BREAKING NEWS

Thursday, March 2, 2023

WAFANYABISHARA WA SOKO LA SAMUNGE WAMJIA JUU LEMA KUMUINGIZA NABII MKUU DKT.GEORDAVIE

 Na



Woinde Shizza , ARUSHA


Wafanyabiashara wa soko la Samunge (NMC) wamemjia juu aliekuwa mbunge wa  jimbo la Arusha mjini Godbless Lema Kwa kitendo alichokifanya cha kumsema nabii Mkuu wa kanisa la Ngurumo ya upako  Kwa kuwapa msaada wa shilingi milioni 100  .

Wakiongea kwa jaziba wafanyabiashara hao walimtaka mbunge huyo kufanya saisa zake bila kumgusa nabii huyo kwani ameweza kuwafuta machozi  pale walipo pata matatizo.

"Siku zote mti wenye matunda ndio unapigwa mawe nabii Mkuu Dr GeorDavie ni mtu wenyematunda na ndio maana unapigwa mawe tunaomba tumjibu Lema vizuri,Lema wewe ni mwanasiasa nabii sio mwanasiasa nabii ni mtumishi wa Mungu ategemei serekali ,wala chama wala siasa anategemea waumini  wake usije ukamkashifu eti kwamba ametoa milioni mia Moja wakati wewe umekuwa mbunge wa miaka 15 umesaidia Nini "alisema 
Mwaji Daudi (mama shilooo) 

Walibainisha  wakati walipo unguliwa na soko yeye alikuwepo tena akiwa mbunge lakini alishishidwa kuwa saidia chochote  ,na hata hakwenda kutoa pole Kwa wananchi waliompa kura zaidi ya kuwa kashifu wafanyabiashara hao kwa kuwaambia kuwa mke wake awezi kuja kununua vitu sokoni hapo  kwani soko hilo linanuka.


"Leo kwanini umseme nabii ambaye ametuona sisi tunafaa na akaamua kutusaidia tunaomba tukwambie  umuache nabii wetu ,tukwambie tu fanya siasa muwache nabii ,yeye ninkipenzi chetu sisi , Samunge na nabii ni mbele Kwa mbele na tukwambie tu ukitaka kuhusa uhai wa soko hili mguse huyu nabii ,kutoa msaada wa milioni 100 sio jambo dogo tumuulize tu yeye ndani ya miaka 15 amefanya nini ndani ya soko la Samunge na uyu baba anaishi maisha sio ya mchezo mchezo lakini ametudhamini watu wa samunge alafu anatokea mtu anaongea ongea tu  hatukubaliani na swala hilo"alisema mwenyekiti  wa soko la Samunge Njola Miraji

Aliongeza kuwa Lema ni muongo Wala hajui kinachoendelea Kwa sababu alikuwa nje ya nchi na aelewi kitu chochote kinachoendelea  na ndio maana amekurupuka na kuongea vitu vya uongo .

"Niseme tu milioni mia Moja Lema awezi kutoa ata shilingi kumi awezi kutoa niseme tu hii yote ni wivu tu ndio inamsumbua ndio maana anaongea vitu asivyovijua ,na niseme tu nabii wetu ni mtu tajiri asivyojua ukienda pale kanisani katoa misaada ya kutosha Kwa waumini wake ,mitaji magari ,Kodi  kawalipia watu ada nzuri zaidi achagui dini Wala mtu wa kumsaidia"alisema Njovu

Alisema Kupitia kauli ya jana amewakera na  wamempuuza sana kwakweli japo Kwa kuwa uyu nabii ametupa msaada wa fedha halisi na sio wa maneno  hivyo tumwambie tu afanye siasa zake na asimuingize mtu alietuona tunafaa kusaidia katika siasa


Kauli ambayo imefanya wafanyabiashara hawa wa soko la Samunge ni ile aliekuwa mbunge wa Jimbo la Arusha Godbless Lema  aliyoiongea katika viwanja vya reli  alipokuwa katika mkutano wa adhara wa wananchi ambapo alisema  anashangaa Wachungaji  kuja adharani kutoa cheki za milioni mia wakati makanisa yao hayana hata tailizi Unakuta mchungaji anakuja anasema nanukuu

"Ninatoa Mimi nabii mkuu milioni 100   kabla ajatoa milioni 100 kwabla ujatoa izo ela ili upate umashuhuri mwekee mungu kwenye nyumba yake tailizi unaishije kwenye nyumba nzuri kuliko  nyumba ya kuabudia  Mungu  huo ni unafiki ,  huyo nashulika naye Mimi nabii Mkuu naanza mikutano hivi karibu "mwisho wa kunukuu

Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates