BREAKING NEWS

Monday, December 19, 2022

DIT NA TEMDO WASAINI MAKUBALIANO YA KUSHIRIKIANA ILI KUZALISHA BUNIFU ZILIZO BUNIWA NA TAASISI HIZO KIBIASHARA





 Wakuu wa Taasisi ya usanifu na ubunifu mitambo ( TEMDO) na Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam(DTI)wakibadilishana mikataba mara baada ya kutia sahihi ya makubaliano ya kufanya kazi kwa kushirikiana kwalengo la kuendeleza na kuzalisha bunifu zilizo buniwa na Taasisi hizi kibiashara.

 Na Woinde Shizza , ARUSHA


Taasisi ya teknologia Dar es salaam (DIT) Kwa kushirikiana na Taasisi ya usanifu na ubunifu mitambo (TEMDO) wamesaini makubaliano ya kufanya kazi kwa kushirikiana kwalengo la kuendeleza na kuzalisha bunifu zilizo buniwa na Taasisi hizi kibiashara.



Taasisi ya DIT imekuwa ikifanya bunifu nyingi lakini zimekuwa zikishidwa kufanyiwa kazi kutoka kwenye natharia kwenda kwenye uhalisia hivyo mashirikiano hayo yatasaidia bunifu nyingi zilizowekwa muda mrefu kufanyiwa kazi kwani temdo wanawataalam wengi pamoja na mashine nyingi za kutengeneza bunifu hizo kwenda kwenye uhalisia



Akiongea wakati wa utiaji Saini katika makubaliano hayo mkuu wa taasisi ya DIT profesa Preksedis Marco Ndomba alisema kuwa makubaliano haya ni muharubaini wa Vifaa Tiba vya hospitali kwani wanazo bunifu zilizopo tayari ambazo zitazalishwa kibiashara kwenye karakana ya vifaa tiba ya Taasisi ya TEMDO kwani kwasasa ina zalisha vifaa Tiba vyenye Ubora na Viwango ulio dhibitishwa na MSD na TMDA


"Tukiambatana nao maana yake ni Kama wana tushika mkono kwenye mandeti kama watazikubali tafiti zetu tutakazo waletea hama tukikubaliana kuboresha bahadhi ya bunifu basi maana yake zinaweza kufika huko zinapo hitajika , tunatafiti nyingi sana tumefanya kama nilivyosema na zipo nyingi sana "alisema 


Aidha alisema kuwa pia wana bunifu nyingi sana za vifaa tiba walizozifanya hivi karibuni na kwakuwa temdo wamepata jukumu la kutengeneza vifaa tiba na wao bunifu walizonazo za vifaa tiba ni zile bunifu ambazo hatua zilizo fika tumeridhika nazo kwamba zinaweza kuendelezwa kirahisi na temdo na kuweza kuwafikia wananchi Kwa urahisi


Alisema kuwa katika taasisi yao wame anzisha chumba maalumu cha kuifadhi hizo bunifu lakini mara nyingi zinahishia pale kwasababu kwanza hawana vifaa machine zile za kuendeleza zile bunifu kama walizokuwanazo temdo pia hawana bahazi ya wataalamu ambao wanaoweza kuzipeleka hizo bunifu kwenye hatua ya kuendelezwa na kuweza kutumika Kwenda kutengeneza bidhaa ambazo zinaweza kutumika kwenye viwanda vidogo vya Kati na vikubwa .



Alibainisha kwamba vile vifaa tiba au binifu walizo nazo nizile za kuwafikia wananchi wa hali ya chini pia tunajaribu kuhakikisha kwamba teknologia zote ambazo zinaendelezwa pale nizile ambazo zinaweza kupatikana na wananchi hasa ni kwenye zile hospitali za mbali kama vijijini 


" Mimi na matumaini yangu kwamba sasa nina fikiri uhusiano huu ni muharubahini wa kuacha kununua vifaa tiba nje ya nchi ambapo hile tabia ya kuendelea kununua vifaa kutoka nchi za nje sasa nafikiri ndo mwanzo wa kuachana na bidhaa kutoka nje hapo awali tulikuwa tunanunua kwasababu tulikua hatushirikiani kwaiyo tulikuwa tunashindwa kupambana na watu wa nje lakini Kwa ushirikiano huu naamini kabisa tunamaliza tatizo la vifaa tiba "alisisitiza



Kwa upande wake mkurugenzi Mkuu wa TEMDO Mhandisi ,Profesa Fredrick Kahimba alieza kuwa makubaliano hayo yatasaidia watafiti wa TEMDO na DIT kufanya kazi za kitafiti Kwa pamoja ikiwa nipamoja na kubalishana Watalamu kwa lengo la kijifunza na kuwaongezea umahiri.



"kwahiyo hizi taasisi zimekutana kushirikiana kupata uzoefu walicho kuanacho wao sisi hatuna na tulicho nacho sisi wao hawana sio hawana kabisa nikwawingi au kwa ubora kama nilivyo sema awali kwamba taasisi ya teknologia ya sanifu na ubunifu mitambo inafamika kwa kuja na bunifu mbalimbali na nyingi Kwa ajili ya kumsaidia mwananchi"alisema Kahimba




Naye mwenyekiti wa bodi ya TEMDO Dkt Richard Masika aliwapongeza kwakuingia katika mashiriano hayo na kuwataka kufanya kazi waliokusudia Ili kuweza kuwasaidia wananchi na kuwasihi kutoingiza siasa yoyote katika makubaliano hayo ambapo pia aliwataka wawe vichocheo kwa ajili ya maendeleo ya viwanda hapa nchini .


 


 Na






Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates