MBUNGE MGIMWA NIPO TAYARI KUNYIMWA KURA KATIKA UCHAGUZI WA MWAKA 2020

Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa aikiongea na baadhi ya walimu wa shule za sekondari na shule za msingi jinsi gani ya kutatua kero zilipo shuleni ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi
Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa  akiwakabidhi zawadi ya mbuzi kwa walimu wa shule za msingi waliofanya vizuri katika moja ya kata iliyopo jimboni kwake.

Na Fredy Mgunda, Iringa

Wananchi wa jimbo la Mufindi kaskazini wametakiwa kuwapeleka watoto wao shule kwa lazima kwa kuwa elimu inatolewa bure na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe Mafuli kwa lengo la kuhakikisha kila mwanafunzi wote waweze kupata elimu na kuondoa ujinga na kuleta maendeleo kwa taifa.

Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahamuod Mgimwa alipokuwa kwenye ziara ya kukagua miundombinu ya shule zilizopo katika jimbo hilo ili kuweza kuzitatua changamoto zilizopo katika maendeo hayo.

Akiwa bado yupo kwenye ziara hiyo mbunge huyo aligundua kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwanzo cha kuwapeleka shule watoto wa hivyo akawataka viongozi wote wa serikali za vijiji kuwa chukulia hatua wazazi ambao hawatawapekeka shule watoto wao.

Mgimwa alisema kuwa yupo tayari kunyimwa kura na wananchi ambao atawachukulia hatua za kisheria kwa kutowapeleka shule watoto wao  kwa ajili ya faida ya maisha yao.

“Nasema kweli nitakubali kuachia ngazi ya kuwa mbunge kwa kunyimwa kura za wananchi wasiopenda maendeleo ya watoto wao,hadi sasa shule zimefungua lakini wazazi hawawapeleki shule watoto nitahakikisha wanachukuliwa hatua za kisheria” alisema Mgimwa

Aidha Mgimwa alisema kuwa sasa imefika mwisho kwa watoto wa jimbo la Mufindi Kaskazini kuwa soko la wafanyakazi wa kazi za ndani wakati wanauwezo wa kuwa viongozi hapo baadae.

“Nasema tena haiwezekani kila mfanyakazi ukifika daresalaam utasikia katoka Iringa jimbo la Mufindi Kaskazini sasa sitaki kusika swala hilo na wazazi wanaofanya hivyo nitawachulia hatua za kisheria serikali ya awamu ya tano inataka kuwa na wasomi wengi ili kuasaidia maendeleo ya nchi”alisema Mgimwa

Mgimwa alisema kuwa wazazi wa jimbo la Mufindi la Mufinda watafungwa kwa kuwapeleka watoto wao kufanya kazi za ndani pindi wamalizapo shule ya msingi au sekondari kufanya hivyo kunadumaza maendeleo yao.

“Haiwezekani mwanafunzi amefaulu halafu mzazi anampeleka kufanya kazi za ndani siwezi kukubali hata kidogo maana nimegundugua wazazi wengi hawapendi watoto wao waendelee kusoma badala yake wanataka wakafanye kazi za ndani narudia kusema mtoto akifaulu asipopelekwa shule nitamchulia hatua za kisheria huyo mzazi” alisema Mgimwa

Mgimwa aliwataka wanafunzi wakike kuacha kufanya ngono wakiwa na umri mdogo ili kupunguza mimba za utotoni na kupoteza dira ya maisha wakiwa watoto wadogo na kufanya hivyo kutawapelekea kufungwa jela kwa kuwa sheria itachukua mkondo wake.

“Acheni kufanya tendo la ndoa mkiwa na umri mdogo ili baadae mjenge maisha yetu viongozi wengine wa wanawake wanavyofanya kazi serikalini na kwenye mashirika mbalimbali ya nje ya nchi na ndani ya nchi”alisema Mgimwa

Mgimwa aliwapongeza walimu wa shule za msingi za jimbo la Mufindi Kaskazini kwa kuendelea kufanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa na kuendelea kuitangaza vizuri jimbo hilo kupitia elimu.
“Kwa kweli nisiwe mnafiki nichukue fursa hii kuwapongeza walimu kwa kufanya vizuri maana kila mwaka elimu inazidi kukua katika jimbo la Mufindi Kaskazi na kuendelea kuitangaza kitaifa” alisema Mgimwa

nao baadhi ya walimu wakuu wa shule zilizopo jimbo la Mufindi Kazskazini walisema kuwa wazazi wengi wamekuwa kikwazo cha maendeleo ya wanafunzi kwa kuwakatisha tamaa juu ya umuhimu wa elimu.

“Hapa katika kata hii ya Kibengu wazazi wengi hawapendi watoto wao kwenda kusoma kwa kuwa watakuwa wanapunguza nguvu kazi zao mashambani ndio maana hawawapatii mahitaji muhimu ya kuwasaidia wanafunzi kusoma kwa uhuru” alisema walimu

Walimu walimuomba mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kutafuta wataalam wa saikolojia kuja kuwapa elimu wazazi ili kukuza taaluma kwa wanafunzi wa kata hiyo.

“Ukiangalia hali ya ufaulu wa shule hizi ni mzuri lakini kutokana na wazazi kutokujua umuhimu wa elimu wamekuwa hawawapeleki watoto wao sekondari wakifaulu mitihani ya shule ya msingi hivyo inapelekea upungufu wa wanafunzi katika shule ya sekondari ya Ilogombe” alisema Walimu.

Mfikwa alisema kuwa wamekuwa wakiitisha mikutano ya mara kwa mara lakini bado tatizo kubwa hivyo jitihada zinahitajika kukomesha tabia hiyo kwa kuwa bila hivyo watoto wa kata hiyo wataendelea kuwa wafanyakazi za ndani tu

Zakayo Kilyenyi ni diwani wa kata ya Kibengu alikiri kuwa wazazi wengi wa kata hiyo hawana elimu juu ya umuhimu wa kujua dhamani ya elimu katika maendeleo ya familia zao na taifa kwa ujumla.

“Kweli kabisa wazazi wa kata ya Kibengu wamekuwa wakiwaambia watoto wasifanye mitihani vizuri ili wasifaulu kwa kuwa wakifaulu watakuwa na gharama kubwa ya kuwasomesha hivyo wakifeli wataenda kuwafanya kazi za ndani na ndio furaha kwa wazazi wa kata ya Kibengu” alisema Kilyenyi

Kilyenyi alisema kuwa uongozi wa kata ya Kibengu utaendelea kutoa elimu kwa wazazi hao ili kurudisha morali ya kuendelea kuwapa mahitaji muhimu yanayohitajika shuleni kwa kwa lengo la kuboresha maisha ya watoto hao.

“Zana potofu zimekuwa kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya wananchi wa kata ya Kibengu hivyo tukiondoa zana hiyo elimu itakuwa kwa wanafunzi wa kijiji hichi” alisema Kilyenyi

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post