BREAKING NEWS

Tuesday, March 21, 2023

UFUGAJI KUKU UNAVYOWEZA KUMTOA MWANAMKE KWENYE UMASKINI


 

"Mradi wa kufuga kuku wa nyama (broiler  ) umeonekana kuwasaidia na kuwainua wanawake wengi hapa nchini  ,asilimia kubwa ya wanawake  wengi   wanaonekana kwenye biashara ya ufugaji kuku   na

 wengi wao wanaeleza biashara hiyo imekuwa mkombozi wa maisha yao” .


TATIZO NINI

Baadhi ya Wanawake wamekuwa wanajiuliza wafanye biashara gani ambayo itawawezesha kuwakomboa au kuwaondoa katika umaskini  ,wengine wamekuwa wanawoga  wa kufanya jambo  kukosa  mitaji,kutokuwa na udhubutu pamoja na elimu ya kutosha wakati huo huo Kuna ambao wanaogopa hasara  

Kwa wale waliodhubutu wanaeleza namna walivyoanza na biashara hiyo ilivyo wainua

WANAWAKE WAELEZA NAMNA UFUGAJI KUKU ULIVYOWEZA KUWAINUA

Milka Lema ni mwanamke ambaye anajishuhulisha na biashara ya ufugaji kuku wa nyama pamoja na wamayai (broiler) anasema kuwa mradi huu umeweza kumsaidia  kubadilishia maisha  yake na kufanya kuwa na maisha tofauti na awali .

“mradi wa kufuga kuku  umeweza kunisaidia mimi kama mwanamke  ambaye ni mjasiriamali   mdogo kujikwamua  kwenye hali ngumu ya maisha  na kunifanya kuweza  kusaidia mahitaji  muhimu ya kusaidia familia  kama kusomesha watoto ,kusaidia jamii na familia  kwa mahitaji madogomadogo  ya kila siku mfano  matumizi na maitaji ya nyumbani kutokana na faida tunayoipata  kwenye ufugaji wa kuku”alisema Milka

Pia alifafanua kuwa ufugaji wa kuku  unasaidia wanawake wengi   kuwa na wazo la ziada  kama kufikiria kuwa na uwezekanao wa kununua eneo kwa ajili  ya makazi ya familia kutokana  na faida wanayoipata



ALIANZAJE BIASHARA HII ?

Milka anaeleza  kuwa alianza biashara hii mika kumi iliopita ambapo alisema alishawishika kufanya biashara hii mara baada ya kuona rafiki yake ameifanya na kufanikiwa ,anafafanua kuwa alianza na mtaji wa vifaranga 100 ambayo ni boxi moja na sasa biashara imekuwa na kufikia vifaranga 2000

Tangu kuanza kwa ufugaji amekuwa  akitenga asilimia chache za faida kwa ajili ya kufanya shughuli zake zingine za kujiendeleza  ambapo anabainisha kupitia ufugaji huo wa kuku ameweza kujenga nyumba yake ya kuishi pamoja na zawapangaji ambapo pia lifafanua  kupitia

 

Jenifa Alphayo ni mwanamke mchacharikaji  anaejituma katika shughuli mbalimbali ikiwemo ufugaji kuku ,ushonaji  ,uzaji wa maua pamoja na kuuza vyungu  kwa ajili ya  kuwekea maua  anaeleza kuwa  ameanza kufuga kuku mwaka 2014 alianza na kuku wa kienyeji wale chotara baadae akaona kuku wale  hawampi faida na walikuwa sio wazuri kwenye  kumletea faida  ndipo alipobadilisha na kwenda kwenye ufugaji wa kuku wa nyama ambao umemsaidia kwa kiasi kikubwa katika kubadilisha maisha yake .

“kuku hawa wanyama nilipoanza nilianza na kuku 500 ili kujifunza ,kujua changamoto na masoko  ,nikatoka kwenye kuku hizo mia tano nikaenda 1000  na sasa nimefika kuku 3000 saa  ingine kama kipindi ni kizuri naenda mpaka kwenye kuku 4000



KUKU HAWA WANAWASAIDIAJE ?

Kuku hawa wana faida zake na hasara zake tukianza na faida

-wanawasaidia kuwaongezea kipato ,wanawafanya kuweza kuendesha familia zao   na shughuli zingine zile zinazohusiana na maswala ya pesa

- wakiwa na hao kuku wakiweza kupata masoko na kuwauza kwa wakati    iinakuwa ni faida na inafaida nzuri  kwa iyo ni biashara  nzuri na inaingiza kipato na haiwezi kumuacha mfugaji mtupu

 CHANGAMOTO GANI WANAKUMBANA NAZO ?

 Kwa upande wa matatizo yapo mengi mno na  kama vile unavyopata faida ndivyo unavyopata shida tukianza na changamoto ya kwanza 

- chakula cha kuku

  Chakula cha  kuku siku zote kiko gali sana ulinganisha na bei ya kuku  iliopo   sokoni na mara nyingi wanao waharibia biashara hii ya kuku ni madalali ,hawa watu wamekuwa  hawaingii katika  kufanya  chochote  lakini wamekuwa wakipanga bei wao ambayo wanataka  ,lakini mfugaji kama mfugaji anapata faida ndogo ambayo  ukilinganisha kama hakuna dalali faida ile yote ingeenda kwa mfugaji .

“mfano unaweza kukuta kuku anauzwa sh 6500 mapaka elfu 7000 mda mungine ukipiga hesabu na gharama zingine  za dawa  umeme na maji faida inakuwa ni ndogo  ,changamoto hii inatokana na kwamba wafugaji atuna umoja wa kusema ya Kwamba sasa  tuamue bei  iwe hii kama watu wa mabuchani wauza nyama za ng’ombe  au wafanyabiashara wengine sisi wafugaji wa kuku kila siku tunaibuka wafanyabiashara wapya  na wanapoinuka wanakuja hawajui matatizo ya kuku wanapoingia kwenye hii  kazi ya kuku anaona auze tu wamtoke  waana wakendelea kukaa ni hasara kwaiyo wakati wewe umekaa na kuku wako utaki kuuza kwa bei ya hasara kuna ambaye anaona auze apate hasara “

-kukatika umeme

Swala la kukatika umeme imekuwa ni shida ingine kubwa inayowasumbua wanawake hawa ambao wanafuga kuku  ,unakuta  mtu umeingiza vifaranga umeme unakatika ,muda mungine unakuta kuku wamekuwa, umeamua kuwaweka kwenye friza umeme unakatika  kwa hiyo kwa nchi yetu hili swala la ukatikianaji umeme imekuwa ni changamoto kubwa sana



ANAWASAIDIAJE WAKINA MAMA WENGINE KUPITIA UFUGAJI HUU

Jenifa anasema kuwa  katika biashara hii amekuwa akisaidia kina mama  kujipatia kipato kwani katika kipindi cha kuchinja  wakinamama zaidi ya kumi hadi 20 wamekuwa wakija kujipatia kipato kupitia uchinjaji pamoja na unyonyoaji wa kuku hawa  na pia  wamekuwa wakiondoka na  mazaga ambayo ni vichwa ,miguu,utumbo na firigisi  ambavyo pia wakiondoka navyo wanaenda kuviuza  na kupata fedha ambayo inawasaida kuendesha familia zao  kwaiyo ni msaada ambao wanawasaidia wale kinamama wa kipato cha chini kuinuka kidogo kwani kinamama hao ukiwafatilia wanawatoto wadogo wanaishi nyumba za kupanga kwaiyo wanasaidika kwakweli kupitia kuku hawa

 

 

AWAHASA WANAWAKE



Aliwataka wanawake kuingia katika  biashara hii kwani ni nzuri na itawasaidia  kuinua vipato vyao  ,na pia nawaambia kabisa wakiingia wajue kabisa kuna faida na hasara   na sio kwenye ufugaji wa kuku tu bali kwenye biashara yeyote uwezi kuingia siku hiyo na kusimama bila kupitia misukosuko haiwezi kuwaacha watupu

“nawashauri kina mama wengine ambao wanataka kuingia kwenye hii fani waingie maana hakuna biashara  ambayo haina changamoto ,waingie maana uwezi kukaa bure ukasema ufanyi chochote  unatakiwa ufanye chochote ili  uweze kujipatia kipato chako mwenyewe

 


WATOA OMBI  KWA SERIKALI

-waiomba serikali iwasaidie  namna ya kufanya bei ya kuku iwe moja ambayo  itakidhi  vigezo na kumsaidia mfugaji kupata faida ya kutosha ,bei hiyo iwe inatambulika  ili kila mtu anapoingia  kwenye fani   ya ufugaji  ajue anapoenda kuuza  atauza kwa bei gani ambayo ita mpatia faida

- kwaupande wa chakula wameiomba serikali   kuangalia namna  watakavyoweka bei elekezi ya vyakula vya kuku itakayo wasiadia kupunguza makali ya bei  au mabaidiliko ya bei ya mara kwa mara

-wameitaka serikali kuwaangalia wafugaji hao kwa jicho la tofauti ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwawezesha  kuwapatia mikopo itakayowasaidia kukuza biashara zao

NINI KIFANYIKE KUWASAIDIA WALE WANAWAKE AMBAO BADO WANAWOGA

-Serikali itoe elimu ya ujasiriamali kupitia Kwa maofisa ustawi wa jamii wa kila kata  ili waweze kuwaelimisha wanawake namna ya kufanya biashara hii na kuwaeleza faida zake

-japo Kuna mikopo iliotegwa na halmashauri Kwa ajili ya Wanawake lakini Kuna haja ya serikali kuwa punguzia mashariti wamama hawa ,pamoja na  wale viongozi wanaotoa fedha hizo kuwahudumia Kwa lugha rafiki Ili wamama wale waweze kujiamini na kwenda kuchukuwa mikopo Kwa ajili ya kuanzia biashara kama ilivyokusudiwa awali na serikali 




Share this:

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

 
Back To Top
Copyright © 2014 MOUNT KILI NEWS. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates