Ticker

6/recent/ticker-posts

MBUNGE MGIMWA AMEKABIDHI MIFUKO 400 YA SARUJI NA BATI 150 KWA AJILI YA UJENZI NA UKARABATI WA MAJENGO YA SHULE NA ZAHATI ZA KATA YA MAPANDA


Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa na diwani wa kata ya Mapanda Obed Kalenga na mwenyekiti wa kijijicha Ihimbo wakati wa kueleza vitu gani ambavyo amevifanya kwenye kata hii kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wa kata ya Mapanda
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa kwenye moja ya darasa ambalo litakarabatiwa kutumia mfuko wake wa jimbo ili liwe kwenye kiwango kinachotakiwa
Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa  akiwa na viongozi mbalimbali wakikagua majengo ya shule na kuangalia majengo yapi yanastahili kukarabatiwa
 Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa akiwa kwenye moja ya zahati ambayo inatakiwa kufanyiwa ukarabati ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa kata ya Mapanda

 Na Fredy Mgunda,Mufindi.

Mbunge wa Mufindi Kaskazini Mahamoud Mgimwa   amekabidhi  jumla ya mifuko ya saruji 400 na bati 150 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa madarasa ya shule za msingi pamoja na zahati za Kata ya Mapanda kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo, alisema kuwa niliomba kuwa mbunge kwa lengo la kuwatumikia wananchi hivyo najitahidi huku na kule kuhakikisha natimiza azma yangu ya kuleta maendeleo kwa wananchi wa jimbo la Mufindi Kaskazini.

“Nimetoa jumla ya mifuko ya saruji 400 na bati 150 kwa ajili ya kuhamasisha ujenzi na ukarabati wa madarasa katika shule na zahati za kata hii ikiwa ni mwamzo tu nitaendelea kutoa saruji nyingine na bati hata vitu vingine ili kulifanya jimbo la Mufindi Kaskazini kupata maendeleo kwa kasi” alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa halmashauri ya Mufindi imeshaanda mpango kabambe ambao utakuwa msaada mkubwa kuchochoe maendeleo kwa kasi huku serikali ikiendelea kufanya jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata maji ya kutosha na kuitumia vizuri ardhi ya halmashauri hiyo kwa kufanya maendeleo.

“mimi lengo langu inapofika kipindi cha uchaguzi ninakuwa nimetatua kero zote za wananchi na kujihakikishia napewa ridha ya kuongoza kipindi kingine kwa maendeleo ya wananchi wa jimbo la mufindi kaskazini na kuongeza kuwa hatakusikia kuwa kuna kitu kinasababisha migogoro ya kugombea ardhi katika jimbo hili la Mufindi Kaskazini” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa alisema kuwa shule na zahanati zilizopata saruji na mabati ni shule za kijiji cha Mapanda,shule ya kijiji cha Uhafiwa,Ukama,Ihimbo na Chogo lengo ni kuchochoe kuleta maendeleo kwa wananchi.

Mgimwa amewapongeza wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo katika kata na ametoa ahadi ya kuendelea kushirikiana kwa kuchangia ujenzi wa shule zote za jimbo la Mufindi Kaskazini na kutatua kero nyingine za wananchi wa jimbo hilo.

Obedi Madembo, Peter Kaguo, Kristopher Ngunda,Thobias Luvinga na Fransisco Mfaume ni wenyeviti wa vijiji vya kata ya Mapanda walimpongeza mbunge huyo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwatafutia wananchi mandeleo kwa kutumia nguvu zake zote.

“Hata ukiangalia mwandishi utagundua gharama alizozitumia mbunge zimewaondolea wananchi kuchangia kabisa hivyo bila mbunge huyu mzigo wote huu ulikuwa unawaangukia wananchi wa vijiji vyote vya kata ya Mapanda” walisema wenyeviti wa vijiji vya kata ya Mapanda

Kwa upande wake diwani kata ya Mapanda Obed Kalenga alimshukuru kwa kazi kubwa aliyoifanya na kuwataka wananchi kuendelea kumuunga mkono mbunge huyo ili andelee kufanya kazi ya kuwatafutia maendeleo wananchi wa kata ya Mapanda na jimbo la Mufindi Kaskazini kwa ujumla.

“Wananchi kweli wananjitoa sana kufanya kazi za kuleta mandeleo hiyo wanapoona kuwa mbunge naye anatumia nguvu kubwa kufanya maendeleo kutaongeza chachu ya kufanya kazi kwa kujitolea kwenye shughuli za kimaendeleo hata mchakato ulivyokuwa hadi kupelekea kushirikiana na wananchi kuanzisha ujenzi na ukarabati wa shule na zahati ili kuendelea kutoa elimu bora kwa wanafunzi wa kata hiyo na kupatikana kwa huduma za afya bora kwa wananchi wote” alisema Kalenga

Post a Comment

0 Comments