‘’Ukosefu wa
elimu sahihi ya matumizi ya intaneti pamoja na
udhalilishaji wa kimtandao kwa wanawake ni moja kati ya
mambo yanayochangia kundi hili kutokuwa na uwiano sawa na
wanaume katika utumiaji wa kimtandao hali inayodidimiza haki yao ya
kushiriki katika mitandao hiyo kikamilifu .’’
Kundi
la wanawake wenye ulemavu ,wanasiasa , wanawake
walio vyuoni na wanaharakati ndio waathirika
zaidi wa uzalilishaji kutoka katika mitandao ya kijamii kutokana na
uelewa mdogo na namna ya kujilinda na kutumia nyenzo hiyo.
Utafiti mdogo uliofanywa na Taasisi
isiyokuwa ya kiserikali ya Zaina Foundation katika mwaka 2022 ulionyesha
kuwa kati ya wanawake na wanaume katika maswala ya
utumiaji wa teknolojia idadi ya wanawake wanaotumia mitandano
ya kijamii ni ndogo na asilimia 18% tu ya wanawake ndo wanatumia
Kukuakwa Teknolojia
ya kidigitali pamoja na mlipuko
waungonjwa wa UVIKO19 umechangia
mabadiliko
ya mfumo
wakufanyakazi baadhi ya watu wamekuwa
wakitumia teknolojia ya TEHAMA
na mitandao kama
sehemu za kupata taarifa kukuza
biashara zao,kufanya kazi na mawasiliano kwa ujumla, hata hivyo, kwa upande mwingine ukuaji wa mitandao
na
matumizi ya TEHAMA yanaongeza
vitendo vya ukatili
wa kijinsia kwa kasi
kubwa zaidi
Ukatili wa Kijinsia mtandaoni
ni aina ya udhalilishaji
Ambao unafanyika kwa njia
ya mitandao na ukatili huu
Ni pamoja na kuwepo kwa lugha
za matusi,kejeli,picha
Au video za utupu.
Ukatili huu umekuwa ukiwa athiri wanawake ,wasichana, viongozi wanchi,
wasanii pamoja na wanawake watetezi wa haki za wanawake na watu maarufu kwa
ujumla,kutoka na udhalilishaji huo umepelekea
wanawake watetezi kunyamazishwa na kupunguza kasi zaoza kutumia majukwaa ya mitandaoni kwa kuhofia kupoteza utu wao na kupewa majina
mabaya ya udhalilishaji , Mara kadhaa udhalilishaji huu umekuwa ukifanywa na wanaume
ambao takwimu yao inaonesha kuwa watumiaji wakubwa wa mitandao kuliko wanawake.
MUHANGA WA UDHALILISHAJI WA KIMTANDAO AFUNGUKA
Rehema ni binti wa chuo
kimoja apa mkoani Arusha (jina limeifadhiwa ) anasema kuwa yeye alikubwa na janga la kuzalilishwa katika mtandao
Anaeleza kuwa alikuwa na
mpenzi wake ambaye ilifika mahala
walishidwa kuendelea na mahusiano kutokana na sababu mbalimbali lakini
kwakuwa mwanaume yule alikuwa ajakubaliana na swala la kuachana ndipo akaamua
kumzalilisha kwenye mitandao kwa kutuma picha zake za utupu ambazo walikuwa
wakitumiana kipindi walipokuwa wapenzi
‘’kipindi cha mapenzi
yetu tulikuwa tunatabia ya kupigana picha kutumiana picha pale mmoja wapo anapokuwa mbali na
mwenzake wakati nafanya hivyo nilikuwa sijui kama kunasiku picha hizo hizo
zinaweza kutumika kunizalilisha ila
nilikuja kujuta wakati yule mwanamme ameamua kutumia picha zile kwani
nilizalilika ikanifikia mahali ata masomo yaliniendea vibaya kwani nilikuwa
kila nikifika chuoni kila mtu ananitolea macho mimi ‘’
Niwasihi tu wanawake
wenzangu wawe makini sana pindi wanapokuwa na wapenzi wao na wajiadhari sana
na na picha wanazopiga kipindi wapo
katika mahusiano pia sikwenda kushitaki
au kuripoti kokote kwa kuofia kuwa ninapoenda kuripoti basi nitaendelesa
kujizalilisha na taarifa hizi zitazidi kusamba “lifafanua
ASASI ZISIZO ZA
KISERIKALI ZAONGEA
Zaina Njovu ni mkurugenzi
wa asasi isiokuwa ya kiserikali inayojishughulisha na kutoa elimu kwa wanawake
juu ya matumizi salama ya mtandao (Zaina Foundation) anaeleza kuwa wanawake wanafanyiwa zaidi ukatii kwa otofauti
kulingana na makundi yao,uku akibainisha
kuwa wanawake wanasiasa ndio wanadhalilishwa zaidi zaidi mtandanoni kulinganishwa na wasio wanasiasa
Alienda mbali zaidi na
kubainisha kuwa pia kundi lingine linalo
zalilishwa ni kundi la wanawake walemavu
na hawa wanadhalilishwa kutokana na hali yao ,ambapo alifafanua kuwa katika
makundi haya ya wanawake wanaodhalilishwa mtandaoni asilimi 80% hawashitaki popote kutokana na sababu mbalimbali.
Anaenda mbele zaidi na kubainisha kuwa sababu inayowafanya wanawake hawa wasishitaki ni pamoja na kutokuwa na elimu ya ufahamu kuwa wanatakiwa kushitaki pili wanawoga kuwa akishitaki anaweza kuuwawa au ahata kujeruhiwa na wahalifu hao mwisho wanawoga wa kudhalilika zaidi baada ya kuripoti.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia