mkurugenzi wa kampuni inayotengeneza taulo za kike zijulikanazo Kwa jina la HQ ,Selina Letara akiongea na waandishi wa habari katika usiku wa tuzo za wanawake wajasiriamali Arusha
Na Woinde Shizza ARUSHA
Wanawake wametakiwa kutokukata tamaa katika kazi zao pamoja na kufanya kazi kwa nguvu na bidii huku wakimtegemea Mungu ili waweze kuondokana na umaskini.
Hayo yameelezwa na mkurugenzi wa kampuni inayotengeneza taulo za kike zijulikanazo Kwa jina la HQ ,Selina Letara alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo za wanawake wajasiriamali Tanzanite ambapo alishinda nafasi ya best brand of the year ilioandaliwa na kampuni ya phide intatament ambapo alisema kuwa niwakati sasa wa wanawake kuamka na kuanza kuchapa kazi.
Aliwataka wanawake kutokata tamaa katika kazi zao na wamtegemee Mungu zaidi huku wakichapa kazi Kwa bidii zaidi na sio kwenda kukesha makanisani na kusema wanapokea miujiza kwani hakuna miujiza unaokuja bila ya kujituma na kufanya kazi.
"Kufanya kazi kwa moyo na kupenda kazi unayoifanya ukishapenda kazi unayoifanya utafanyakazi Kwa moyo na kupenda kazi unayoifanya ,Mimi sikuanza na kazi ya pedi Moja Kwa moja bali nilianza Kwa kutembeza mitumba mlango kwa mlango baadae nikaja kufanya kazi ya kushona mimi ni mwanamitindo na baada ya hapo ndio nikaja nikafungua kampuni ya pedi haya mafanikio yote yametokana na Mimi kupenda kazi yangu "alisema Selina
Aidha alisema kuwa watanzania wengi wamekuwa na tatizo la kutokujali mda kitu ambacho kimewafanya waendelee kubaki katika umaskini hivyo aliwataka wabadilike Ili waweze kutoka kwenye umaskini.
"Waafrika wengi atujali mda ,muda ni fedha ukijali mda lazima ufanikiwe ,ukijali muda lazima ufanikiwe lakini pia unatakiwa ujali wateja ili ufanikiwa ata wakikuuloza maswali ya kijinga wavumilie wajibu vizuri ili wakuuingishe na waweze kurudi tena ,mimi ndio nilichofanya adi kufikia apa"alisema
Aidha aliwataka wateja wao wa bidhaa za HQ kukaa mkao wa kula kwani wanaendelea kuwaletea bidhaa mpya na bora kwa ajili yao.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia