BREAKING NEWS

Wednesday, December 7, 2022

MADHARA YATOKANAYO NA WANAWAKE WA JAMII YA KIFUGAJI KUJIFUNGULIA MAJUMBANI

 


Na Woinde Shizza , ARUSHA


 Tanzania imefanikiwa kupunguza vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano, bado ipo changamoto kwa baadhi ya Wanawake wa jamii ya kifugaji (Maasai) kujifungulia majumbani.



Kumekuwa na tabia ya Wanawake wa Jamii hiyo kujifungulia majumbani jambo ambalo linaleta madhara yakiwemo ya vifo vya mama na mtoto


Naishock Lomanyani ni mama ambaye amekubwa na tatizo la kufiwa na ndugu yake ambaye alifariki mara baada ya kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua, anaeleza kuwa sababu kubwa zinazowafanya wasijifungulie hospital ni pamoja ya kukosa elimu ya kutosha ya madhara ya kuzalia nyumbani pia woga na hofu 



"Unajua asilimia kubwa ya watu wa jamii zetu bado wana imani za kizamani bado hawajapata elimu ya kutosha Kuhusiana na matatizo yanayotokana na kujifungulia majumbani ,wapo ambao wana elimu na wanaenda kujifungulia katika vituo vya afya lakini wengi wao bado elimu ni duni"alifafanua 


Elias Melau ni mume wa Neema Nyangusi anaeleza kuwa yeye kama mume haoni sababu ya kumpeleka mwanamke wake kujifungulia katika kituo cha afya kwani hivi vituo vimekuja miaka hii zamani enzi za wazazi wao havikuwepo na walijifungulia majumbani salama


"Mimi kiukweli sioni sababu kwakuwa ata ukiangalia yule mke wangu pale anamimba lakini anafanya kazi mpaka mwisho ,unaona zile kuni yeye ndio kaenda kukata hivyo anajijengea mazingira ya mazoezi tangu anapobeba mimba ikifika kipindi cha kujifungua hateseki kwenda hospital anajifungulia apa apa kwakuwa njia inakuwa nyeupe kingine ,wanawake wetu wanakula sana vyakula vya jadi siyo walaji wa  mafuta kama wanawake  mjini wanavyokula"alisema 



UTAFITI UNASEMAJE


Kulingana na Utafiti wa Idadi ya Watu  

na Afya wa mwaka 2015-16,takwimu za vifo vya mama zimeendelea kwa vifo 556 kwa kila wanawake 100,000 wanaojifungua kutokana na sababu kama ukosefu wa huduma bora, ukosefu wa huduma za dharura ya uzazi, uhaba mkubwa wa wanawake kuweza kupata huduma za afya kwa uhuru, na sababu zitokanazo na uzazi kama vile kutokwa na damu baada ya kujifungua.




Miradi ya USAID ya Afya ya mama na mtoto (MCH)nchini Tanzania inaendelea kusaidia jitihada za kuzuia vifo vile vitokanavyo na Uzazi, ikitoa kipaumbele cha kuboresha afya ya 

wanawake walio katika mazingira magumu, Katika ngazi ya kitaifa, USAID inatoa usaidizi wa kitaalamu kwa Wizara ya Afya, 

Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa Tanzania bara na kuwezesha utoaji wa huduma za kuokoa maisha kwa akina mama, Mifano ya usaidizi wa kitaalamu ni pamoja na kuandaa miongozo ya kliniki ya kujifungua kabla ya wakati


ASASI ZISIZO ZA KISERIKALI ZA LONGA



 MARY BARNABA MUSHI mkurugenzi wa Shirika la Women and Children Welfare Support anaeleza baadhi ya sababu zinazopelekea wanawake wa Jamii hiyo kujifungulia majumbani kuwa  ni pamoja na kutokuwa karibu na huduma za afya ,elimu kutoendelea kuwafikia kama inayotolewa mijini ambapo matamasha yanafanyika ,matangazo yanafanyika ya kuwaeleza wananchi mathara ya kujifungulia majumbani.


Alibainisha kuwa Kwa jamii za kimasai hususa  wale waliofanyiwa ukeketaji wamekuwa na hofu ya kwenda kujifungulia hospitali wakihofu kuwa wakifika huko wanaweza kutukanwa au kujibiwa majibu ya hovyo  na wakati mwingine  kushtakiwa Kwa sababu wamefanya vitendo vya ukeketaji Kwani nyakati hizi zipos heria kali pale mtu anapokutwa amemkeketa mtoto wa kike.

Gharama kubwa pia zimekuwa zikisababisha jamii hiyo kutokwenda kujifungulia hospital maana huduma za mama mjamzito zimekuwa sio za bure tena kama awali, Kwa Sasa  wanawake wanapokwenda kujifungua wamekuwa wakinunua vifaa wenyewe Hali ambayo imekuwa inawapa changamoto kutokana na vipato vyao kuwa chini.


NINI KIFANYIKE

-Elimu zaidi inatakiwa kutolewa wanawake wa Jamii hizi za kimasai juu ya  madhara ya kujifungulia majumbani

-Vituo vya afya vijengwe ndani ya jamii hizo Ili kupunguza gharama za kufuata huduma hizo mbali

-serikali iwawekee vifaa vya kujifungulia katika vituo hivyo ya afya na pia ikiwezekana  wapewe huduma bure Ili kupunguza changamoto ya vifo Vitokanavyo na uzazi.








Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates