Shirika
la Umeme Tanzania (TANESCO) tunautaarifu Umma na Wateja wetu wote kuwa, tumetoa
muda wa siku nne (4) kuanzia Januari 12, 2018 hadi siku ya Jumatatu Januari 15,
2018 kwa wadaiwa sugu wawe wamelipa madeni yao.
Baada
ya muda huo kuisha Shirika litasitisha Huduma ya umeme dhidi ya Wateja
watakaoshindwa kulipa madeni ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua zingine za
kisheria.
Ofisi
za TANESCO zitakuwa wazi siku ya Jumamosi Saa 3:00 Asubuhi hadi Saa 9:00
Mchana.
mawasiliano
Kituo
cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985
100
Tovuti: www.tanesco.co.tz,
mitandao ya kijamii:
Mitandao
ya kijamii
Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,
Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/
IMETOLEWA
NA: OFISI YA UHUSIANO
TANESCO
MAKAO MAKUU
JANUARI
11, 2018