwashinda kutokana na wachezaji wao kutoizoea hali ya hewa ya mkoa wa Arusha pia alisema kuwa timu yake ilikuwa inamda mrefu haijaingia kambini kwa ajili ya kujiandaa na mechi hile.



Aliwasihi washabiki wa mpira hususa ni wapenzi wa timu ya simba kuwa na subira kwani katika kipindi hichi cha mechi za kirafiki wanafanya mazoezi na wakitaka kuiona timu ya simba waisubiri katika msimu wa ligi kuu ndio wataitambua simba yao vizuri na kuikubali .



Kwa upande wa timu ya Fc Leopard ambayo wanacheza nayo leo (kesho) alisema kuwa timu hiyo ni nzuri na inamazoezi ya kutosha kwani timu hiyo kwa sasa ipo katika msimu wa ligi ambayo umeanza nchini Kenya na kwa sasa timu hiyo ndio ambayo inawika sana katika nchi yao ila alisema kuwa wanaimani watashinda mechi hiyo kwani wachezaji wameshazoea hali ya hewa na wale ambao wanaumwa wameshapata nafuu hivyo kikosi kizima cha simba kitafanya mashambulizi.



Ezekiel alisema kuwa mpaka sasa timu hii ya Fc Leopardi imeshawasili mkoani hapa kwa ajili ya mechi hiyo na kubainisha kuwa maandalizi yote kwa ajili ya mechi hiyo yamekamilika.



Alitaja viingilio vya mechi hiyo kuwa katika jukwaa kuu kiingili kitakuwa shilingi 5000 huku jukwaa B kingilio kikiwa ni shilingi elfu tatu na mzunguko ikiwa ni shiligi elfu mbili.



Aidha alibainisha kuwa katika siku hii ya mechi pia wanachama wapya waliojiandikisha watakabidhiwa kadi za uwanachama katika uwanja huu huu wa sheikh Amri Abeidi.



Alitoa wito kwa wapenzi wa soka wa mkoa wa Arusha kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao ili iweze kushinda.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates