"Idadi ya wanawake wanaomiliki ardhi nchini ni ndogo sana nahii inasababishwa na baadhi ya mitizamo ya jamii pamoja na mila na desturi zetu"
Kwa mujibu wa takwimu za serikali zilizofanywa mwaka 2016 zinaonyesha kwamba ni asilimia 19% tu ya wanawake ndio ambao wanamiliki ardhi wakati wanawake hawa hawa ukiangalia asilimia 54% ya wazalishaji katika kilimo ambao ni uti wa mgongo wan chi yetu ni wao .
NINI KINASABABISHA WANAWAKE WENGI WASIWEZE KUMILIKI ARDHI
-Mila ,tamaduni na desturi
Hii ni kati ya sababu kubwa zinazochangia wanawake wengi kutokumilikishwa au kutokumiliki ardhi kwa wanawake pia mila hizi zinakandamiza mfumo mzima wa maisha ya wanawake na kuwanyima ushiriki katika maamuzi ya familia, jamii na hata umiliki wa mali na rasilimali,aidha zimekuwa zikitoa mwanya kwa wanaume kuwa na sauti kubwa katika jamii, hivyo kuwakandamiza wanawake katika misingi ya kupata haki sawa na wanaume.
-kutokuwa na elimu
Wengine wanasema sababu inaowapekea wanawake wengi kutomiliki ardhi ni kutokana na wengi wao kutokuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na haki yao ya msingi ya kumiliki ardhi na hivyo ndio inapelekea wanaume kutotoa kipaumbele katika kuwaandikisha kwenye hati mara tu wanaponunua kiwanja au eneo jipya.
-wanawake wengi kutokujiamini
Wanawake wengi wamekuwa hawajiani katika utendaji kazi hivyo ndio sababu inawapelekea wao kunyanyaswa na kunyimwa haki zao za msingi na iwapo basi wanawake wataamua kujiamini wataogopewa ,wataaminiwa na watakuwa na uwezo wa kudai haki zao za msingi kama vile kumilikishwa ardhi
WAADHIRIKA WAONGEA
Salome ni muathirika mkubwa wa madhara ya wanawake kudhulumiwa haki ya kumiliki mali na ardhi kutokana na madhila na machungu aliyopitia, baada ya ya kumpoteza mume
“Sikuwa najitambua, sikufahamu wapi nitapata haki zangu na nini cha kufanya, lakini kupitia mafunzo ya haki ya kumiliki ardhi kwa wanawake, utawala bora, uwajibikaji katika jamii na usawa wa kijinsia, nimeweza kutambua thamani yangu na nafasi yangu kama kiongozi wa familia na jamii ,awali wanawake hawakupata kufikiria kuwa viongozi wala kugombea nafasi za uongozi,pia nimeweza kuwa mwerevu na jasiri katika maswala haya
‘Kulikua na dhana kwamba uongozi ni mojawapo ya majukumu ya wanaume, Watu hawakuamini katika uwezo wa wanawake kuongoza, hoja na mawazo yao yalipuuzwa,jambo hili lilichangia kudhoofisha kujiamini kwa wanawake lakini kutokana na mafunzo na elimu mbalimbali tunazopatiwa na watu mbalimbali zikiwemo asasi za kiraia yametubadilisha
Ukiangalia zamani haikuwa rahisi kwa wanawake kurithi ardhi kutoka kwa wazazi na waume zao, ilikuwa kawaida kwa familia na jamii kumteua mwanaume kusimamia mali na ardhi kwa niaba ya mwanamke, kwa sababu wanaume walithaminiwa zaidi kuliko wanawake lakini sasa ivi wanawake wameamka na kutambua kwamba wote tupo sawa, na kwamba mwanamke ana haki ya kumili ardhi kama ilivyo kwa mwanaume, majukwaa ya ardhi ya wanawake, yamewasaidia kwa kiasi kikubwa, Ni sehemu ya kujadili na kutafuta ufumbuzi wa masuala ya wanawake ,
Neema aliyejitambulisha kama mwanamke jasiri katika jamii ya Wameru, ambaye aliachika na kuachiwa watoto wawili wa kulea, anasema aliamua kupigania haki yake baada ya mumewe kuanza kuuza ardhi pasipo kumgawia sehemu yake na watoto.
Mary Mw ita ambaye ni mwanasheria anasema kuwa mwanamke kama alivyo mwanamme wote ni binadamu na Tanzania imeridhia mikataba ya haki za binadamu na katiba ya Tanzania ibara ya 13 (1) inasema watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ubaguzi wowote kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.
Ibara hii inaonyesha kwamba mwanamke na mwanamme wapo sawa na kama wapo sawa basi swala la umiliki wa mali ikiwa ni ardhi wote wapo sawa sio hiyo tu bali katiba pia katika ibara ya 24 imeweka bayana juu ya umiliki pia ina imesema katika aya ya kwanza kuwa kila mtu anahaki ya kumiliki mali na haki ya hifadhi ya mali yake aliyonayo kwa mujibu wa sheria kwa maana kwamba kila mtu ana haki nakwa maana hiyo pia mwanamke ana haki na hata sheria ya ndoa pia ina mpa haki ya kumiliki mali
‘Faida ya umiliki mali inamsaidia ata mwanamke pale mwanamme anapokuwa amefariki inamsaidi kuondoa migogoro ya umiliki mali,pia jamii ijue wanawake ni wachumaji wazuri lakini kwa akili za wanawake kwa vile wanajua kupenda unakuta mtu anafukuzwa kwenye nyumba na kwa ajili ya mapenzi anakaa kimnya wakati walishirikiana kuchuma napenda
-Elimu ya kutosha itolewe kwa jamii kuhusu uwepo wa sheria ya umiliki wa ardhi kwa wanawake nchini
- Ni wakati sasa wa serikali na Azaki kushirikia kutoa elimu juu ya haki ya mwanamke kumiliki ardhi kwa mujibu wa katiba ibara ya 24na sheria ya ardhi kifungu namba 3(11).
-serikali ipitie upya sheria za ardhi ili kupendekeza mabadiliko .
-mtazamowa jamii mila na desturi zetu ambazo ni lazima ushirikiano uwepo wa kutoa elimu kuhusu haki ya mwanamke kumiliki ardhi kwa mujibu wa katiba
-ni jukumu la wadau wa haki na wadau wa sheria kuendelea kuhimiza haki ,kukemea vitendo vya uonevu katika jamii ambavyo vinahusisha mpakana umiliki wa mali na kumuona mwanamke awezi kumiliki
-ni mwakati wa mwanamke kuhamka ,kusimama na kufikiri kwamba anatakiwa kimiliki mali
AFISA MAENDELEO YA JAMII ANENA
Blandina Nkini ni ofisa maendeleo ya jamii mkoa wa Arusha anasema kuwa nafasi ya umiliki wa ardhi kwa wanawake wa mkoa wa Arusha yapo mabadiliko ambayo yanaonekana lakini kwa mila na desturi za mkoa wetu hapo zamani mwanamke alikuwa haruhusiwi kumiliki ardhi ,na siku zote huwa inakuwa ya baba na mama anaruhusiwa kulima ,kutumia anavyotaka lakini haruhusiwi kuiuza anae iuza anakuwa ni baba .
“sasa jambo hili limekuwa la miaka mingi na mda mrefu lakini kupitia elimu mbalimbali za maswala ya haki za kumiliki ardhi kupitia kwa wazee wetu wa mila tumeweza kufundisha mabaraza ya wa mama wa umasaini hivyo tumeona wanawake wa kimasai wamekuwa na haki sasa ya kumiliki ardhi na wengi wameweza kupewa hati miliki za mila mfano wilaya ya Longido pamoja na ngorongoro kunamashirika yasio ya kiserikali ambayo yamekuwa yakitoa elimu lakini pia kuwasaidia kuweza kupata hizo hati miliki za kimila za kumiliki ardhi na elimu hizo zimewasaidia sana “
“kwa sababu tumeona kwani ni jinsi gani watu wengi yaani wababa wengi wa kimasai sasa hivi wameweza kuwaruhusu wake zao kupewa zile hati za kimila kwa ajili ya kumiliki lakini mfumo dume na mila hapo nyuma zilikuwa zinamnyima kabisa mwanamke kumiliki ardhi ,wala kuuza na walikuwa wanasema ardhi ni ya baba na siku zote kwa upande wamila za kimasai tunaamini kuwa mwanamke ni mtoto tu hata kama angekuwa ni mtu mzima kiasi gani na wanaamini mtoto awezi kumiliki ardhi “alisema
JE MUAMKO UKOJE BAADA YA KUTOA ELIMU ?
Baada ya kutoa elimu kwa mkoa wetu wa Arusha muamko kweli ni mzuri maana kwa upande wa wilaya ya Longido zaidi ya hati 1000 zimetolewa kwawanawake hivyo unaweza ukaona kunaongezeko kubwasana la umiliki wa ardhi hususa ni kwa wanawake hawa wa jamii za kimasai nabado tunaendelea kutoa elimu kila siku na kuwa elimisha ili waendelee kuendelea kutoa kabisa mfumo dume wa kusema mwanamke anahaki ya kumiliki ardhi .
ATOA USHAURI KWA WANAWAKE
Katika swala lakumiliki ardhi napenda tu kuwashauri wa baba wajue kwamba katiba yetu ya Tanzania inasema binadamu wote ni sawa na kama binadamu wote ni sawa inamaana kwamba kila kilichopo katika nchi hii tunahaki sawa za umiliki awe baba au mama kwa iyo atuoni sababu ya kuendeleza zile mila na desturi ambazo tunaziona zimepitwa na wakati hatuwezi kusema ni mbaya ila kunamila ambazo zimepitwa na wakati hivyo kuna haja ya kuanza kuziondoa taratibu na kuwaruhusu sasa wanawake kuweza kumiliki ardhi kwa sababu tunaona kabisa kwa upande wa maswala ya mifugo na kilimo mwanamke anamchango mkubwa sana
mwanamke anauwezo wa kufanya shughuli nyingi sana ambazo zinazalisha kiuchumi kwa iyo ni wakati umefika sasa wa mama au mwanamke kuinuka na wanapo itwa kwenye semina au mafunzo ya maswala ya haki za wanawake na ardhi wawe wanashiriki ili tuweze kujua ni jinsi gani na wao wanaweza kumiliki aridhi .
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia