"Nianze
Kwa kummwagia sifa Mwanamke ambaye ni mama mwanamke ni mwalimu ,
mwanamke ni kiongozi na pia mwanamke huyo huyo ni super women
kheri ya sikukuu ya Wanawake, wanawake wote Tanzania japo kuwa ndio
tunaelekea mwishoni mwa mwezi wa kuanzimisha siku hii “
Leo tunaangazia tatizo la ajira linavyowasumbua
wanaweke wengi katika sekta binafsi pamoja na zile za serikali ambapo Pengo la kijinsia libakia kuwa moja ya tatizo linalokabili dunia katika
masuala ya kazi, hii ni kwa mujibu wa ripoti iliofanywa na shirika la kazi duniani ambapo ilisema kwamba wanawake wana fursa ndogo zaidi
ya kushikiri kwenye soko la ajira ikilinganishwa na wanaume.
Japokuwa kitakwimu wanawake ni wengi zaidi ya wanaume, wanawake
wanakumbana na changamoto zinazowafanya kushindwa kufurahia matunda ya kazi zao
na kuzidi kuongeza umaskini na utegemezi mambo ambayo yanasababisha ukatili wa
kijinsia, Utegemezi huo unatokana na mfumo dume hasa kwenye maswala ya mwenye
haki ya kumiliki mali au vitu
Kutokana na Ripoti ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imeeleza
kuwa hakuna mabadiliko makubwa ya mgawanyo wa ajira kisekta kwa kutumia tafsiri
ya kitaifa kati ya mwaka 2014 na 2020/21 japokuwa ajira katika Serikali Kuu na
Serikali za Mitaa zilisinyaa.
Mabadiliko makubwa ya mgawanyo wa ajira
yameonekena miongoni mwa watu walioajiriwa katika sekta ya kilimo (66.8% 2014
na 58.4% 2020/2021) na shughuli nyingine binafsi za kiuchumi zisizo za kilimo
(mwaka 2014 asilimia 26.6, na mwaka 2020/21 asilimia 22.7).
Ripoti hiyo ya Watu wenye Uwezo wa Kufanya Kazi
ya mwaka 2020/21 imesema kuwa kusinyaa kwa kiwango cha waajiriwa Serikalini
kunatoa taswira kamili ya hatua zilizochukuliwa na Serikali kati ya mwaka 2015
na 2020 ambapo zilitolewa ajira mpya chache. Aidha, kupungua kwa
kiwango cha ajira katika sekta binafsi za kiuchumi zisizo za kilimo kunaashiria
uwekezaji mdogo katika sekta hizo ama uwekezaji umejikita katika maeneo
yanayohitaji nguvu kazi kidogo.
Aidha pia kwa mujibu wa takwimu zilizofanywa pia na ofisi ya taifa ya TaKwimu (NBS) ya mwaka
2020/2021 kwa upande wa shamba binafsi ,familia na kaya zinaonyesha kuwa licha
ya mwanamke kupitwa katika baadhi ya sekta
za ajira ,wamejitaidi kwenye
kilimo ambapo wamepanda kwa asilimia 56.6 huku wanaume wakiwa 60.3 tofauti
na sekta zingine.
Hii inaonyesha kwamba zinahitajika juhudi kubwa
kuvutia uwekezaji na biashara zenye uwezo mkubwa wa kuzalisha ajira hasa kwa
wanawake ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali.
MWANAMKE AELEZEA JINSI TATIZO HILI
LILIVYOKUBWA
Teodora Mrema ni mwanamke anaeleza kuwa tatizo la ajira bado ni changamoto
kubwa inalowakumba wanawake
Changamoto hiyo kwenye swala la ajira kwa wanawake bado
halijawa na usawa kwa sababu ukiangalia kwa asilimia kubwa
sekta ya ajira hususa ni serikalini
wanaume kwa asilimia kubwa ndio wanao
pewa kipaumbele ukioangalia kwa mfano
serikalini kitengo Fulani unagundua kwamba wanaume ni wengi kuliko wanawake kwaoiyo swala hili
bado ni changamoto
Mbali na serikalini lakini pia ukirudi kwa
upande wa sekta binafsi shida bado ipo kwani ukifuatilia sehemu hinyo wanawake
wamekuwa wakikutana na vikwazo mbalimbali pindi wanapotafuta ajira kwani
wengine wamekuwa wakilazimishwa hata kutumia miili yao ili wapate ajira hali
ambayo inawakatisha tamaa kabisa
CHANGAMOTO ZINAZOWAKUTA WANAWAKE WAKATI
WAKISAKA AJIRA
-Unyanyasaji wa kingono
Wanawake wengi wamekuwa wakienda kuomba ajira
wanakutana na tatizo hili la unyanyasaji ,ambapo wale waajiri wamekuwa
wakitumia fursa ya kumuona yeye ni mwanamke
hivyo amnyanyapae kwa kumtaka
kingono
-Wanawake kuzaraulika hata kuonekana kuwa wanapo kuwepo katika soko la ajira wana fursa ndogo ya
kufanya kazi katika ubora
Kutokana na changamoto hizo zinazosababisha ukosefu wa kipato, baadhi
ya wanawake na wasichana hujiingiza kwenye biashara zisizo halali ikiwa ni
pamoja na biashara ya ngono, na kwa kufanya hivyo wengi wamejikuta wakifanyiwa
vitendo vya udhalilishaji hususani kubakwa, kulawitiwa, kupigwa na hata
kukashifiwa
-Ubaguzi wa kijinsia
Swala hili limekuwa linawaathiri wanawake na wanaume kwa mtizamo wa
usawa wa kijinsia, Haki, majukumu na fursa sawa kwa wanawake , wasichana na
wavulana kuwa jinsi moja ni dhaifu au ni bora zaidi na si kwa kuzingatia ubora
wao halisi.
-Ukatili Dhidi ya Wanawake
Hiki ni kitendo au vitendo vya
unyanyasaji vyenye kulenga jinsia ya kike na vyenye kusababisha au kuleta
madhara ya kimwili, kingono, kihisia, kisaikolojia, kiuchumi na kijamii ,Kitendo
au vitendo hivi hujumuisha kutumia nguvu na vitisho vya kumnyima mwanamke haki
na uhuru.
NINI KIFANYIKE ILI KUPUNGUZA TATIZO
LA AJIRA KWA WANAWAKE
-Swaumu John anaeleza baadhi ya mambo
yatakayosaidia kuongeza idadi ya wanawake katika sekta muhimu za ajira ni
pamoja na
*kuwapa ujuzi
na maarifa ,mitaji na mikopo kuendeleza shughuli zao za uhakika
*kuwatengenezea mfumo mzuri utakaowasaidiha kufaidika
na shughuli zao ili
kuboresha ustawi wa maisha yao
*ni vyema serikali au sekta binafsi ikawa na
uwiano sawa kwa sababu wanawake wakipewa nafasi wanaweza pia
kuzitumiha fursa sawa na wanaume
*Kuhakikisha ushiriki wa Wanawake katika
ngazi zote za kutoa maamuzi na utekelezaji wa maendeleo ya sera na program.
*Kuhamasisha upatikanaji wa mikopo kwa wanawake, mafunzo, ujuzi
endelevu na kupanua huduma hizo mijini na vijijini katika ngazi zote ili
kuwapatia wanawake maisha bora na kupunguza kiwango cha umasikini kwa wanawake.
*Kuhakikisha kuwa madhara ya utandawazi pamoja madhara ya mipango ya kibiashara na sera
hayamuathiri mwanamke.
SERIKALI IFANYE NINI
• Serikali inawajibika kuhakikisha kwamba watu wote wanawake kwa
wanaume bila kujali rangi, jinsi, lugha, dini, siasa, kabila, hali ya mtu au
mahali alikotoka, wanapata fursa sawa za kiuchumi na wanatumia fursa hizo bila
ubaguzi wa namna yoyote ile
• Serikali inawajibika kuhakikisha kwamba utajiri wa taifa
unaendelezwa, unahaifadhiwa na unatumiwa kwa manufaaa ya wananchi wote kwa
ujumla na pia kuzuia mtu kumnyonya mtu mwingine.
• Serikali pamoja vyombo vyake vyote vya umma vinawajibika kutoa nafasi
zilizo sawa kwa raia wote, wake kwa waume, bila ya kujali rangi, kabila, dini
au hali ya mtu. Pia serikali inawajibika kuhakikisha kwamba aina zote za
dhuluma, vitisho, ubaguzi, rushwa, uonevu ,upendeleo vinaondolewa nchini.
habari hii imeandikwa na mwandishi Woinde Shizza ARUSHA
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia