Ticker

6/recent/ticker-posts

KIGWANGALA AMJIBU LOWASSA


Mdogo wangu Fredrick Lowassa, tulia usiwe na hofu. Sikukurupuka kuhusu issue ya Mzee wako, Ndg. Edward Lowassa, kama ana kiwanja ama la, kwenye eneo la Plot No. 4091 Njiro Arusha.

Ukweli ni kwamba nilichokisema ni kuwa ‘tusubiri tupate majibu toka kwa mamlaka inayohusika na kutoa hati za umiliki wa ardhi kwa sababu kuna majina mengi makubwa yanasemwa, yakiwemo ya Mawaziri Wakuu wastaafu, Ndg. Frederick Sumaye na Ndg. Edward Lowassa, watumishi wa zamani wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro na Bodi ya Utalii Tanzania, kuna Mkuu wa Mkoa wa zamani Ndg. Ole Njoolay anatajwa, kuna Waziri wa Zamani Ndg. Batilda Buriani, Mkurugenzi wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Ndg. Mshana Joseph na wengine wengi, lakini hatuwezi kuwahukumu ama kuwataja waziwazi kwa sasa mpaka tupate nyaraka maana inawezekana wanasingiziwa ama vipi’.

Na nilisema kuwa ‘mtu anaweza kumtaja mtu mwingine kwa chuki ama kwa mazoea tu kuwa huyu huwa hakosi kwenye tuhuma za ufisadi wowote ule, lakini haimaanishi kuwa yumo kwenye ufisadi huu ama hayumo.’

Hii sidhani kama ni kutaja jina la Mzee wako. Tutulie tusubiri wenzetu wa ardhi wamalize uhakiki kisha watatuambia kwa mamlaka yao kamili kabisa!’

Naomba ufahamu hakuna dhambi kwa mtu kumiliki kiwanja, hata Mzee wako anayo haki ya kufanya hivyo ili mradi tu  amiliki kihalali na afuate taratibu tulizojiwekea kama nchi.

Dkt. Kigwangalla, Mb.,
WMU.

Post a Comment

0 Comments