SINGLE MAMA NI NANI
single mama ni yule mama amabaye analea mtoto au watoto mwenyewe bila ya kuwa na mchango wowote kutoka kwa baba
au unaweza kusema ni kile kitendo cha Kulea mtoto/watoto na mzazi mmoja jambo ambalo ni tatizo kubwa sana katika jamii
Mzazi mmoja kama amefariki hiyo haina jinsi lakini kama wote mpo hai kuna athari wanapata watoto
baadhi ya athari ambazo mtoto anaweza kuzipata ni pamoja na
- ukosefu wa maadili
- ukosefu wa mahitaji ya msingi kwa mama asiye kazi ya maana.
- ukosefu wa ushauri toka kwa baba
- ukosefu wa maisha bora
tumekuwa tukiona baadhi ya watoto wapo na maisha magumu sana mpaka wanashindwa kwenda shule sababu mama hana uwezo.
baadhi yao wanafikia hata hatua ya kujiingiza katika tabia za wizi, watovu wa nidhamu na hata mabinti wanaanza mapenzi wakiwa katika umri mdogo sana na wakiulizwa wanasema wamejiingiza kutokana na hali mbaya ya kiuchumi
wengi wao wamekuwa wakibainisha kuwa mama zao wanashindwa kuwahudumia na inabidi akubali kusaidiwa na watoto, ambao kwa umri wao hawakustahili.
NINI KINASABABISHA KUWA SINGLE MOTHER
-baadhi ya mambo yanayosababisha wanawake wengi kuwa single mother ni pamoja na uvumilivu kuwa mdogo kwa pande zote mbili yaani kwa baba na mama wa mtoto/watoto.
-kipindi cha nyuma bibi/mama zetu walikuwa wanavumilia mengi sana akiwa ananyonyesha basi hata amsikie mumewe ana mchepuko au aujue alikuwa hawezi kusema lolote kwa kuwa analea.
-kushidwa kuvumilia visa na vituko vingi sana toka kwa waume zao
-Na hata katika maisha yao kwa familia niliyotoka mie sijawahi kumsikia mama akihadithia uovu wa baba hata siku moja japo kwa shoga yake au kwa jirani,
Sio kwamba walikuwa hawakosani hapana lakini watoto tulikuwa hatujui saa ngapi wanagombana na saa ngapi wanapatana ,lakini wasasa wakigombana kidogo tu hadi mtaa wa tatu watajua
-Wenza wa sasa baadhi yao hawana maadili yaani ndoa zimekuwa ili mradi mmewaona viongozi wa dini ikapita dua basi lakini maisha mnayapeleka kama movie ya vichekesho.
-Hakuna mwenye amri na mwingine akatekeleza wote mafahari ndani ya zizi moja lazima mmoja atoke.
-Mdada ukiachana na mwenza wako unatamba nitamlea mwanangu na nitamtunza kwa hali yoyote nisimuone kuja mtaka mtoto, hizo huwa ni hasira na kutokuona mbele au kutothamini ubora wa mtoto.
-Pia wadada mnadanganywa kubeba mimba kwanza ndio akuoe ili aonekane kidume basi kama ana uwezo kidogo ndio utajiachia na kumwamini kuliko Mungu aliyekuumba matokeo hakuoi unabaki kulea mtoto na sometimes na matumizi asilete.
-unamwaminije mtu mliyekutana meno thelethini na ushee kinywani jamani ningewaona wa maana kama mngefunga hata mkataba kuwa asipokuoa umshitaki hivi hivi unaachia goli anafunga kweli?
ah wadada sometime akili zetu anajua aliyetuumba kwa kweli.
-hebu tuvumilie kwa ajili ya watoto ili wakue katika malezi mazuri na bora wakijitegemea wanapunguza mzigo kwa wazazi kuliko wakikosa elimu wakawa na tabia za ajabu kila siku mama polisi kwenda kumtolea mtoto dhamana kashikwa kwa wizi au ukahaba.