TFC YAPAKIA TANI 200 ZA MBOLEA KUTEKELEZA AGIZO LA RAIS DK. JOHN MAGUFULI

 Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC), Salum Mkumba (kushoto), akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Premium Agro Chem Limited inayosambaza mbolea alipofanya ziara ya kikazi ya siku mbili jana na leo jijini Dar es Salaam kujionea zoezi la kusafirisha mbolea kwenda mikoani. Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa kampuni hiyo,  Brijesh Barot, Mkurugenzi Mtendaji,  Sagar Shah na Oparesheni Meneja, Rhoda Mwita.
 Wafanyakazi wa kampuni hiyo na Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakipakia mbolea hiyo kwenye gari tayari kwa safari ya kwenda mikoani.
 Malori ya JWTZ yakiwa katika foleni ya kupakia mbolea hiyo.
 Shehena ya mbolea hiyo ambayo inasafirishwa kwenda mikoani kwa wakulima
 Mbolea ikibebwa kuingizwa kwenye malori tayari kwa safari ya kupelekwa mikoani.
 Malori yakiwa katika foleni ya kupakia mbolea hiyo.

 Maghara ya kampuni ya Premium Agro Chem Limited yenye mbolea hiyo.

 Na Dotto Mwaibale


KUFUATIA agizo la Rais Dkt John Pombe Magufuli, kwa Wizara ya Kilimo, kuhakikisha ndani ya siku saba kumaliza malalamiko ya mahitaji ya mbolea kwa mikoa ya Katavi na Rukwa, Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC) imeanza mara moja kuteleleza agizo hilo. 

Waandishi wa Habari  jana na leo wameshuhudia watendaji wa TFC wakihaha kutafuta magari ya kukodi kwa ajili ya kusafirisha mbolea kuipeleka mkoani Rukwa na Katavi, ambapo zaidi ya tani 600 zimeanza kusafirishwa kuanzia juzi siku ya agizo hilo. 

Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TFC, Salum Mkumba, alisema mara baada ya taarifa ya Ikulu juzi, waliamua kuanza kupakia mbolea hiyo, kwa kutumia magari makubwa (malori) ya kukodi pamoja na magari makubwa ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ). 

“Kwa sasa sisi TFC hatuna akiba ya mbolea, lakini hawa wenzetu wa Primium Agro Limited, wanayo akiba ya kutosha, hivyo tunachukua kwao kwa makubaliano maalum,” alisema Mkumba. 

Mkumba aliongeza kusema kwamba, kutokana na uzito wa agizo hilo lililotolewa na Rais Magufuli, wameongeza nguvu ya magari, yanayoelekezwa mikoa ya Katavi na Rukwa, ambako mahitaji ya mbolea hiyo ni makubwa kwa sasa. 

Alisema nusu saa baada ya tamko la Rais Magufuli, alipokea taarifa kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Uwekezaji Charles Mwijage, akimtaka kuhakikisha wakulima kwenye maeneo husika wanatulia kwa kupokea mbolea. 

“Mbolea hii inapelekwa kwa wakulima kote nchini na itauzwa kwa bei elekezi ya szerikali, na ninawashukuru hawa wenzetu wa kampuni ya Premium Agro Limited kwa kuwa tayari kushirikiana kwa maslahi ya wananchi na Taifa letu,” alkisema Mkumba. 

Mkumba alisema wameamua kuingia makubaliano na kampuni binafsi ya Premium Agro Chem Limited, kupeleka mbolea hiyo kwenye maeneo hayo na mengineyo nchini yenye mahitaji, lakini akiamini kuwepo kwa unafuu kwenye maeneo mengine. 

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Primium Agro Chem Limited, Sargar Shah, alisema kwamba makubaliano na TFC ni kupakiwa kwa zaidi ya tani 1000 za mbolea hiyo kwenda katika mikoa ambayo wo hawana mawakala na kurahisha upatikanaji na pia kwa bei elekezi ya serikali. 

Meneja Biashara wa Primium Agro Chem Limited, ambaye kwa sasa ndiye anayesimamia zoezi hilo Brijesh Barot, alisema wamejiandaa vizuri kufanya kazi hiyo mchana na usiku kwa nia ya kufikia malengo ambayo serikali imeyahitaji. 

Barot alisema kampuni hiyo tayari kuanzia mwezi Septemba, imesambaza kwa wakulima kupitia kwa mawakala wao zaidi ya tani 19,500 za mbolea ya kupandia aina ya Urea, ikiwa kwenye ujazo wa kilo 25 na kilo 50. 

Barot aliongeza kusema kwamba, kampuni yake imeendelea kusambza na kuuza kwa wakulima mbolea zaidi kwa bei elekezi, licha ya kuwa tayari walimaliza kuuza tani 3,500 zilizoagizwa na serikali na kutakiwa kuuzwa kwa bei elekezi. 

“Sisi ni watanzania, wafanyabiashara wazalendo kwa nchi hii, hatutaki kufanyakazi kwa ajili ya kutafuta faida,badala yake tunaungana na Mheshimiwa Rais Magufuli, kuisaidia jamii kwa kufanya kazi ” alisema Barot.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post