SHIRIKA LA CORDS LATOA MSAADA WA MAHINDI KAYA ZAIDI YA 300 ZINAZOKABILIWA NA NJAA LONGIDO

 



mwandishi wetu,Longido


Shirika la Utafiti, Maendeleo na Huduma kwa jamii( CORDS) jana limekabidhi tani 7.1 za mahindi kwa kaya 395 za vijiji viwili vya wilaya ya Longido mkoa wa Arusha ili kukabiliana na uhaba wa chakula.


Akizungumza wakati wa ugawaji mahindi hayo, ,Afisa idara ya miradi ya shirika la CORDS ,Martha Katau alisema wameamua kutoa mahindi ya msaada baada ya kubaini kaya nyingi zinakabiliwa na njaa.


"tumekuwa na miradi kadhaa hapa Longido, ikiwepo ya 0kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, lakini tumebaini kuna upungufu wa chakula kwa kaya nyingi na hivyo tumeona tusaidie walau kidogo"alisema


Alisema katika mgao huo, kijiji cha Ildonyo kaya 165 zimepatiwa tani 2.6 na kijiji cha Orpurkel Kaya 230 zimepatiwa tani 4.5 ili kusaidia kukabiliana na upungufu wa chakula.



Kaimu Afisa kilimo wa wilaya ya Longido, Mariam Fivawo alisema ukame umesabisha uhaba wa chakula katika maeneo mengi ya wilaya hiyo ambayo asilimia 95 ya wananchi ni wafugaji.


Hata hivyo, aliwataka wananchi wenye mifugo kujitahidi kuuza baadhi ya mifugo yao ili waweze kununua chakula cha bei nafuu ambacho tayari kimepelekwa na serikali katika wilaya hiyo.


Mmoja wa wanufaika wa msaada huo, Witness Alais alisema msaada huo wa mahindi utasaidia sana kukabiliana na njaa kwani licha ya kukosa chakula lakini pia hata maziwa ya mifugo hawana kutokana na mifugo mingi kufa kwa ukame na iliyobaki haiwezi kuzalisha maziwa kwa wingi.


"tunashukuru shirika la CORDS kwa kutupa msaada huu ambao utasaidia hasa akina mama na watoto ambao wanashida kubwa zaidi ya chakula"alisema



Shirika hilo pia wiki iliyopita lilitoa msaada wa mahindi tani 12 kwa kaya 553 katika vijiji vya Idonyonaado na Emuruwa katika kata ya Mfereji wilaya ya Monduli mkoa Arusha.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post