Na Woinde Shizza,Nduruma
Wananchi wa kata ya Nduruma halmashauri ya Arusha wilayani
Arumeru wamejitoa kuchangia fedha za kujenga choo kwa ajili ya watumishi
wa kituo cha Afya Nduruma ambao wamehama kwenye nyumba hizo kutokana na
nyumba hizo kukosa vyoo.
Wananchi hao wamefikia uamuzi huo baada ya kuthibitisha tabu
inayowakabili watumishi hao wanaolazimika kuishi mbali na kituo hicho na
kusababisha utendaji wao kazi kulegalega jambo linalosababisha pia
upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi hao kusuasua.
Akizungumzia hatua hiyo Kaimu Muuguzi Mkuu halmashauri ya Arusha
Sista Agusta Komba amesema kuwa fadha hizo zimechangwa na wananchi wa
Nduruma, watumishi wa idara ya Afya kwa kushirikiana na shirika la
InGender Health na kupata kiasi cha shilingi milioni moja kwa lengo la
kufanikisha ujenzi wa choo hicho.