KAYA 3,894 KUPATA HUDUMA ZA AFYA KATIKA KITUO CHA AFYA NDURUMA

 Na Woinde Shizza

Takribani kaya 3,894 zenye wastani wa watu wa tano kwa kaya katika halmashauri ya Arusha wilayani Arumeru zinategemewa kunufaika na huduma za afya mara baada ya upanuzi wa miundo mbinu ya kituo cha Afya Nduruma kukamilika.

Akizungumza na mwandishi wetu Mganga Mkuu Halmashauri ya Arusha Dkt. Omari Sukari amesema kuwa mara baada ya kituo hicho kukamilika kinategemea kuhudumia zaidi ya watu 14,000 na kaya 3,894 kutoka kata ya Nduruma na kata za jirani za Mlangarini na Bwawani na vijiji jirani vya mkoa wa jirani wa Manyara.

Idadi hiyo ya watu inatokana na kata hizo kutokuwa na kituo kingine cha Afya na kuongeza kuwa kituo hicho ni mkombozi kwa wananchi wa maeneo hayo kwa kuzingati uhitaji wa huduma za afya kwa jamii.


Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post