BILIONI 2 ZATUMIKA KUBORESHA SEKTA YA AFYA MKOANI ARUSHA

Baadhi ya mafundi wakiwa kazini kwenye ujenzi wa kituo cha afya Nduruma,wilayani Arusha.
Katika kutekeleza maelekezo ya uboreshaji  na  ukarabati wa vituo vya afya nchini, Mkoa wa Arusha amefanikiwa kuboresha vitua vya afya viwili kwa awamu ya kwanza.


Akitoa taarifa fupi ya maendeleo ya ujenzi wa vituo hivyo,Mganga mkuu wa Mkoa Dr.Vivian Timothy Wonanji, amesema mpaka sasa kwa mkoa wa Arusha zoezi hili linaendelea vizuri na kwakasi kubwa.

Awamu ya kwanza, Mkoa ulipata kiasi cha bilioni 1.4 kwa ujenzi wa vituo viwili vya afya,ambapo ni kituo cha afya cha Nduruma kilipata kiasi cha shilingi milioni 500 kwaajili ya ujenzi na milioni 200 kwaajili ya ununuzi wa vifaa na kituo cha afya cha Kambi ya Simba kimepata milioni 500 kwaajili ya ujenzi na milioni 200 za ununuzi wa vifaa.


Amesema kituo cha fya cha Nduruma kilichopo katika halmashauri ya Arusha kinaendelea na ujenzi wa majengo matano na mpaka sasa yapo katika hatua ya ukamilishaji,majengo hayo yakiwemo wodi ya wazazi na jengo la upasuaji.


Kituo cha pili ni Kambi ya Simba kilichopo katika Wilaya ya Monduli, ambapo mpaka sasa ujenzi unaendelea wa majengo nane yakiwa kwenye hatua ya upauwaji.

Aidha,amesema katika awamu ya pili ya ujenzi wa vituo vya afya, mkoa wa Arusha umeshaanza maandalizi yake kwa uundaji wa kamati mbalimbali zakusimamia shughuli nzima na kiasi cha shilingi bilioni 1.2 zimeshatolewa na benki ya dunia kwa ujenzi wa vituo vya afya 3 .

Wilaya ambazo zimepata fedha hizo ni, Wilaya ya Ngorongoro katika ujenzi wa kituo cha afya cha Sakala, Wilaya ya Monduli kituo cha afya cha Mto wa Mbu na Wilaya ya Longido ujenzi wa kituo cha afya cha Engarenaiobor,ambapo kila kituo kitapatiwa kiasi cha shilingi milioni 400.


Pia, serikali imetoa fedha za ukarabati wa vituo vya afya mkoani Arusha, kikiwemo kituo cha afya cha Murieti,kimepata kiasi cha milioni 700.
                                                                
Kituo vingine ni kituo cha afya cha Usa liver ambacho kimepata kiasi cha shilingi milioni 700 kwaajili ya ukarabati wa chumba cha upasuaji kwa wakinamama.

Kituo cha afya cha Ololiendeki wilayani Longido nacho kimepata kiasi cha milioni 700 kutoka serikalini.
 
Dokta Wonanji amesema, mpango huu wa ukarabati wa vituo vya afya kwa mkoa wa Arusha, awamu ya kwanza vituo  vya afya 2 vimeweza kunufaika, na awamu ya pili utakamilishwa kwa ukarabati wa vituo vya afya 6 na kupelekea mpango huu kukarabati vituo vya afya 8 kwa mkoa mzima wa Arusha.

Mpango huu wa ukarabati wa vituo vya afya upo katika awamu mbili,yakwanza ilianza rasmi Septemba,2017 na utakamilika Januari,2018,ambapo awamu ya pili umeanza Januari 2,2018 na utakamilika Aprili,2018.

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post