BREAKING NEWS

Sunday, August 7, 2011

SIMBA KUCHEZA NA VICTORS KESHO


Godfrey Nyange Kaburu katika kati ni Makamu mwenyekiti wa timu ya simba wa kwanza kushoto ni Moses Basena kocha wa timu ya simba ,kuliani ni kocha wa timu ya Victors Fc Josephy Mutyaba wakati wa mkutano wa waandishi wa habari




mkuu wa msafara wa Victors FC akiongea mbele ya waandishi wa habari


kocha wa timu ya Simba Moses Basena akiwa anaongea na mkuu wa msafara wa timu ya victors Akatwele Aizak katika uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini hapa
Timu ya simba inatarajia kucheza kesho katika mchezo wa kirafiki baina yao na timu ya Victours kutoka Uganda baada ya timu ya simba ya Uganda kukosa ruhusa ya kuhuthuria katika mechi iliyokuwa imepangwa kuchezwa kwenye Tamasha la Simba Day.

Akiongea na waandishi wa habari mapema jana katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Makamu mwenyekiti wa chama hicho Jofery Nyange Kaburu alisema mpaka sasa maandalizi yapo tayari na timu zitakazocheza kesho zimesha wasili kwa ajili ya mashindano haya.

Alisema kuwa timu ya simba wa Uganda ambayo ilikuwa inatakiwa icheze kesho na timu ya Simba sport klabu ilishindea kuhuzuria mechi hiyo kutokana na kukosa ruhusa ya kutoka nje ya nchi yao.

"unajua kuwa timu ya Simba ya Uganda inamilikiwa na jeshi la wananchi wa nchi hiyo hivyo haiwezi kutoka nchini bila kupewa kibali ivyo walikosa kibali cha kuja na kwa bahati nzuri walitueleza ndipo tukaamua kuwasiliana na timu ya victors maana tulikuwa tunajuana wakakubali ndo wakaja badala ya simba ya uganda"alisema Nyange

Nyange alisema kuwa hali hiyo imepelekea kuwepo na mechi nyingine ambayo nayo mpaka sasa imekubali kucheza mchezo huo wa kirafiki ambao utachezwa katika Uwanja wa sheikh Amri Abeid mjini hapa na imeshawasili kwa ajili ya mechi hiyo.

Alisema kuwa katika Tamasha hilo pia kutakuwa na mambo mbalimbali ambapo mbali na kucheza mchezo huo wa kirafiki pia wataweza kufanya mambo mbalimbali ikiwa ni njia mojawapo ya kuimarisha timu ya Simba kwa wadau na wapenzi wake.

Katika Tamasha hili pia tuta tangaza wachezaji wetu wapya ambao tumewasajili kwa msimu huu kwa wapenzi wa Simba Mjini hapa, sanjari na hilo tutatangaza jezi zetu mpya ambazo nazo zitatumika kwa msimu ujao wa ligi kuu”alisema Nyange.

Katika hatua nyingine Nyage alisema kuwa kupitia mchezo huo wataweza kutangaza na kutoa kadi mpya za wanachama kwa kuzingatia wananchama wapya ili waweze kufanya timu hiyo iwe na uimara zaidi kwa mashabiki wake na pia wataweza kuitambulisha jezi mpya ya timu hiyo ambayo wataichezea katika msimu ujao.

Nyange alibainisha kuwa kwa upande wa burudani wanatarajia kuwepo na mechi ya ufunguzi ambayo itacheza timu ya viongozi wa simba kutoka makao makuu dar es salaam pamoja na viongozi wa mkoani hapa ambao watacheza na timu ya maveterani ya mkoani hapa .
Aidha alisema kuwa watawapa kipaumbele kipaumbelee wasanii chipukizi wa mkoa wa Arusha ili waweze kujitangaza kupitia tamasha hilo.

Naye kocha wa timu Victours kutoka Uganda Joseph Mutiyamba amesema kuwa wamejipanga vema katika mchezo huo ambapo wamejiandaa sana katika kupambana na Simba Ya Tanzania ili kurudisha ushindi Uganda

Joseph amesema kuwa katika Tamasha hilo pia wameandamana na wachezaji saba ambapo wanatokea katika Timu ya Taifa ya Uganda ambapo nao wataweza kusaidia kutia joto katika Tamasha hilo.

Alisema kuwa amefurahia kwa jinsi walivyopokelewa na wapenzi wa soka wa mkoa wa Arusha pamoja na wanasimba kwa ujumla na amefurahia pia kualikwa kusherekea siku hii ya simba pamoja na wanasimba .

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates