“wazazi na jamii inapaswa kuwapa watoto nafasi sawa bila kujali jinsia tumepata fursa ya kuzungumza mawili matatu na mwanafunzi, mwalimu pamoja na afisa elimu wa mkoa wa Arusha juu ya fursa zilizopo kwa watoto wa kike kielimu “
Neema Mollel ni msichana wa kimasai ambaye alikuwa na ndoto ya kusoma na kufika mbali kielimu lakini anaeleza kuwa ilifikia wakati alishidwa kuendelea na masomo yake kutokana na baba yake mzazi kumlazimisha kuingia katika ndoa akiwa mdogo pamoja na yote alikuwa bado anaitaji kupata elimu
“mimi nilikuwa napenda sana kusoma na nilipata fursa ya kupelekwa shule na ma mama yangu nilisoma lakini nilipofika darasa la sita baba yangu alinifata na kuniambia anataka niache shule na niolewe lakini kutokana na kuwa nilikuwa bado naitaji kusoma nilienda kuwaeleza walimu walimuita baba na kumshauri lakini hakuwaelewa na aliendelea kunilazimisha kuolewa ,kwa vile walimu waliona ninania ya kutaka kusoma ndipo walinichukuwa na kunitorosha katika kijiji changu yaani pale nilipokuwa nasoma wakanitafutia shirika la kunisaidia likanichukuwa na linanaendelea kunisomesha hadi sasa nilikuja katika shirika hili nikiwa la sita na sasa nimemaliza la saba nashukuru mungu wameniendeleza na sasa nasomea ufundi “
Alieleza kuwa anaamini kabisa alifanyiwa kitendo hicho kutokana na dhana ya mwanamke kutothaminiwa katika jamii.
Naye Ng'ookoko Sabaya anaeleza kuwa katika jamii zao anasikitishwa sana na kitendo cha wanawake kuzarauliwa na kuonekana wao kazi ya nikulea familia na kutafuta maitaji ya familia
"Yaani baadhi ya familia wa jamii yetu bado wanamfumo dume japo kuwa serikali imetoka elimu bure lakini Kwa vile ni mtoto wa kike anaenda kusoma basi baba hajigusi Kwa chochote zaidi ya kumuachia mama majukumu yaani hamnunulii mtoto wa kike hata daftari ,Sasa ivi kunamaswala ya chakuka shuleni ,Unakuta kisa ni mtoto wakike baba hamlipii Kwa madai hata akimlipia akasoma baadae awezi kuja kumsaidia kwani ataolewa na kuondoka kwenda katika familia ingine ambayo wanaamini kule ndipo atakapo saidia"alisema Ng'ookoko
TATIZO HASWA NINI?
kuna changamoto mbalimbali ambazo zinawakumba watoto wa kike haswa wa jamii za kimaasai pamoja kuwa serikali bado inaendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kumpatia mtoto wa kike elimu lakini bado kuna baadhi ya wanaume wa makabila hayo bado wanadhana ya kusema mtoto wa kike hana haki ya kupata elimu kazi yake ni kuolewa na kulea familia tu
Watoto wa kike wanakabiliwa na changamoto nyingi Kiini cha matatizo haya ni kukosekana kwa usawa wa kijinsia katika jamii nyingi hasa za kiafrika kati ya watoto wa kike na wa kiume kuanzia ngazi ya familia.
TUMEFIKAJE APA
Ipo dhana potofu iliokuwepo katika jamii ambapo wengi huamini kuwa mtoto wa kike hawezi kufanya kitu cha muhimu ukilinganisha na mtoto wa kiume halihii hutokana na mfumo dume uliotawala katika jamii nyingi, Jamii zimekuwa zikiamini kuwa mtoto wa kiume ni muhimu sana kuliko wa kike na hivyo hupewa kipaumbele na fursa katika nyanja zote ikiwemo kupata elimu.
NINI KIFANYIKE
Hata hivyo changamoto zinazowakabili watoto wa kike zinatatulika Mwalimu Idda anapendekeza mambo yafuatayo ili kuwasaidia watoto wa kike kuimarisha uwezo wao na kujiamini.
-lazima suala la elimu lipewe kipaumbele kwa mtoto wa kike
Waalimu wanatakiwa kufanya bidii ili kuleta usawa baina ya wavulana na wasichana kwenye suala la elimu.
Kuwahamaisha kupenda elimu na kumpa moyo katika masomo yake ni mojawapo ya mbinu za kumuimarisha mtoto wa kike, kwani itamfanya ajione yuko sawa na mtoto wa kiume.
- elimu ya utambuzi ni muhimu sana.
Mtoto wa kike anatakiwa kukumbushwa K kuwa yeye ni sehemu ya jamii na hivyo kazi yake sio kuzaa pekee, hii ni kwasababu baadhi ya maeneo mwanamke alikuwa hasomeshwi, kisha akikua kazi yake ni kuolewa na kuzaa watoto jambo hili sio sawa, mtoto wa kike anatakiwa aelimishwe anawajibika kuijenga jamii yake kwa namna nyingi sio kuzaa pekee pia anatakiwa kutambua mchango wake kwa jamii upo kiuchumi na kadhalika
- kampeni zinaweza kusaidia wanajamii kuondokana na dhana potofu ya kuwa mtoto wa kike hana thamani sawa na mtoto wa kiume
Asasi mbalimbali za kiserikali na zisizo za kiserikali kama vile TAMWA zinaweza kutoa elimu kwa jamii ya thamani ya watoto wote, wa kike na wa kiume pia vilevile, wazifahamishe jamii namna ya kuripoti matukio yanayohusu unyanyasaji wa mtoto wa kike.
- ajira ya wasishana wa ndani ipigwe vita nchi nzima.
Inatakiwa kuwepo sheria inayoelekeza au kutoa mwongozo wa ajira za wasichana wa ndani, Kwamba sheria itamke wazi kuwa msichana aliye chini ya miaka 18 asiajiriwe kufanya kazi za ndani, kufanya hivyo kutachangia sana jamii nzima kumthamini mtoto wa kike na kumuongezea nafasi mtoto wa kike kufikia ndoto zake.
- mtoto wa kike anatakiwa kuthaminiwa katika nyanja zote na apewe nafasi kushiriki kama haki yake kikatiba na kibinadamu
Ofisa elimu mkoa wa Arusha mwalimu Abel Ntupwa akiongea na mwandishi wa habari hizi
OFISA ELIMU MKOA WA ARUSHA AFUNGUKA
Ofisa elimu mkoa wa Arusha mwalimu Abel Ntupwa anasema kuwa elimu ya Tanzania ni elimu ya wote inayotolewa bila kuangalia jinsia ya wanafunzi hali yake kwa mfano ulemavu ,serikali inatoa elimu ya fursa sawa ya elimu kwa wote .
Kwa kutambua katika jamii kuna makundi ambayo yamepewa kipaumbele au yapo katika hali hatarishi zaidi yakiwemo ya wanawake au wasichana ndio maana serikali inatoa kipaumbele zaidi kwa watoto wa kike lakini bila kuwasahau wavulana
Toka mwaka jana serikali yetu imetoa waraka wa mtoto yeyote yule haswa wa kike ambaye alikatisha masomo yake anapata tena fursa ya kuweza kuendelea hii yote ni kumpa nafasi maana uko nyuma mtoto wa kike alikuwa akipata ujauzito ndio ilikuwa imeshaisha lakini kwa kutambua umuhimu wao na nafasi yao katika jamii na kuona kwamba mtoto wa kike akiweza kupambana anaweza kufika mahali pale alipodhamiria na ndio maana kunakuwa na fursa zilizotolewa kwa ajili yao .
Alitoa wito kwa wazazi wajaribu kuitikia huu mdundo na ngoma ambayo serikali imejaribu kwenda nayo kwani hatuwezi kujua mbele ya safari hali itakuwaje uko mbele lakini kwa sasa hivi kwa vile fursa zipo wafuate sheria ,taratibu na muongozo ambao upo na unamuelekeza namna gani mwanafunzi aliekatishwa masomo anaweza kurudi kuendelea na masomo .
Lakini tunakuta tena fursa nyingine huwa tunaangalia mauthurio inapewa kipaumbele sana inachunguzwa mara kwa mara je huyu mtoto wa kike mauthurio yake yakoje ?na pale ndio maana au unakuta kuna ofisa elimu kata ,watendaji kata lakini maafisa ustawi wa jamii wote hawa wapo kuangalia mauthurio ya wanafunzi na ndio maana unakuta shule kama ina bweni mtoto wa kike anapewa kipaumbele kukaa katika bweni na hii inasaidia kumlinda na kumuongezea nafasi mtoto huyo .
Tunajiwekea mazingira ambayo yanajionyesha mtoto wa kike wanavyoenda kwenye uchunguzi kwa mfano kwa sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia kidato cha tano kwaiyo tunaacha muunganiko wa masomo ya sayansi unakuta kwamba taasisi na shule zimejengwa kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kike ndio maana unakuta kwamba kwa mkoa wa Arusha kuna shule moja ya wasichana kwa ajili ya masomo ya sayansi kwa ajili ya wanafunzi wa kike inayoitwa Arusha girls.
Nitoe shime na niseme fursa zipo lakini pia lazima zinaswe ,mtu asije akakaa tu na kusema sisi ukutuna fursa ,lazima wazinase wanavyopata fursa za kupata elimu ya sekondari lazima wajitume wasome masomo ya sayansi
Kwa mkoa wa Arusha kila tukifanya uandikishaji kwenye madarasa ya mitiani ya kidato cha tatu unakuta wasichana wapo juu ya wavulana kwa asilimia 51% kwa wasichana na asilimi 49% ya wavulana kwa iyo nadhani serikali ikiwemo vyombo vya habari na mashirika ya kimataifa ,yasiyokuwa ya kiserikali na yale ya kiserikali yamepigana na kupiga debe elimu na umakini wa wasichana ,kumekuwa na mwitikio chanya mpaka tumeweza kuhofia kwamba ipo siku tutaanza kampeni za kuwaambia wazazi waleteni watoto wa kiume wajewasome mashuleni
Ukienda mbali zaidi baadhi ya shule zetu ukiangalia takwimu zinaonyesha kuwa mtoto wa kike wanaongoza ata katika idadi ya wanafunzi ,ukiangalia kwenye historia tuliotoka ni tofauti sana hata hivi inatupa changamoto kwamba kumbe tukisimama katika hali yoyote ile tukajaribu kuwa na dhamira moja tukahamasishana tukawa na muongozo mmoja wa Tanzania ni rahisi sana kuitikia yale ambayo yanakuwa yameshaelekezwa .
Kwa upande wa watoto wa kike wa jamii za kifugaji inaonyesha kwamba shule za bweni zimeondoa au zimesaidia sana kupunguza tatizo la ndoa au mimba za wanafunzi wa kike .
ATOA WITO KWA WAZAZI
-Wazazi wafatilie mienendo ya watoto wao na kutowaachia walimu peke yake kwani kwa kufanya hivyo kutamsaidia kujua tabia ya mwanae ukizingatia katika kipindi hichi kumekuwepo na wimbi la mmomonyoko wa maadili ikiwemo tishio la kuwepo tabia za ushoga na usagaji
-wazazi wengi wamekuwa wanajali sana biashara zao na kusahau familia zao kwani wengi wao wamekuwa wakiingia makazini asubui na kurudi usiku wakati huo ambapo wakifika majumbani wanakuta watoto wamelala na wanapo ondoka asubui wanawaacha wamelala hivyo wanashindwa kabisa kujua maendeleo ya watoto wao pamoja na tabia zao hivyo wawe makini na watoto wao
-wazazi wapunguze ubize wa kutafuta fedha pamoja na maisha yao ya kila siku na watambue zawadi waliopewa na Mungu ni ya mtoto wake hivyo wawalee watoto wao katika njia nzuri pamoja na njia ipasavyo
WITO KWA WANANCHI
Katika kuhakikisha tunamsaidia mtoto wa kike ni wajibu wa kila mtu kutumia nafasi aliyonayo iwe nyumbani, shuleni, kazini, ama katika jamii kuondoa matatizo yanayomkabili mtoto wa kike kutokana na ubaguzi.
Kila mmoja asisite kuzungumza na waalimu maana wao hutumia muda mwingi sana na wanafunzi na wanaweza kuwajengea watoto dhana chanya ya usawa wa kujinsia wakiwa na umri mdogo.
Habari hii imeandikwa na Woinde Shizza , ARUSHA
Post a Comment
unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia