Na Woinde
Shizza,Arusha
“Tatizo la wanawake
wengi kutopata mimba au kuchelewa kubeba ujauzito limeonekana kuwa kubwa
sana na linaongezeka siku hadi siku ambapo
zipo sababu mbalimbali ambazo zinasemekana ndio chanzo halisi cha tatizo hilo
huku sababu moja wapo inayoonekana kuchangia ni mfumo wa maisha wanayoishi ”
Mwandishi wa habari hizi alifanya mahojiano na Daktari wa
magonjwa ya kina mama kutoka hospitali ya seliani ( Selian Lutheran
Hospital)Dkt . Christopher Tesha ambaye
aliweza kuelezea zaidi baadhi ya sababu zinazopelekea wanawake kutokubeba mimba au kuwa wagumba
ambapo alianza kwa kuelezea ugonjwa halisi
UGUMBA NINI ?
Ugumba ni hali ya kushidwa kupata mtoto na hili linawahusisha watu wote kwa maana ya
wanawake pamoja na kina mama
SABABU
ZINAZOSABABISHA UGUMBA
Sababu zinazo sababisha ugumba zipo nyingi kuna watu wanaweza wakawa wanauwezo wa
kupata watoto au mtoto mwanzo lakini baadae wakashidwa kupata
na kuna watu wanakuwa hawana uwezo tangu walipo zaliwa
-Tuanze na hawa ambao
wanashidwa kupata watoto tangu kuzaliwa
*watu hawa ambao wanapata tatizo hilo tangu wanapo zaliwa hii inatokana na sababu tu za
kiafya ambazo walivyo zaliwa ule uwezo
wakutengeneza mtoto hawana kama ni wababa na wakina mama uwezo wa kubeba ujauzito
hawana labda kwasababu hawana mayai au mfuko wa uzazi haujakaa vizuri na vitu kama hivyo .
- Ugumba
unaotokea baadaye maishani
Huu ni ule ambao mwanamke
na mwanaume wameshawahi kupata ujauzito au kutungisha mimba angalau mara moja
maishani mwao na baada ya hapo hawajafanikiwa kupata au kutungisha mimba tena.
DKT TESHA ANAELEZA BAADHI YA SABABU
ZINAZOSABABISHA UGUMBA UNAOTOKEA BAADAE
* maambukizi ya via
vya uzazi
Sababu zingine zinazoweza kusababisha mtu asipate mtoto ni
maambukizi ya via vya uzazi labda kwa kina mama au kina baba au kwa bahati
mbaya wanaweza pia wakaugua wakafanyiwa
upasuaji ambao unahusiana na mfuko wa
uzazi wa kina mama hiyo itawasababishia
kushidwa kupata watoto .
*Mfumo wa maisha
Mfumo wa maisha unaweza pia ukawa unachangia kwa kiasi kikubwa
mwanamke au mwanaume kutokupata mtoto ,pia
magonjwa yanayopelekea kuadhirika kwa via vya uzazi yamekuwa ni mengi hivyo kupelekea kuharibu mfumo mzima
wa uzazi
*vyakula tunavyokula
* Tatizo la
ugumba linaweza kutokea wakati wa yai au kiumbe kilicho ndani ya mfuko wa uzazi
(uterus) kushindwa kukua hadi kufikia kuwa mtoto, mayai yaliyo ndani ya mfuko
wa uzazi kushindwa kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi (uterus lining),
matatizo kwenye njia ya kupita yai au mayai wakati yanakwenda kwenye mfuko wa
uzazi na matatizo ya mayai ya uzazi (ovaries) kushindwa kutoa mayai.
* Tatizo la ugumba kwa wanawake pia husababishwa na matatizo
katika mfuko wa uzazi na shingo ya kizazi kama uvimbe na matatizo katika mfumo
wa kuganda damu.
* Sababu nyingine ni afya iliyodhoofika
*matatizo ya kula, baadhi
ya madawa au sumu, msongo wa mawazo
*tatizo la kukosekana kwa usawa wa mfumo wa vichocheo mwilini na
uzito uliopitiliza.
*
unywaji pombe kupindukia
*kuwa na magonjwa ya muda mrefu kama kisukari
*magonjwa ya kinamama,
magojwa ya zinaa au saratani.
*uvutaji sigara, madawa
ya kulevya kama cocaine, bangi, hashishi ,
* wanawake wanaopata hedhi bila kutoa mayai, kuwepo kwa cervical
antigens ambazo huua mbegu za mwanaume hivyo kusababisha mwanamke kutokupata
watoto mwanamke
*Idadi ya watu ambao wanashindwa kupata watoto inaongezeka
lakini pia matatizo ambayo yanahusiana
na maambukizi kwenye via vya
uzazi na
mifumo ya uzazi inaongezeka kwa
kiasi kikubwa haya ndio mambo makubwa yanayosababishia watu kutokupata watoto .
TATIZO LA
UGUMBA LIKOJE KWA SASA
“tatizo hili kwa kiasi kikubwa ni kubwa na linaongezeka kwa kasi na inawezekana
likawa linaongezeka kwa sababu pia
ongezeko la watu limekuwa ni kubwa lakini pia
kwa ujumla linaongezeka pamoja kuwa hana takwimu sahihi lakini linaonekana sana ukilinganisha na miaka
iliopita kwa hiyo jamii yetu inakubwa na
changamoto za kushidwa kupata watoto kwa kiasi kikubwa sana na tatizo linaongezeka “alibainisha Dkt
Tesha
AELEZEA SWALA LA MATUMIZI YA DAWA
- Swala la matumizi ya dawa
za kuzuia uwezekano wa kupata ujauzito kwa wanawake na mabinti kwa ujumla alisema kwa sasa dawa hizo zinatuika kwa
kiasi kikubwa sana na kwa bahati mbaya zaidi zinatumika bila kufata utaratibu bila hata kupata ushauri wa kitaalamu hivyo alitumia muda huo kuwashauri wanawake
haswa mabinti wadogo mashuleni ,wale wa mitaani na hata kina mama watu wazima ambao wanategemea kuzuia
ujauzito wanaoamua kwenda dukani na kuchukuwa dawa kuzimeza
waache kwani sio sahahi kwa kuwa
wanameza bila maelezo ya kitaalamu lakini pia
wanazimeza nyingi zaidi kuliko
kawaida kwa hiyo sio nzuri wala salama kwa afya zao .
- changamoto ya kuona ninamna gani wafanye ili wasipate
ujauzito bila kujipanga ni afadhali waendele hospitalini waonane na daktari ili washauriane watapata
maelezo ya kitaalamu ambayo yaakuwa ni msaada mkubwa sana kwa afya zao
MUHANGA WA
KUTOKUPATA MTOTO AELEZEA
Anjela anaeleza kuwa yeye ni muhanga wa janga hilo la kutokupata
mtoto anaeleza kuwa amekuwa anapitia wakati mgumu sana haswa pale anapowaona
watu ambao amekuwa nao wanawatoto lakini
hana
Anaeleza kuwa ameshakaa kwenye ndoa kwa muda zaidi ya miaka 15
lakini hakupata mtoto ,na kutokana na
masumango alikuwa akipata kutoka kwa
mume wake na wifi zake ilimbidi abebe virago vyake na kuamua kuondoka katika
ndoa yake
Anaeleza pia alishajaribu kutumia dawa za aina mbalimbali
zikiwemo za hospitalini pamoja na zile za mitishamba kutoka kwa wabibi
mbalimbali lakini hakubahatika kupata mtoto
“sio kwamba sijawahi kubeba mimba nilishabebaga awali ila
sikubahatika kujifungua kwani katika kuangaika kwangu nilifanikiwa kupata
lakini ilifika siku nikawa najisikia vibaya na nilipoenda hospitali niliambiwa
ni typhoid sikuwa na nia ya kupima mimba maana sikuwa na wazo hilo baada ya
kutumia zile dawa kwakuwa zilikuwa nyingi ndipo ilitoka nilikuja kjua ni mimba
baada ya kuumwa tumbo sana na kwenda hospitalini”alisema
ANATOA
USHAURI GANI
Aliipongeza serikali kwa kuendelea kutoa elimu na kusema
kuwa elimu inatolewa lakini watu waoenda
kupata elimu hiyo ni wachache,lakini pia
watu wamekuwa wanapeana ushauri mtaani bila kufata utaratibu ndio
maana mwisho wa siku wanapata matatizo hivyo aliwashauri watu wawe na
kiu na hamu ya kupata elimu kuhusiana na
afya zao ili kama ni kutumia dawa au kufanya chochote wafanye wakiwa wanajua
wanafanya nini ili mwisho wa siku wasije
wakapata matatizo wakaanza kusema laiti wangejua
-Watafute elimu kwa kwasababu zipo kila hospitali ina wataalam
wanaoweza kutoa izo elimu tena bure ili kujikinga na mazara yanayotokana na
matumizi holela ya dawa na sio za uzazi wa mpango tu bali hata dawa
zingine zozote zile
- ni wajibu wa wanawake au ni vyema kila mtu ajijengee tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuendelea kuimarisha afya yake pamoja na kuangalia vyakula anavyokula na sio kula tu vyakula mradi kushiba
-Tiba
ya tatizo ni pamoja na ushauri nasaha kutoka kwa wataalamu wa afya na
kuwaelimisha wapenzi wawili, Kuna wanaume wengi ambao hufika kilele haraka
wakati wa kujamiana na hivyo kutoa mbegu ya kiume mapema kabla ya muda muafaka,
hii husababisha lawama zote hupelekwa kwa mwanamke pasipo mwanaume kugundua
kuwa tatizo ni lake.
-Tatizo
lingine ni kutofahamu lini hasa ni muda muafaka wa kujamiana ili kushika mimba
kwa urahisi,Kwa wanawake ambao hawajui hata mzunguko wao wa hedhi, yaani
hawajui wanaanza na kumaliza hedhi lini na wakati wa hedhi wanatumika kwa muda
wa siku ngapi.
-Ongeza nafasi yako ya kushika
ujauzito kwa kujamiana angalau mara tatu kwa wiki kuelekea wakati wa ovulation
au kujamiana wakati wa kipindi chote cha ovulation.
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia