Ndoa za Utotoni ni nini?
Ndoa za utotoni ni pale msichana au mvulana wanapoinga katika ndoa wakiwa chini ya umri wa miaka 18 kwa kawaida, ndoa hiyo
huwa mmoja wapo kati yao amemzidi umri .
SABABU ZIPI UPELEKEA NDOA ZA UTOTONI
Zipo sababu nyingi zinazopelekea baadhi ya wanaume wenye umri mkubwa kutaka kuoa wasichana ,Mara nyingi hutokea Kwa sababu ya mila na tamaduni, mawazo ya kizamani juu ya wanawake na wanaume.
Wakati mwingine, wasichana huolewa kwa kuwa wamepata ujauzito (mimba)wakiwa wadogo , muda mungine kwa sababu ya shinikizo kutoka kwenye familia kuwataka waolewe kabla hawajapata mimba,wazazi pia wamekuwa wakiweka shinikizo kwa vijana kuingia katika ndoa kutokana na mila, au kwa vile wao ni maskini
MADHARA HUTOKEA KWA MABINTI WANAOOZESHWA MAPEMA
-Ndoa za Utotoni huathiri afya ya msichana,Kukwamisha msichana asiendelee kupata elimu, pia uleta uhasama baina ya familia na huondoa pia mwanamke furaha.
-madhara ya tokanayo na msichana kuacha kwenda shule kupata elimu nzuri husababisha kushidwa kupata kazi nzuri itakayomuwezesha kuendesha maisha yake
-Wasichana hupata mimba wakiwa katika umri mdogo kabla ya miili yao kuwa tayari na hii husababisha kuongeza hatari ya kupata maradhi na hata kifo,ambapo pia uwaweka katika hatari zaidi ya kupata magonjwa kama Ukimwi au magojwa yatokanayo na ngono, kwa kuwa hawajajengeka kikamilifu.
-Wasichana wana hatatari ya kufanyiwa ukatili kihisia ,kimaumbile kutokana na nguvu za kimahusiano zisizolingana kati ya msichana na mwanaume,pia hujikuta wamekatwa/wametengwa toka kwenye
familia zao, na marafiki zao ambao wapo bado shuleni.
-Wasichana wanaolewa katika umri mdogo,hawako huru kufanya
maamuzi yao wenyewe, Wana majukumu mengi katika umri mdogo ikwemo kuwa mama, kutekeleza majukumu ya nyumbani
na kuwahudumia waume zao, pia hawana mda wala uhuru wa kujiangalia wao wenyewe au kupanga mambo ya baadaye ,pia ndoa za Utotoni huwadhulumu wasichana utoto wao, na ndoto zao za baadae kwani kuchelewa kuolewa kwa msichana hadi kufika
utayari, kunamwezesha kuweza kufanya maamuzi yake katika maisha.
TUNAWEZAJE KUTOKOMEZA NDOA ZA UTOTONI
-Ili kutokomeza ndoa za utotoni tunatakiwa Watu wazima na vijana tufanye kazi kwa pamoja kwa kusaidia kubadili mtazamo na imani ndani ya jamii Kwa kupaza sauti Katika jamii dhidi kutokomeza Ndoa za Utotoni.
-Kuwathamini wasichana, na kuelewa kuwa wao wana haki ya kufanya maamuzi juu ya maisha yao ,hii ina maana kuwa kama livyo kwa wanaume na wavulana ,wasichana pia
wanaweza kuchagua kuolewa na nani au lini,pamoja na kuwa na haki ya kuamua nani wa kufanya nae ngono, wawe na
watoto wangapi, na kwa wakati gani pamoja na kuwa na haki ya kufanya ngono salama ya kutumia kondom Ili kujikinga na
magonjwa yatokanayo na ngono, pamoja na UKIMWI.
-Kutoa taarifa kwa walimu , wazazi, na viongozi katika jamii endapo kunaviashiria vya msichana kulazimishwa kuolewa.
-Kuwakumbusha watu wanaowalazimisha wasichana kuolewa, kuwa wanavunja sheria, na sheria itachukua mkondo wake dhidi yao,
Watu wazima ambao wanataka kutokomeza ndoa za utotoni, wameweza kubadi shera katika nchi nyingi na kulifanya suala la ndoa za utoton kuwa ni kosa la jinai wakishirikiana na mashirika yasio kuwa ya kiserikali pamoja vijana kuhakikisha kuwa sauti za wasichana zinasikika maamuzi muhimu yanafanyika, kama vile kubadilisha sheria na sera.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia