Rose Jackson , Arusha
Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa kusheherekea miaka 50 ya Unesco ya mkataba wa urithi wa dunia wa mwaka 1972 utakaofanyika jijini Arush
Akizungumza katika semina ya wanahabari iliyoandaliwa na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro mkuu wa kitengo cha sayansi asilia kutoka shirika la umoja wa Mataifa linaloshulikia maswala ya elimu ,sayansi na utamaduni ofisi ya Dar es salaam ( Unesco) Keven Robert amesema kuwa Unesco kwa kushirikiana na mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro wameaandaa maadhimisho hayo ambayo yatafanyika desemba 12 hadi 14 jijini Arush
Alieleza kuwa wameandaa maadhimisho hayo ili kuleta nchi nyingine kuja kujifunza namna ambavyo tanzania imeweza kutekeleza mkataba huo
,"Unesco imeridhia maadhimisho haya kufanyika Tanzania kwa kuwa Tanzania ni nchi mwanachama wa Unesco aliyeridhia mkataba mwaka 1977 na pia imeweza kutekekeza mkataba kwa namna nzuri bila kuwepo changamoto hivyo kuoenekana Tanzania imeweza kufanya vizuri katika kutekeleza uhifadhi wa Mamlaka ya Ngorongoro"aliongeza Robert
Alisema kuwa maadhmisho hayo yanaleta wataaamu zaidi ya 50 kutoka nchi mbali mbali za Afrika ili kuangalia changamoto na mafanikio ya mkataba wa mwaka 1972 na kujifunza jinsi ambavyo Tanzania imeweza kuhakikisha hifadhi ya Ngorongoro inasimamiwa vizuri
Kwa upande wake kamishna msaidizi wa uhifadhi kutoka mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro mhandisi Joshua Mapunda amesema kuwa semina hiyo imetolewa kwa wanahabari ili kuongeza uwelewa kuhusiana na uhifadhi na mikataba mbali mbal
Alidai kuwa urithi wa dunia una faida nyingi lakini elimu imekuwa haiwafikii wananchi hivyo kupitia semina hiyo itaongeza uelewa juu ya uhifadhi na faida za mkataba wa Unesco ambao Tanzania umeweza kuitekeleza katika kuhifadhi na kuendeleza mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro