BREAKING NEWS

Saturday, August 6, 2011

Flag this message MATEMBEZI YA CHAKI ARUSHA YAFANIKIWA KUKUSANYA ZAIDI YA MILION 46 KWA AJILI YA UJENZI WA SHULE YA NKOASIO MERU

Wadau wa elimu hapa nchini wamefanikiwa kuchanga zaidi ya milion 46 katika matembezi ya chaki ambapo fedha hizo ni kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Nkoasiao iliopo katika kata ya Kingori wilayani meru Mkoani hapa.

Akiongea mara baada ya kukamilika kwa matembezi hayo ambayo yameandaliwa na klabu ya Rotery golden sunrise ya Arusha kwa kushirikiana na chama cha kimataifa cha kundi la waelimishaji (PDK), tawi la Tanzania, Raisi wa Rotary Mjini hapa bw Beatius Mlingi alisema kuwa fedha hizo zitakuwa na manufaa sana kwa ajili ya shule hiyo ya Nkoasio.

Alieleza kuwa lengo halisi la matembezi hayo ambayo yalienda sanjari na uchangishwaji wa shule ya Nkoasio ambayo bado ina uitaji mkubwa sana wa ujenzi ili iweze kukamilika , huku lengo lingine la matembezi hayo likiwa ni pamoja na kumtia moyo mwalimu wa Tanzania kuhusiana na uimu wa kazi yake.

Beatius ameeleza kuwa kwa sasa asilimia kubwa ya watanzania wamesahau sana sekta ya elimu hali ambayo inasababisha hata wanafunzi walio wengi wa kitanzania kutembea umbali mrefu katika kutafuta elimu huku baadhi ya wanafunzi hao kuwa hatarini sana kupata vishawishi mbalimbali vya kidunia.

"leo kupitia matembezi haya ya chaki tumeweza kupata zaidi ya milion 46 kwa ajili ya shuguli mbalimbali za ujenzi wa shule ya Nkoasio sasa hii inatakiwa ichukuliwe kama changamoto na asasi nyingine katika kuleta ufafanuzi na utatuzi wa masuala mbalimbali ya elimu"alisema Mlingi.


Kwa upande wake rais wa PDK hapa nchini ,bw Gedion Rwegerera alisema muda umefika kwa jamii kujijengea utamaduni wa kujichangia maendeleo yao badala ya kutegemea wahisani halli ambayo nayo inachangia kwa kiwango kikubwa sana kushuka kwa viwango vya elimu hapa nchini wakati watanzania wenyewe wana

Rwegerera alisema kuwa uamuzi huo wa asasi hiyo utaweza kuwasaidia wananchi hususan wa wanafunzi wa kata ya Kingori ambapo hapo awali watoto walikuwa wanalazimika kutembea umbali mrefu wa kutafuta elimu hali ambayo nayo inafanya jamii hiyo ya kata ya Kingori kuwa nyuma Kielimu.

Alimalizia kwa kusema kuwa ni vema kwa kila asasi na mashirika kuweza kusaidia shuguli mbalimbali za maendeleo na kuachana na tabia ya kuachia kazi yote serikali hali ambayo inafanya watoto wengi kukosa elimu jambo ambalo lina madhara makubwa sana kwa Taifa la Baadaye. uwezo wa kuendeleza elimu kwa kiwango kikubwa sana na kufanya nchi kuweza kuzalisha wataalamu wengi zaidi.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates