Pendo Renatus Mkenda mmiliki wa salooni ijulikanayo kwa jina la New paradise beauty saloon akiendelea kumsuka mteja
Na Woinde Shizza,Arusha
"Mwanamke ananafasi kubwa sana katika biashara hasa kwa kuzingatia wingi wetu wa wanawake tunajua kwa sensa iliofanyika mwaka 2022 inaonyesha idadi ya wanawake ni kubwa ukilinganisha na idadi ya wanaume kwani jumla ya watanzania ni 61,741,120 ambapo kati yao wanawake 31,687,990 na wanaume 30,053,130 hivyo mwanamke ananguvu ya kufanya kazi na kuinua uchumi wa nchi " .
Pendo Renatus Mkenda ni mwanamke anaefanya biashara ya salooni ijulikanayo kwa jina la New paradise beauty saloon anaeleza kuwa mwanamke kwajinsi tu alivyoubwa ameubwa kuweza kumudu mambo mengi na endepo mwanamke ataweza kushiriki kikamilifu katika biashara kama jinsi ambavyo tunafanya wanawake wengi utakuta kwamba biashara ya mwanamke ni rahisi sana kufanya vizuri hasa kutokana na utaratibu wake wa kawaida ule ambao amejiwekea wa kujiwekeza
Lakini wanawake waliowengi pia wanafanya vizuri pia katika biashara lakini mwanamke huyu huyu ata kama sio mfanyabiashara moja kwa moja wapo wakina mama ambao wapo nyumbani na wanaume zao ni wafanya biashara utakuta kwamba kwa kiasi kikubwa kama anashirikishwa vyema .
“mwanamke ambaye sio mfanyabiashara lakini mume wake ni mfanyabiashara ananafasi kubwa ya kushiriki katika biashara ya mume wake na wengi mtajiuliza kwanini ?iwapo mama ni mfujaji wa fedha utajikuta ata baba hawezi kutunza fedha hizo lakini kama anaelewa mume wake anachokifanya na anafanyabiashara baba oviasi mwanamke ananafasi kubwa kwakuwa endapo ata weza kutunza na kusaidia baba kuhakikisha kwamba kile anachokifanya anafanya bila kuharibu malengo kusudio utakuta mwanamke anafanya biashara kwa njia ya moja kwa moja kwa mchango wa mwanamke ni mkubwa sana katika kufanya biashara.
VIKWAZO GANI VINAMKABILI MWANAMKE ?
Betrice Gerard ni mwanamke mfanyabiashara yupo mkoani Arusha anaeleza kuwa kikwazo namba moja kinachomkabili mwanamke mfanyabiashara Tanzania ni uwoga wa kukopa katika taasisi mbalimbali na uoga huo unatokana na mfumo dume ambao zamani ulikuwepo ,wapo wanawake ambao wanatamani kufanya biashara hata ndogo ndogo tu lakini wanaogopa ata kuchukuwa hata zile fedha za asilimia kumi ambazo zimetolewa na serikali kwa ajili ya wanawake wakiofia kwamba mwanaume hataki kwa sababu wanaimani kwamba wakichukua zile fedha atakuja kumuuzia nyuma au hata kuaribu aseti za familia .
Kiukweli ni kwamba wengi ambao wamefanikiwa ni wale ambao wananidhamu ya fedha lakini pia wanakopa katika taasisi mbalimbali ilimradi tu wasiingie katika mkumbo wa wanawake ,unakuta mtu anachukuwa mkopo masalani shilingi laki moja lakini anatakiwa kulipa shilingi laki moja na themanini ndani ya miezi sita au laki moja nanusu yaani faida ya shilingi ya elfu hamsini wengi wa hivyo wanakuwa wanashidwa kufikia malengo na wengine ni wale ambao wanachukuliwa vifaa vyao
"Lakini kama tutajikita vizuri na kupata elimu sahihi ya utunzaji na matumizi sahihi ya fedha kila anaekopa ataweza kufanikiwa kukosekana kwa mitaji kwa sasa ni stori ambayo wanawake tumeepukana nayo kutokana na taasisi za kifedha kuwa nyingi lakini serikali imeandaa kuwepo na vikundi na kila mmoja aweze kukopa kupitia vikundi hivyo na waweze kujikwamua kimaisha"alisema
"Ni wakati sasa wa wanawake wenzangu wengi kuachana na uwoga lakini tuachane na ile kwamba mimi nimechukuwa mkopo wa laki moja nimekuona wewe labda umevaa kitenge cha waxi shilingi elfu thelasini na Tano au arubaini na tano basi natoka kwenye yale malengo kusudiwa naenda kufanya kile ambacho mwenzangu anafanya kwa namna hiyo wengi tutatumbukia kwenye shimo na atutafikia malengo kusudiwa"alisema betrice
Ofisa maendeleo jamii mkoa wa Arusha Blandina Nkini akiongea na mwandishi wa habari hizi
JE KWA UPANDE WANAWAKE WA MKOA WA ARUSHA HALI IKOJE
Ofisa maendeleo jamii mkoa wa Arusha Blandina Nkini alibainisha nafasi ya mwanamke kwa upande wa biashara kwa mkoa wa Arusha wanawake wanamuako mkubwa sana na tunaweza kusema wanawake wa mkoa wa Arusha wanaongoza katika biashara kuliko wanaume katika kufanya biashara kiasi kwamba mpaka sasa tumeona kabisa jinsi gani wanataka kuanza kusahau kabisa swala la malezi na makuzi kwa sababu unaweza kuona kwamba wanawake wa mkoa wa Arusha hawalali unakuta wanatoka majumbani saa kumi na moja na wanaingia katika masoko mbalimbali ya kibiashara
“labda kitu ambacho naweza kuwashauri wanawake waendelee kuwa wabunifu katika biashara
ili kufanya biashara tofauti zaidi ambazo zinaweza zikawaingizia kipato kikubwa zaidi kuliko wote kufanya biashara ya aina moja ambapo inafika mahali mtu anashindwa kufanya biashara kwa sababu ni kwamba biashara zile unakuta wanafanya za aina moja”
Muitikio wa kuchukuwa mikopo kwa wanawake ni mkubwaa maana wanaweke wengi wa mkoa huu wameamka na kwakweli wanachukuwa imefikia mahali hata muda mungine wanawake wanakuwa wengi kuliko fedha ambazo zimetegwa ,unakuta wengi wanaitaji iyo mikopo lakini wanashirwa kupata kwa kuwa ni wengi mno na pesa zinakuwa hazitoshelezi hivyo bado uhitaji wa wanawake wa mikopo ni mkubwa mno “
ATOA USHAURI KWA WANAWAKE
Kuna wanawake ambao wamekuwa wanaogopa kuchukuwa mikopo lakini ni waambie tu watoe hofu wawe na udhubutu na niseme tu biashara yeyote ambayo mtu anafanya ni lazima awe na udhubutu kwa sababu ukiogopa na kusema kuwa hili uliwezi inamaana kwamba kila siku basi utabaki hivyo ulivyo hivyo ni washauri tu wawe na udhubutu na ujasiri wa kusema kwa hiki kitu nakiweza na sio lazima mtu anapo anza biashara aanze na mtaji m kubwa bali anaweza akachukuwa hata mtaji wa shilingi elfu hamsini au laki moja na mtaji huo ukaweza kukuzalishia faida na baadae biashara ikaweza kuwa kubwa
“mimi niwashauri tu waanze na biashara ndogo ndogo kwanza lakini baada waendelee kukuza biashara zao na kukuza kipato chao “
Kwa upande wanawake ambao wapo majumbani namaanisha wale ambao wapo majumbani kwa kujitakia wenyewe lakini kuna wale ambao wapo majumbani wanaume wao wamewakataza kufanya kazi nianze na wale ambao wamebweteka ni washauri tu waamke wasikae nyumbani tu kwa kubweteka bali watoke huko nyumbani na waanze kufanya kazi kwani kwa maisha ya sasa ivi hauwezi kutegemea kipato cha mtu mmoja tu maana kipindi hiki familia inajengwa na watu wawili mama atafute na baba pia atafute hivyo waamke na watoke na wao wakatafute
Kwa upande wa wale wanaosumbuliwa na mfume dume ambao wanaume wao hawataki wafanye kazi tunaendelea kutoa elimu kwa wababa kwa maswala ya ukatili wa kijinsia maana hata kumnyima mama kufanya biashara ni aina ya ukatili kwa upande wa uchumi ,hivyo tunaendelea kuwaelimisha kidogokidogo na tunashukuru muamko ni mkubwa na kunamabadiliko makubwa kwa kuwa tunaona ni jinsi gani hata kwa wenzetu hawa wamasai wameanza kuwa ruhusu wake zao kwenda sokoni pamoja na kufanya biashara zao kwa iyo kunamuamko wa wababa wale ambao walikuwa na mfumo dume kuwaruhusu wake zao kwenda kufanya biashara .