BREAKING NEWS

Wednesday, March 22, 2023

RAIS SAMIA AJENGA MIKAKATI YA KUKUZA UCHUMI





Na mwandishi  wetu,Dar es salaam 



Kada wa CCM Kata ya Jangwani   Mohamed Fidahusein amesema miaka miwili ya utawala wa Rais Samia  suluhu Hassan imejenga  mikakati ya kukuza  uchumi, uongozi bora na kuwapa heshima wanawake wa Tanzania na Afrika. 




Hayo yametamkwa  na kada wa CCM kata ya jangwani Mohamed Fidahusein katika shina la CCM mtaa wa chui  jijini  Dar es Dar es salaam 




Fidahussein alisema utawala wa Rais samia kwa  kipindi cha miaka miwili  akiwa madarakani , amesimamia nidhamu ya kazi serikalini , kukomesha maonevu ,uzembe,  manyanyaso na kusimamisha uongozi wa haki. 




Alisema kutokana na uchapakazi  wake  ni wazi  kiongozi  huyo wa kwanza mwanamke nchini, amewainia na kuwafanya wanawake wa Tanzania na Afrika wajiamini zaidi  kifikra ,kujitegemea na kuheshimika.




Aidha kada huyo ameyashauri makundi ya vijana na wanawake huku akitaka kila kundi lifanyekazi kwa bidii bila kupoteza muda kwani nguvu walizonazo leo zitumike ipasavyo kuwapa manufaa na kuwekeza kwa kesho yao.





"Nimevutiwa na utendaji makini  wa miaka miwili ya  utawala wa Rais Samia . Amefanikiwa kujenga mikakati ya kukuza uchumi imara. Najua wapo ambao kwa makusudi wanabeza mafanikio hayo. Uongozi wa Rais wetu  utaacha alama  isiofutika katika nchi yetu  milelele " Alisema Fidahussein. 




Kada huyo pia alisema kama ambavyo mji wa Roma huko Italia haukujengwa kwa siku moja, ndivyo ambavyo uchumi   wowote unapoanza kujengeka , matunda yake huwa hayaonekani machoni mwa watu kwa haraka. 




Akizungumzia kuhusu  utawalabora ,utawala wa sheria na nidhamu  serikalini ,alisema mama  huyo ana haki ya kuungwa mkono na vyama vyote vya siasa. 



Kada huyo  alidai  Rais Samia ameshatoa  msimamo wa serikali yake ,  kuitangazia dunia akisema anachukizwa na uonevu, uvunjaji sheria pia akizihimiza kwa ngazi  nyingine  za serikali kulinda haki za binadamu.




"Kwa kipindi  cha miaka miwili ya utawala wa Rais  samia kuna  uwazi katika uendeshaji wa taasisi za umma ,Watu wengi wanaacha polepole kutozilalamikia mahakama na polisi, Taasisi za  ukusanyaji mapato  nazo hazionei wala kuwasakama wafanyabiashara  "Alieleza 




Kuhusu kupanda kiwango cha hamasa za michezo  hususan mpira wa miguu,  Fidahussein alisema  katika utawala wa Rais huyo timu za simba na Yanga  zimeanza kuonyesha makali yap baada ya  kufuzu kuingia robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika.




"Wakati serikali ya awamu ya sita kijijijenga kimataifa , kidiplomasia na kwenye taasisi za fedha .Viongozi na makada wa Chama lazima tuzidi kukiendeleza chama chetu , Tutapita kila mtaa, nyumba kwa nyumba  kuelezea utekelezaji wa ilani ya chama "Alisisitiza kada huyo.


Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates