MATHARA YA UKATILI KIMTANDAO
Kama ilivyo kwenye aina nyinigine
za ukatili,ukatili wa mitandaoni una madhara mengi baadhi yake ni pamoja na
·
-Madhara ya kisaikolojia
Haya yanaweza kupele kewa
mtendewa kupata msongo wa mawazo na kusababisha kujiua au kupoteza mwelekeo katika
maisha.
·
Kupelekea wanawake hasa wanawake
watetezi kupoteza dira za harakati zao za utetezi wa haki za binadamu hususani haki
za wanawake ,watoto pamoja na makundi ya pembezo
·
Inajenga hofu na kuvunja moyo
kwa wanawake kushiriki kwenye ngazi za uongozi
na maamuzi wa kihofia kudhalilishwa na
kupoteza utu wao.
AELEZEA NINI KIFANYIKE
-Zaina Njovu alisema kuwa ni vyema jamii itoe ushirikiano kwa
wanawake waliodhalilishwa kwanza kwanza
wasiwatenge pili wasiwadhalilishe zaidi kwa
kusambaza maudhui hayo zaidi
-Serikali itunge
sheria ambazo ni rafiki na zimlinde mwanamke na udhalilishaji
-Serikali ielimishe
jamii juu ya madhara ya udhalilishaji na
uwepo wa hizi sheria za kulinda udhalilishaji mtandaoni
SHERIA INASEMAJE
·
Sheria zinazo linda na kuzuia
ukatili wa kijinsia mitandao ni pamoja na sheria ya maudhui ya mitandaoni(OnlineContentRegulation)
ya mwaka 2020 ambayo inakataza na kutoa adhabu ya kurusha maudhui ya udhalilishaji
zikiwemo picha au video za utupu ,lugha za udhalilishaji zinazo kwenda kinyume na
utamaduni wa Mtanzania.
·
·
Sheria ya Kimakosa ya Mtandao
2015 (CyberCrimeAct) ambapo kifungu cha 23 kinakataza na kupinga uonevu mtandaoni
kuwa nikosa kisheria kwa mtu yoyote Kufanya uonevu wa aina yoyote kwa kutumia njia
za kieleketroniki na kufanya hivyo nikosa kisheria,na yeyote atakayekutwa na kosa
hili atatumikia kifungo kisichozidi miaka mitatu jela au zaidi ama kulipa faini isiyo pungua millioni tano au
yote kwa pamoja.
KWANINI UKATILI YA KIMTANDAO UNAKITHIRI JAPO SHERIA ZIPO
*Sababu zi nazo pelekea ukatili
wa mitandaoni kuendelea kukithiri ni
pamoja na uelewa mdogo kwa wananchi juu ya sheria zinazo zuia na kukataza
Ukatili wa kijinsia mitandaoni.
*Hofu ya kuendelea kudhalilika
hasa pale kesi zinapo taka kwenda mahakamani.
*Tamaduni za jamii nyingi
kwenye mitandao kukaa kimya badala ya kukemea wanapo ona vitendo vya ukatili kwenye
mitandao vinaendelea
*Mapungufu katika utaratibu
waripoti kwa vyombo husika
NINI KIFANYIKE KUKOMESHA TATIZO HILI
-Kampeni za kupaza sauti na
kukemea ukatili wa kijinsia mitandaoni ziendelee na nguvu kubwa itumike kufanya kampeni hizo
-Watu wafundishwe kukemea
wanapoona mwanawake anafanyiwa au
amefanyiwa vitendo vya ukatili mitandaoni.
Muhanga au mtu yeyote
aliefanyiwa au alieona ukatili unafanyika kutoa taarifa kwa vyombo vya mamlaka
kama vile polisi na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) pamoja na vituo vya msaada
wa kisheria ili wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Kwa asasi zisizo za
kiserikali zinazohusiana na mambo ya kupinga unyanyasaji wa kijinsia waendelee
kuimarisha utekelezwaji wa Sheria ya
makosa ya mitandaoni
waendelee kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi sahihi ya mitandao.
TCRA WANAFANYA NINI ?
Jasmine Kiyungi ni afisa
kutoka kitengo cha mawasiliano na
uhusiano wa umma kutoka TCRA anaeleza kuwa wao wanatoa elimu kuhusiana na matumizi sahihi ya mtandano pia inaelimisha watu waweze kuepukana na utumiaji mbaya wa mitandao katika hilo wanatoa elimu yao kupitia sehemu mbalimbali ikiwemo redio
,magazeti,tv wana vipindi ambao wanavyo
lakini pia wanatoa elimu kupita
moja kwa moja .
Sheria ambazo
wanawachukulia wale watu ambao wanafanya vitendo vibaya mitandaoni anapo bainika jukumu la kufuatilia kesi lina hamia kwa
polisi ambapo kuna sheria ambazo zipo
ambazo zinafatiliwa ambapo
zinapofatiliwa yule mtu akikamatwa kuwa anahatia anachukuliwa sheria ambazo zipo kwa mujibu
kama zilivyokuwa zimewekwa .
Katika kudhibiti hili
wamekua wakitoa elimu kwa wanawake kutokuwa na mawasiliano na watu wasiowajua
kwenye mtandao , pia wanatoa elimu kwa vijana
na wanafunzi wa shule wajifunze
kutumia mitandano ya kijamii vizuri pia wajilinde kutowaamini watu wasio wajua mitandaoni
“tunaelimisha jamii yetu
awe mwanamke au mwanamme ajue kutumia mitandao ya kijamii vizuri ,tunakuwa na
kampeni kila baada ya miezi mitatu na
kwenye izo kampeni hatuachi kupitisha ujumbe juu ya matumizi sahihi ya mtandano
,tunaamini kwamba tukielimisha uma kwamba watumie mitandao ya kijamii vizuri
udhalilishaji utapungua “alisema Aica Bensoni afisa masoko TCRA
Habari hii imeandikwa na
woinde shizza wa libeneke la kaskazini
blog
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia