NDOA ZA UTOTONI ZINAVYOWAATHIRI WANAWAKE WA PEMBEZONI (MAASAI)



Picha na maktaba Mkono wa mtoto mdogo wa miaka 15 (jina limehifadhiwa) ambaye tayari ameolewa ambao ni moja wapo ya maeneo ya mwili aliyojeruhiwa baada ya kupigwa na mumewe, Namendea Lesiria

 Na Woinde Shizza , ARUSHA


Asilimia 31% ya wasichana nchini Tanzania huolewa kabla ya kutimiza umri wa miaka 18, kwa mujibu wa shirika la watoto la Umoja wa Mataifa Unicef


Mahakama ya juu zaidi Tanzania imebatilisha sheria inayoruhusu familia kuwaoza wasichana wadogo wenye umri wa kuanzia miaka 14.


Mahakama kuu ya rufaa imebatilisha uamuzi uliotolewa awali na mahakama nyingine nchini kwa misingi ya kuwa ndoa za watoto zinakiuka haki za wasichana, na nii kinyume cha sheria na katiba ya nchi .

Neema ni msichana wa miaka 14, baba yake alimwambia kuwa anataka Neema aolewe na mwanaume aliemzidi umri mbali na hilo pia alitaka aache masomo yake na kwenda kutumikia ndoa yake 

Baba yake Neema tayari alikuwa ameshapokea Ng'ombe sita Kwa ajili ya mahari ya Neema ndipo Neema alipojua hilo mara baada ya kugusiwa na mama yake aliamua kuwaambia walimu wa shule alipokuwa anasoma ndipo waliamua kumtorosha Neema na kuamua kumpeleka katika kituo ambacho kinalea mabinti waliokimbia kukeketwa pamoja na waliokimbia kuozeshwa mapema kijulikanacho Kwa jina la Health Integrated Multisectoral Development (HIMD)

Mbali na Neema pia Kuna Binti Mwingine aliejitambulisha Kwa jina la Sara Binti huyu alikuwa anasoma katika shule Moja ya msingi iliopo ndani ya jiji la Arusha yeye ana umri wa miaka 13 yeye alifukuzwa nyumbani mara baada ya kubakwa na baba yake wa kambo ambapo mara baada ya kufanyiwa kitendo hicho alipata ujauzito na Sasa anaishi katika kituo cha asasi isikuwa ya kiserikali inayowahifadhi mabinti waliokimbia majumbani kwao kutokana na kukimbia kufanyiwa ukeketaji pamoja na ndoa za utotoni( HIMD)na mtoto wake ambapo kituo hicho kumemsaidia na anaendelea na masomo yake ya shule ya msingi mara baada ya kujifungua

"Mimi nilikuwa na ndoto ya kusoma mama yangu alikuwa ameenda kwenye biashara zake nikawa nimebaki nyumbani na baba ndipo baba akaniingilia Kwa nguvu ,na nilipokuja kumwambia mama alikataa na kunifukuza na kudai namsingizia mume wake ,huku akinilazimisha nimtaje alienibaka ili wakaniozeshe nilivyosisitiza ni baba ndipo alipoamua kunifukuza adi navyoongea Sasa ivi ajui hata ninapoishi "alisema

 


ASASI ZISIZO ZA SERIKALI ZINASEMAJE



MARY BARNABA MUSHI wa mkurugenzi wa Shirika la Women and Children Welfare Support anasema kuwa ndoa za utotoni zimeonyesha zina adhari kubwa maana watoto wamekuwa hawana msemaji wa kuweza kuwapazia sauti ,wakuweza kukata vitendo hivyo ukilinganisha jamii zetu zimekuwa zikiangalia vitu ambavyo vinapelekwa katika familia ya muhusika na kufanya mtoto wa kike aonekane anadhamani yeye ni wakuolewa


Ndoa hizi zinasababisha mtoto wa kike kukosa elimu ,haki ya kujieleza kama yeye mtoto wa kike ,anakosa haki ya kufanya maamuzi yake binafsi maana maamuzi yote amekuwa akifanyiwa na wazazi wake na hii inapelekea mtoto wa kike kukandamizwa na kuonekana yeye hanamsaada wowote Kwa jamii


"Kuendelea kukandamizwa kuona mtu ana dhamani kwenye jamii haswa ukiangalia jamii za pembezoni kesi nyingi zimekuwa zikiripotiwa ni zile za unyanyasaji au ukatili wa kijinsia wengine wanapigwa na wengine wanaweza kusababishiwa majeraha au kufariki kutokana na kubeba mimba angalia mdogo na wakati wa kujifungua anaweza pia kupata athari zaidi za kiafya "alibainisha 


NINI KIFANYIKE


-SERIKALI ibadili sheria ya ndoa ilikuweza kutambua mtoto wa kike anapaswa kuwa ni anaethaminika kwenye jamii 

-sheria ya ndoa inayoongelea mtoto chini ya miaka 18 anaweza kuolewa irekebishwe kwani sio sahihi na asasi za kiraia ziendelee kupaza sauti na kuomba wanaharakati wengine waendelee nao kupaza sauti Ili sheria hii ibadilishwe


-sheria hii ikibadilika watu ambao wamekuwa wakiozesha au wanaosababisha wataacha mara moja maana watakiwa wanaogopa sheria kali ambayo itakuwa imetugwa na kuwekwa na serikali.


Naye Mratibu wa dawati la jinsia katika Shirika la Wanahabari la Kusaidia Jamii za Pembezoni (MAIPAC), Debora Makando ameiomba Serikali kuchukuwa hatua kali kwa vijana ambao bado wananyanyasa watoto pamoja na wale ambao bado wamekuwa wakiwaozesha watoto  na kuwafanyiwa ukatili ikiwepo kupigwa na kukeketwa.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post