wafanya biashara wakiwa wametandaza bithaa zao chini hadi katika njia ya magari kitu ambacho kimekuwa kero kubwa kwa watembea kwa miguuu pamoja na waendesha magari kwani wamekuwa wakipita kwa shida katika barabara hiyo ,huku watu wanaotumia vyombo vya moto kutokupita kabisa katika barabara hiyo ambayo ipo katikati ya jij la Arusha (picha na Woinde Shizza)
Na Woinde Shizz,Arusha
baadhi ya waanchi wanaotumia vyombo vya moto pamoja na wale wanaotembea na miguu katika baadhi za barabara za jiji la Arusha wamelalamikia kitendo cha wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) kutandaza bidhaa zao hadi katikati ya barabara .
Wakiongea na mwandishi wa habari hizi wamesema kuwa kunabaadhi ya barabara ikiwemo ya mtaa wa majengo iliopo katika jiji la Arusha pamoja na fres kona imekuwa kero kupita kutokana na wamachinga kutandaza bidhaa zao hadi barabarani kitu
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha kwa jina la George Saleu alisema kuwa wamachinga hawa haswa wanaouza bidhaa zao katika barabara ya fresi kona wamekuwa kero kwani wanatandika bidhaa hadi katika barabara kitu ambacho ni hatari hata kwa usalama wao
"unajua ukiangalia kama pale freskona unakuta mama ametandika vitu adi barabarani yaaani kanakwamba gari ikikosea kidogo tu inawagonga ,yaani kibaya zaidi awajali hata usalama wao kweli mimi napenda kuwaambia wabadilike na pia serikali jamani itusaidie angalau wawekewe mipaka ya kukaa barabarani"Alisema Saumu Juma
Aidha waliwataka viongozi kuangalia jinsi ya kuwasaidia wafanya biashara ili wasipate matatizo