Rose Kitosio,Arusha.
Wakulima
wa chama cha nafaka Amcos mkoa wa kilimanjaro wamekabdhiwa hundi
yenye thamani ya shilingi milioni 257 kwa ajili ya fidia ya hasara
waliyoipata kwenye kilimo cha ngano kwa msimu wa mwaka 2021 /2022.
Akikabidhi
hundi hiyo Mkurugenzi mtendaji wa shirika la bima la NIC Insuarance
Dr Elirehema Doriye amesema fedha hizo ni fidia kwa wakulima hao
mara baada ya kupata hasara kwenye kilimo cha ngano.
Alisema
kuwa wakulima hao kwa msimu huo walilima kilimo cha ngano na kufanya
uwekezaji wa milioni mia tano na kutokana na ukame walipata hasara ya
milioni 257 na kwamba kutokana na hali hiyo shirika la NIC limewapa
fidia hiyo ili waweze kufanya maandalizi ya msimu ujao wa kilimo.
"Kiwango
tulichowapa wakulima hawa kitafidia hasara waliyopata katika kilimo
chao na pia itawasaidia kufanya maandalizi ya msimu wa kilimo ujao kwa
kuwa walishakatia mazao yao bima" aliongeza dr Doriye.
Aidha
aliongeza kuwa wakulima ambao wanakatia bima kilimo wanawapata fidia
ambazo zitawawezesha kuondoa hasara ambazo wamezipata.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhiwa hundi ya fedha hizo mtendaji katika chama
cha nafaka cha Amcos Petro Jacob ameishukuru serikali kwa utararitibu
huo wa kutoa fidia huku akiahidi kuwa wataendelea kushirikiana na NIC
katika shughuli zao za kilimo..
Meneja
wa Bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko kanda ya kaskazini bw Peter
Mobe aliwataka wakulima wanaolima mazao wajiunge na shirika la Nic ili
majanga yanapotokea waweze kufidiwa hasara wanazopata.
Naye
meneja wa Nmb tawi la Siha Frenk Kilasi amewashukuru Nic kwa kutoa
fidia hiyo kwani inaenda kuwarudisha shambani wakulima ambao walipata
hasara kwenye mazao yao.