Na Woinde Shizza , ARUSHA
Naibu Waziri wa Uwekezaji ,Viwanda na Biashara,Exaud Kigahe amewataka wawekezaji wanaoshindana katika sekta ya viwanda,ndege na makampuni ya utalii kutumia teknolojia rafiki ili kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa inayochangia mabadiliko hasi ya tabia nchi.
Hayo yalisemwa Jijini Arusha na Naibu Waziri Kihage wakati wa ufunguzi wa kongamano la madhimisho ya Ushindani Duniani katika kilele cha siku ya ushindani Duniani.
Alisema endapo kampuni hizo zitazingatia matumizi sahihi ya matumizi ya hewa ukaa itasaidia kupunguza hewa ukaa inayochangia mabadiliko ya tabia nchi.
Alisema lengo la wafanyabiashara wote ni kupata faida hivyo lazima kuhakikisha ushindani wa haki unazingatiwa ikiwemo kuhakikisha mamlaka ya ushindani zinazuia ukiritimba katika biashara ikiwemo nguvu ya soko kuwameza washindani katika biashara.
Pia kudhibiti muingiliano wa biashara katika unaolenga kuwaweza washindani katika baadhi ya biashara na kuongeza kuwa ongezeko la mabadiliko ya tabia nchi unahatarisha usalama na uhatarishi wa theluji katika mlima Kilimanjaro.
“Wawekezaji katika sekta ya Viwanda,ndege na makampuni ya utalii kutumia teknolojia rafiki katika kudhibiti mazingira ikiwemo wanyama katika sekta ya utalii katika upunguzaji wa ikolojia ya wanyama ikiwemo ukataji ovyo wa miti ikiwemo mkaa ”
Alitoa rai kwa wadau mbalimbali kupanda miti ili kudhibiti uongezeko la hewa ukaa hivyo ni lazima miti ipandwe katika kulinda ikolojia ya wanyama sanjari na uoto asili
"Ili kuendelea kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ni vyema tukapanda miti Kwa wingi na Kila mmoja kumuhamasisha mwenzake kitokukata miti ovyo ili kuweza kudhibiti ongezeko la hewa ya ukaa"alisema
Naye Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani Tanzania (FCC),Dk,Aggrey Mlimuka Alisema kongamano hilo ni muhimu katika kuhakikisha kunakuwa na uendelevu na ushindani katika kuhakikisha utalii unakua kwa kasi sanjari na ulinzi wa mazingira
Awali Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Injinia Richard Ruyango alitoa rai kwa wadau mbalimbali katika sekta ya mazingira kuhakikisha mazingira yanalindwa ili kuzuia matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi na ikolojia.