Mkurugenzi wa elimu sayansi na teknolojia Prof.Maulilo Kipanyula akizungumza katika mahafali ya 14 ya Chuo cha ufundi Arusha.
Na Woinde Shizza, ARUSHA
Chuo cha Ufundi (ATC) Arusha, kimetakiwa kufanya mageuzi makubwa ya mitaala ili kiendane na mahitaji ya soko kwa wahitimu ,ukizingatia kwamba dunia ipo kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda.
Hayo yameelezwa jijini Arusha na Mkurugenzi wa elimu sayansi na teknolojia Prof.Maulilo Kipanyula Mkurugenzi akizungumza katika mahafali ya 14 ya chuo cha Ufundi Arusha, ambapo jumla ya wahitimu 962 wa ufundi stadi ngazi ya ,Astashahada, Stashahada na Shahada wametunukiwa vyeti.
Amesema wizara ya elimu, sayansi na teknolojia inatambua mchango mkubwa unaotolewa na chuo hicho katika kuendeleza sekta ya ujenzi na teknolojia nchini kupitia ushiriki katika miradi mbalimbali ya serikali na kuzalisha wataalamu waliobobea wa ufundi stadi .
Ameongeza kuwa ,wizara ipo kwenye mchakato wa kufanya mageuzi makubwa ya elimu ,kisera na mitaala,hivyo ni vizuri chuo hicho cha ufundi Arusha kiendane na jitihada za wizara kufanya mageuzi ili yaendane na mahitaji ya soko.
“Mageuzi mtakayoenda kuyafanya mkumbuke kwamba dunia ipo kwenye mapinduzi ya nne ya viwanda muangalie mahitaji ya soko yanahutaji wahitimu wa aina gani,”amesema Prof Kipanyula.
Aidha amekipongeza chuo hicho kwa kukamilisha miradi mikubwa mitatu ya miundo mbinu ambayo ni bweni la wasichana lenye uwezo wa kilaza wasichana 428,hospitali ya tiba na kujifunzia ,madarasa na maabara.
Awali Mkuu wa chuo cha ATC Dk Mussa Chacha amesema kuwa chuo hicho kimeanza mradi wa ujenzi wa tawi la chuo hicho Kampasi ya Kikuletwa wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, unaofanyika kupitia mradi wa kujenga ujuzi kwa maendeleo na uingiliano wa kikanda katika Afrika Mashariki(EASTRIP).
Amesema kuwa ,mradi huo unaofadhiliwa na benki ya dunia utakuwa kituo cha Umahiri katika sekta ya nishati Jadidifu na tayari chuo kimesaini mikataba miwili na kampuni ya ujenzi na ujenzi huo umeanza.
Mwenyekiti wa bodi ya utawala ,Diana Mlambugi amesema bodi imekuwa ikifanya kazi kubwa kukabiliana na changamoto ya bajeti ya chuo kwa ajili ya miradi mbalimbali inayoathiri utekelezaji majukumu ya chuo.
Amemshukuru Rais Dk Samia Suluhu kwa kuendelea kukipatia fedha chuo ili kuboresha miundo mbinu yake kipitia fedha za maendeleo zilizowezesha kulipa moshahara ,mafunzo viwandani ,chakula cha wanafunzi na maendeleo ya chuo.
Mkuu wa chuo cha ATC Dk Mussa Chacha akizungumza katika mahafali hayo jijini Arusha