TAASISI ZINAZOTOA MIKOPO ZINAVYOMUINUA MWANAMKE

 



Na Woinde Shizza , ARUSHA

Wanawake wengi walikuwa wanashidwa kufanya shughuli zao za kimandeleo ,biashara kutokana na kile kinachosemekana kuwa ni kukosekana Kwa mtaji lakini mara baada ya taasisi binafsi pamoja na mikopo inayotolewa na serikali imekuwa suluhisho la tatizo hilo

Milka Lema ni mwanamke ambaye ameweza kujikwamua na kuanza biashara kutokana na mikopo inayotolewa na taasisi za kifedha binafsi pamoja na fedha za halmashauri.

AELEZA ZAIDI

Anabainisha kuwa kabla ya kuingia katika taasisi hizo za mikopo aliteseka sana maana alikuwa hajui namna gani ataweza kupata fedha Kwa aji ya kukuza mtaji katika biashara yake ambapo alieleza kuwa awali woga ulimfanya kutokujiamini na kwenda kuchukua mkopo

" Nina rafiki yangu alinipa moyo na kunishauri kuwa nikitaka kufanikiwa kwanza natakiwa kuthubutu ,kuacha woga na kufanya maamuzi ,baada ya kupata ushauri wake nikaamua kuchukua na kwenda katika taasisi moja binafsi ya mikopo ijulikanayo kama Daily na ndio nilianza kuchukua mkopo wa laki mbili na kuingiza katika biashara yangu ambapo Kwa sasa hivi nachukua mkopo wa hadi milioni Tano .


Mfanyabiashara wa culture Yasinta Mkawe akiwa katika biashara yake

Kwa upande wake Yasinta Mkawe alisema kuwa tatizo la wananawake sio wathubutu na ndio maana wanashidwa kujitoa na kwenda katika hizo taasisi Kwa ajili ya kuchukua fedha zitakazo wasaidia kuendeleza na kukuza biashara zao .

"Hii mikopo inatusaidia sana wanawake kuongeza kipato chetu na pia mitaji yetu katika biashara zetu ,kukuza au kutupa nguvu katika kukuza biashara zetu mfano Sasa hivi biashara ni ngumu lakini napata nguvu kutoka katika taasisi hizi tunasaidika kwakuwa tunaongeza mitaji na biashara zetu zinakuwa"alisema Yasinta 

Alisema woga unawafanya wanawake wengi wasichukue mikopo hii,pia riba kubwa ni chanzo ,mzunguko mdogo katika biashara zao unawafanya kuwa waoga huku wengi wao wakihisi deni Hilo litawafanyà washindwe kuurejesha 

WITO GANI WANATOA KWA WANAWAKE WENZAO

-Waliwataka wanawake wengine kuwa na uthubutu wa kufanya jambo hilo itawasaidia  kufanya maendeleo bila woga

-Waliwataka wathubutu kuchukua mkopo Kwa kuanza kidogo kidogo hadi pale watakapo pata uzoefu mzuri wa kukopa na kurejesha.

WANAITAKA NINI SERIKALI

-Wameitàka serikali kuendelea kushawishi taasisi binafsi kupunguza riba Ili wanawake wengi waweze kuchukua mikopo hiyo na kurejesha bila tatizo 

Wamesema Elimu iendelee kutolewa Kwa wanawake juu ya faida za kuchukua mikopo 

Aidha wameiomba Serikali itoe mikopo isiyo kuwa na riba ili kumuwezesha kila mtanzania hususani mwanamke kuchukua mkopo bila ya kuwa na hofu wala woga.

TAASISI ZA MIKOPO ZISIZOKUWA ZA SERIKALI NAZO ZINA NENO



Eliza Akyoo ni ofisa mikopo pia ni ofisa mshauri mwelekezi wa taasisi ya mikopo ya Daily  akiongea na mwandishi wa habari hizi

Eliza Akyoo ni ofisa mikopo ambaye pia ni ofisa mshauri mwelekezi wa taasisi ya mikopo ya Daily anaeleza kuwa wao ni taasisi ya mikopo inayotoa fedha Kwa wajasiamali wadogo wadogo wa vikundi pamoja na wafanyabiashara mmoja mmoja wanawake pamoja na wengine huku akifafanua kuwa asilimia kubwa ya watu wanaochukua mikopo hiyo ni wanawake.

Amesema muamko wa wanawake kujitokeza kuchukua mkopo ni mkubwa kiasia hivyo wanalazimika kuwapa ushauri wanawake wengi  faida za kuchukua mkopo 



Valentine Alex afisa mikopo wa Daily akiongea na mwandishi wa habari hizi

Valentine Alex afisa mikopo wa taasisi hiyo anasema kuwa wamekuwa wakiwapa elimu ya mkopo wanawake wale wanaoenda kwao kuchukua mkopo pamoja na wale ambao hawajiamini kuchukua mikopo na kuwaambia kuwa mikopo ni haki ya mfanyabiashara yeyote yule anaejitambua na mwenye biashara ambayo ni endelevu.


tunaongea na wateja wetu hata wale ambao hawajawahi kukopa sehemu yeyote tangu wamezaliwa ,tunawaeleza kwamba kama wameweza kupata mtaji kidogo na kuanzisha biashara na kuendesha zaidi ya mwaka mmoja hawata shidwa kufanya marejesho ya mikopo pamoja na hayo pia tunawafundisha namna ya kuchagua kikundi ambacho kitaweza kufanya kazi vyema pindi wanapopewa fedha hizo.



"Wanawake wengi wamekuwa wanatendwa kutokana na watu ambao wanaungana nao kwenda kuchukuwa mikopo ,hivyo tunawashauri namna ya kujua watu watakaoendana nao ,wanawashauri kabla ya kuingia katika taasisi ya mikopo ni vyema wakachunguzana Kwa muda ,na pia niseme tu wanawake wanaokuwa waoga ni wale ambao wameshakutana na wengine ambao ni matapeli pamoja na wale waliolemewa na mikopo mingi



Alisema kuwa mwanamke yeyote wa kitanzania ni mpambanaji na ndio maana hata Rais Samia Suluhu Hassan ni mwanamke ambaye ameweza kujaribu na kukaa kwenye viti vya juu hivyo aliwasihi waamke wajitokeze kuchukua mikopo kwa ajili ya kukuza biashara zao


"Niseme tu sisi Daily financial services LTD tunahitaji wanawake wanaoogopa ili tuweze kuongozana nao vyema na kuwaelimisha zaidi ili nao wapate mikopo na kwenda kufanya kazi na  kuleta marejesho ambapo mbali na hiyo pia wataweza kukuza mitaji yao kupitia Mikopo yetu hivyo ni wasihi wanawake waamke wajitokeze kuchukua mikopo na sisi tupo tayari kuwapa"alisema


Maafisa mikopo wa Daily financial wakiendelea na kazi

Kwa wale wanaosema wanaweza kujikimu kupitia mitaji yao niwaambie ni waongo hamna mfanyabiashara yeyote anayeweza kujikimu bila kuchukua mkopo ,ukitaka biashara ikuwe na iendelee ni vyema wakakimbilia katika taasisi za kibenki ,fedha za halmashauri Kwa ajili ya kukuza biashara zao.














Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post