BREAKING NEWS

Thursday, August 11, 2011

DIWANI AJITOLEA KUJENGA SHULE YA SEKONDARI

WANANCHI katika kata ya Sambasha wilayani Arumeru mkoani Arusha ,wapo mbioni kuondokana na changamoto ya muda mrefu inayowakabili watoto wao ya ukosefu wa shule ya sekondali ,hali ilinayowalazimu kutembe umbari mrefu kuifuata elimu ,baada ya diwani wa kata hiyo kujitolea kuwajenga shule hiyo .





Changamoto hiyo inasababisha wanafunzi hao kuamka usiku sana na kutembea umbali wa zaidi ya kilometa tatu kufuata huduma ya shule katika shule ya sekondari Ilkiding’a hali inayopelekea wanafunzi wengi kushindwa kuhudhulia masomo yao kwa wakati na wengine wakiishia vichakani kwa kuchoka na mwendo mrefu wa kila siku.



Diwani wa kata hiyo ,Wiston Melakiti Laizer alisema kuwa, changamoto hiyo imetokana na kugawanywa kwa kata ya Ilkidinga iliyokuwa na vijiji sita ,na kuanzishwa kata mpya Sambasha yenye vijiji vitatu,ambapo vijiji vya Tiboro,Shimbora na sambasha viliunda kata hiyo.



Alisema kuwa, kutokana na kata hiyo kuwa mpya inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kutokuwa na shule hata moja ya sekondari, kwani miradi mingi ya maendeleo iliyokuwa ndani ya kata hiyo ,imehamika katika kata hiyo ya Ilikiding’a.


Kufuatia changamoto hiyo ameamua kuanzisha ujenzi wa shule ya sekondani,ambapo sehemu kubwa ya gharama za ujenzi wa shule hiyo zikitokana na mchango wake kwa kushirikiana na michango kutoka kwa wananchi wa vijiji hivyo.



Alisema ujenzi wa shule hiyo kwa sasa unatarajiwa kukamilisha madarasa matatu ya awali ikiwemo ofisi za walimu na mwalimu mkuu,na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu ambapo gharama za ujenzi huo ni zaidi ya shilingi 60 milioni.



Ambapo kwa awamu ya kwanza wamejenga madarasa matatu kwanza kwa ajili ya kuanza kupokea wanafunzi watakaofaulu kuingia kidato cha kwanza mwakani, huku baada ya kukamilika kwa awamu ya kwanza wataanza tena awamu ya pili ya ujenzi mwingine wa madarasa matatu .



Laizer alisema kuwa lengo ni kuwa na kidato cha kwanza hadi cha nne , na kutokana na changamoto hiyo katika ujenzi wa awamu ya pili kila kijiji kitawajibika kujenga darasa moja, hivyo aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia shughuli za maendeleo katika kata hiyo mpya wilayani Arumeru.



Alisema kuwa,mbali na kukabiliwa na changamoto hiyo ya elimu , pia wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa kituo cha Afya kutokana na kuwa zahanati iliyopo kuwa ni ndogo na haikidhi changamoto za wananchi walio wengi.



Alisema kuwa,ukosefu wa kituo cha afya imekuwa ni tatizo kubwa kwa akinamama wajawazito ambao wamekuwa wakiteseka kipindi cha kujifungua kutokana na kufuata huduma hizo umbali wa kilometa 12 hadi hospitali ya Mkoa ya Mount Meru, huku wanaokwenda hospitali ya Seliani wanatembea umbali wa kilometa 3 hadi 4 kufuatana huduma hizo muhimu.



‘Ninachojaribu kusisitiza hapa ni kuwa ,kutokana na changamoto hizo ninajitahidi kutafuta wafadhili katika sehemu mbalimbali ili kuweza kujenga wodi nne na hatimaye kukarabati zahanati hii na kuwa kituo cha Afya kulingana na uhitaji wa watu ulivyo mwingi,nah ii itasaidia sana kwa ajili ya kulaza wanawake wajawazito ambao wamekuwa wakikumbana na changamoto kubwa sana hususani kipindi cha kujifungua’alisema Laizer.



Alifafanua kuwa, katika kuhakikisha wananchi wanaondokana na changamoto hizo wapo katika mkakati wa kununua gari la kubebea wagonjwa (Ambulance) ili kuondokana na changamoto ya usafiri wakati mgonjwa anapohitaji kuwaishwa katika hospitali nyingine kwa huduma za haraka.



Aliwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kuchangia miradi ya maendeleo katika kata yao, ikiwa ni pamoja na kuitunza miradi ambayo ipo kwa sasa hivi kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa sana kuendelea kusaidia wananchi wa kata zingine ambao watahitaji huduma mbalimbali.



Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates