BREAKING NEWS

Saturday, August 6, 2011

SIMBA DAY KUFANYIKA ARUSHA

Timu ya Simba inatarajia kufanya tamasha lake lijulikanalo kama simba day mapema Agosti nane mwaka huu katika uwanja wa kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid jijini hapa .

Akiongea na waandishi wa habari msemaji wa klabu ya simba tawi la mkoani Arusha Ezekiel Mwakyembe alisema kuwa tamasha hilo litashirikisha michezo mbalimbali ikiwemo mpira wa miguu pamoja na ngoma za asili.

Alisema kuwa katika tamasha hilo ambalo litashirikisha timu mbalimbali ikiwemo timu ya Simba sport klabu ya jijini dar es salaam ambayo itakutana na timu ya Simba ya nchini Uganda.

Alibainisha kuwa pia mbali na timu hizi mbili kukutana pia kutakuwa na mechi baina ya timu ya viongozi wa Simba Spoty Klabu ambao wanataumana na timu ya makocha wa mkoa wa Arusha.

Alisema kuwa mpaka sasa kila kitu kimekamilika na timu zote zimeshawasili mkoani hapa kwa ajili ya tamasha hilo ambalo litafanyika jumatatu Agosti 8.

Mwakyembe alisema kuwa tamasha hili litakuwa mahususi kwa ajili ya kuwapa zawadi watu ambao wameisadia timu ya simba pamoja na kuwafanyia mema timu ya simba ambao alibainisha ni pamoja na viongozi ,wachezaji pamoja na wanachama .

Mbali na hilo pia alisema kuwa tamasha hili pia litakuwa ndio fursa ya kuwatambulisha wachezaji wapya na wazamani ambao wamesajiliwa rasmi kuichezea timu hiyo msimu ujao.

"tamasha hili litakuwa ni fursa ya kuwatambulisha wachezaji wapya waliosajiliwa kuichezea timu hii kwa wadau na wanachama wa simba"alisema Mwakyembe.

Alibainisha kuwa pia mechi hii pia itakuw ani fursa ya wachezaji kuendelea kufanya mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na ligi mbalimbali zijazo ikiwemo ligi kuu,Ngao ya hisani pamoja na kombe la shirikisho ambapo alisema kuwa kwa upande wa timu ya Simba ya Nchini Uganda nayo inatarajia pia kushiriki katika mashindano haya kombe la shirikisho.

Alisema kuwa pia katika siku izo kutakuwa na kadi za kujiunga na timu hiyo na kusema kuwa kwa sasa zimepungua bei hivyo ni fursa ya kila mtu ambaye anataka kujiunga na klabu hiyo ya simba kujitokeza kuchukua kadi hiyo ya uwana chama.

Alitoa wito kwa wadau wa soka wa mkoa wa Arusha na nje ya mkoa wajitokeze kwa wingi kusherekea kwa pamoja siku hiyo ya Simba day ambapo alisema kutakuwa pia na michezo mingi pamoja na burudani nyingi .

Mpaka sasa timu hii ya simba imeshawasili mkoani hapa na inaendelea na mazoezi katika uwanja wa sheikh Amri Abeid jijini.

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates