TUME ya Sayansi na Teknolojia ya vyuo vikuu COSTECH,imepongeza Chuo kikuu cha Dar es Salaam na Chuo cha ufundi Arusha kwa kuanzisha programu maalumu ya mafunzo ya ujasiriamali na biashara kwa wanafunzi wa shule za sekondari za mkoa wa Arusha ili kuwawezesha kuibua miradi itakayowawezesha kujiajiri baada ya kuhitimu masomo yao.
Pongezi hizo zimetolewa na Mkuu wa Ndaki ya Costech,Elasto Mnyuka kutoka Costec wakati akitunuku vyeti kwa wanafunzi na walimu wa shule hizo waliofanya vizuri katika kuwasilisha miradi yao ya ubunifu hafla iliyofanyika chuo cha ufundi Arusha ATC.
Amesema kupitia Programu hiyo ya Future Stay Business wanafunzi wameonyesha umahiri katika kuandaa ubunifu wa miradi ya kiuchumi ambapo wakimaliza shule watakuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki biashara zao kutokana na ubunifu wao .
Programu hiyo inashirikisha walimu, wanafunzi na wafanyabiashara ambapo wafanyabiashara wamekuwa wakiwaongoza na kusimamia ubunifu wa miradi husika inayoibuliwa ambapo wanafunzi hao hutumia taaluma yao ya kuwa bidhaa na biashara kwa kuzingatia kanuni za kisayansi.
Mnyuka,amesema kuwa, Programu hiyo ilianzishwa mwaka 2017 katika chuo kikuu cha Dar es Salaam,kwa kushirikisha shule tano za sekondari na sasa ipo katika chuo cha ufundi Arusha ambapo hushirikisha shule saba ikiwa ni kupanua programu hiyo ambayo inalenga kuzifikia shule zote za sekondari nchini.
Amesema Programu hiyo inawawezesha wanafunzi hao kuelewa changamoto za ajira na biashara na hivyo wao kupata suluhisho ambapo wanakuwa na uwezo mkubwa kuanzisha miradi mikubwa ya kiuchumi ikiwemo viwanda pindi wakihitimu elimu.
Awali Mkuu wa Chuo cha ufundi Arusha, Dokta Mussa Chacha, ametoa wito kwa shule za sekondari mkoani Arusha hasa zenye mchepuo wa Sayansi kutembelea chuo hicho ili kujifunza jinsi somo la Fizikia linavyofanya kazi kwa vitendo.
Amesema matatizo makubwa duniani ni maarifa sahihi ya kufanya jambo kwa vitendo hivyo ameshauri wanafunzi kupewe maarifa sahihi ili wayatafsiri katika vitendo na kuwawezesha kubuni na kuibua miradi ya kiuchumi.
Makamu mkuu wa Chuo hicho Dokt Yusufu Mhando,amesema mafunzo ya ubunifu yatawawezesha wanafunzi kuwaongoza kwenye ujasriamali na kuwa wabunifu kwenye biashara zao na hivyo kuboresha maisha hivyo amewaomba watembelee chuo hicho kwa kuwa ni taasisi ya maarifa.
Kwa upande wake Josephine sepeku meneja mradi wa FSBL-DTBi amesema kuwa, mashindano hayo yanawajenga wanafunzi kujiamini na kuwa wabunifu katika masomo ya sayansi ambapo amesema wanawajengea uwezo kufikia kujiajiri wenyewe
Josephine amesema wanafunzi hao wapatao 35 kutoka shule 7 za jijini Arusha walishiriki katika mashindano ya ubunifu hususani kuonyesha ubunifu wao katika vifaa mbali mbali ikiwa ni sehemu ya kutatua changamoto ya ajira nchini.
Amesema katika mashindano hayo wanafunzi watatu wamepatikana mara baada ya kushindana katika mashine walizo buni wenyewe ambapo mashine hizo zinasaidia katika mambo mbalimbali ikiwemo mashine za kutunza mazingira ambazo ni mashine rafiki katika mazingira .
Josphine ametoa wito kwa shule zingine kushiriki mashindano hayo kwani ni chachu ya ajira kwa vijana kuanzisha viwanda vyao wenyewe na kufikia serikali ya viwanda na costeck itaendelea kuibua vipaji vyao na kufikia malengo yao .