BREAKING NEWS

Saturday, August 6, 2011

VIJIJI VYAJIPANGA KUJENGA SHULE YA SEKONDARI

Vijiji vitatu vya Nkoanekoli, Sangananu, na kiwawa vyote vilivyopo katika halmashauri ya Meru Mkoani hapa vinatarajia kujenga shule ,maalumu ya vipaji kwa wasichana ambapo shule hiyo itaweza kuongeza ufanisi wa elimu katika wilaya Ya Meru

Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa vijiji hivyo Bw Sangito Andrew mapema jana wakati akiongea na gazeti hili mara baada ya kumalizika kwa mkutano baina ya vijiji hivyo vitatu.

Sangito alisema kuwa shule hiyo ambayo itajengwa katika eneo la kiwawa litakuwa na manufaa makubwa sana kwa wananchi wa eneo la Meru ambapo kwa sasa bado wilaya hiyo haina shule kwa ajili ya wasichana hali ambayo itafanya wasichana wa eneo hilo kujikita zaidi katika elimu

Alieleza kuwa shule hiyo ambayo itaanzwa kujengwa hivi karibuni itaweza kuwanufaisha wakazi wa eneo hilo wapatao laki moja ambapo hali hiyo itaweza kuzaa hamasa kubwa ya ongezeko la wasichana wenye elimu ndani ya wilaya hiyo ya Meru

“tuna hekari 12 za eneo lakini kwa sasa tutaweza kujenga shule kwa ajili ya wasichana wetu tena wenye vipaji maalumu ambapo itakuwa ni shule yetu ya kwanza kwa vipaji maalumu ndani ya wilaya yetu”alisema Sangito

Hataivyo alieleza kuwa kwa sasa bado kuna maeneo mengi ya wazi ambapo maeneo hayo yanatakiwa kutumiwa vema kwa ajili ya shuguli mbalimbali za maendeleo kama vile ujenzi wa shule, hospitali, ofisi za serikali ili kuweza kuokoa jamii na matatizo ambayo yanasababisha madhara makubwa sana ndani ya jamii ya mkazi wa Arusha

Alisema endapo kama maeneo hayo ya wazi yataweza kutumika vema na kuachana na tabia ya kuuzwa yataweza kuwa na manufaa makubwa sana kwa taifa lijalo ambapo ardhi itakuwa ni sehemu mojawapo ya kuweza kulikomboa taifa hilo

“jamani ni vema kama wananchi waakachana natabia ya kuuza ardhi kwa kuwa ardhi ni rasilimali ambayo hairabiki na pia kama tutaitumia vema ardhi yetu tutaweza kuwa na manufaa kwa kuwa kama tutaijengea kwa ajili ya jamii yetu tutaweza kuacha urihi mzuri tofauti na kuuza ardhi kama baadhi yetu tunavouza ardhi zetu”alisema Sangito.

Naye diwani wa kata hiyo Loti Nnko alisema kuwa nazo kata nyingine bado zinauwezo wa kuhakikisha kuwa zinaweka malengo hata ya ujenzi wa shule za wasichana, wavulana, wenye vipaji maalumu ili kuweza kuibua vipaji zaidi ndani ya kata hizo

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates