Mfumo huria , uhuru na demokrasis isio mipaka umedaiwa ni kati ya mambo yalioporomosha maadili ,mila na utamaduni hadi kujitokeza vitendo vya ushoga, ulawiti na usagaji.
Baadhi ya wananchi waliohojiwa kwa nyakati tofauti na Mwandishi Wetu jijini Dar es salaam wamezitaja sababu kadhaa.
Elias Issack Hoza Mkaazi wa Mission quater kariakoo, alisema kukua kwa uhuru , demokrasia na kinachoitwa haki za binadamu kumesawa kuchangia kudhoofisha kwa sheria katika baadhi ya mataifa hususan barani Afrika.
Hoza alitoa mfano akisema utamaduni wa Uropa, Asia au Marekani ni tofauti kabisa na ule wa Afrika hivyo alidai ili utamaduni mmoja ukubalike lazima tamaduni nwingine zikubali kupotea.
"Neno demokrasia limebeba maana na upana usiofikirika kulikoidhoofisa mifumo ya kijamii , kanuni na sheria. Zimeshafutika kanuni za asili kinadharaia na kiuhalisia . Ili demokrasia inayotakiwa ifanyiekazi lazima tamaduni nyingine zife " Alisema Hoza.
Sebastian Sembuli anayeiishi Magomeni Mtaa wa Tosheka alisema enzi za ujima na baadae ukoloni hadi kujitawala kuna mambo katika jamii za hayakuwezekama kuguswa ikiwemo watoto kuwa na sauti au maamuzi mbele ya wazazi wao.
Sembuli alidai hivi sasa baada ya kujitawala,kumejitojeza madai ya kulilia ustawi wa demokrasia na baadhi ya watu ktaka uhuru unaovuka mipaka na kuwa moja ya kichicheo cha mmomonyoko wa maadili na kanuni za kijamii.
"Ikiwa leo hii mtoto anathubu kumkalikia kwa sauti mazazi wake na mzazi amekaa kimya hilo ni janga. Uhuru na demokrasia hii ni zaidi ya wazimu. Ikiwa jirani hawezi kumchapa mtoto wa jirani yake ni aibu" Alisema Sembuli.
Joyce Kimario anayeishi Ilala Mtaa wa Arusha alisema ingawaje wanawake wamepewa uhuru na kutambuliwa haki zao, uhuru huo umekuwa ukitumika vibaya na kusibabisha ndoa nyingi kuvunjika na familia kuyumba.
Kimario alisema endapo kutakosekana mgawanyo wa majukumu kati ya mke na mume, huruma na mapenzi yakapuuzwa , hapo ukatili huchukia nafasi hatimaye kanuni za kinidhamu, adabu na maadili huvunjika .
"Heshima ya familia,mila , dasturi na kanuni za makabila ziheshimiwe. Nafasi ya mwanamke ibaki kama ilivyo.Mwanamke usivunjwe utu wake kwa kigezo Uhuru zaidi. Yanayofanyika leo zamani hayakuwepo na dunia ilitulia"Alieleza .
Hamis Hamprey anayeishi Hale mkoani Tanga na mfanyabiashara wa sokoni kariakoo , alisema kuenea ushoga,ulawiti na usagaji ni matokeo ya baadhi ya dola za Afrika kukosa nguvu za kiuchumi na kubaki kuwa tegemezi .
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia