JE MWANAMKE ANA HAKI YA KUDAI TALAKA?


  

Fatuma Swalehe  ni mwanamke mwenye  umri wa   miaka( 29) alipoolewa kulingana na vipigo alivyokuwa akipata kutoka kwa mume wake alitamani kuomba talaka lakini  kulingana na woga aliokuwa nao na hofu ya  kuchekwa na jamii ilibidi avumilie ndoa ile ya manyanyaso

 

 

Miaka mitano baadae  aliamua kuachana na ndoa ile kutona na manyanyaso aliokuwa akiyapata kutoka kwa mwanamme wake ambaye  kabila lake  ni masai anaeleza kuwa chanzo kilichomfanya aamue kuikimbia ndoa yake ni manyanyaso aliyokuwa anayapata kutoka kwa mume wake kwa kile alichokidai kuwa  asilimia kubwa ya manyanyaso aliyokuwa akiyapata  yalisababishwa na yeye kutokupata mtoto kwa kipindi chote cha ndoa alichoishi.

 



chanzo cha picha:www.northpad.ng

JE ALIDAI TALAKA MARA BAADA YA KUSHIDWA KUISHI KWENYE NDOA

 

Fatuma anaeleza kuwa kutokana na tatizo hilo  alivumilia sana mateso lakini mwisho wa siku alishidwa kutokana na kuzidiwa kwa mateso pamoja na  kuletewa mke mwenzake katika nyumba ambayo alishirikiana kujenga na mume wake

 

Anaekeza kuwa alitoa malamiko yake kwa wazee wa boma lakini aliambulia patupu kwani kila mmoja alikuwa anamwambi avumilie kulingana na kauli za watu ndipo alipovumilia na mwisho alishidwa na kuamua kuondoka bila ya kupewa kitu chochote kwani alipojaribu kumwambia mwanamume wake ampe talaka alikataa kumpa

 

"Niliendelea kuhisi upweke na kukosa matumaini, nilikuwa nahisi kana kwamba napiga kelele lakini hakuna anayenisikiliza ndipo nilipoamua kuweka aibu mbali na kuamua kuondoka bila  kukabidhiwa hati yangu ya talaka  wala mali yeyote  niliochuma na mume wangu ." alisema

 

“unajua kipindi chetu ulikuwa ukiolewa ukaonekana  umetoka kwa bwana  unaonekana Malaya ,unaonekana wewe mtu wa ajabu tofauti na sasa mtu anaolewa leo wiki inayofata katoka hivyo hilo jambo pia lilinichukuwa mda sana mimi kutoka katika ndoa pia niseme tu ukweli pia dini ili nizuia kingine mbali na dini  pia nilikuwa sijui kama ninahaki ya kwenda kudai talaka “ alifafanua bi Fatuma

 

VIONGOZI WA DINI  YA UISLAMU WANASEMAJE KUHUSU UTOAJI WA TALAKA

 

Sheikh   Abubakari Rashidi alisema kuwa mpaka sasa tumejadili haki ya asili ya kutoa talaka ambayo ni ya mume peke yake, Lakini anaweza kumpa mke wake haki ya kutoa talaka, Utoaji  wa mamlaka haya kwa mke unaweza kuwa wa jumla au unaoweza kutumika katika mazingira fulani.

Ili kuhakikisha kuwa haibatilishwi huingizwa katika mkataba wa ndoa kama sharti la kudumu, ambapo kwa mujibu wa sharti hilo mke hupewa mamlaka fulani ambayo tayari watakuwa wameshakubaliana,imekuwa ni kawaida tokea zamani kwamba wanawake wanaohisi kwa namna yoyote kuwa na shaka na mwenendo wa waume zao huhimiza kuwekwa kwa sharti hili katika mikataba yao ya ndoa na hutumia mamlaka waliyopewa, pindi kukiwa na haja ya kufanya hivyo hivyo sio sawa kusema kuwa haki ya talaka ni haki ya mtu mmoja tu na kwamba Uislamu umempa haki hiyo mwanaume tu.

Talaka ni haki ya asili ya mume, ikiwa uhusiano wake na mke wake ulikuwa wa kawaida, Kwa kawaida kama anataka kuishi na mke wake anapaswa kumjali, kumpatia haki zake zote anazostahili na kuishi naye kwa wema, Kama akiona kuwa hawezi kuishi naye kwa wema anapaswa kumlipa haki zake zote na kutengana (kuachana) naye,pia Mbali na kumlipa haki zake anapaswa kumlipa kiasi kingine cha fedha au mali cha ziada kama shukrani kwa wema wake hii ni kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu .

 

 

 

Katika hali hizo talaka haitegemei ridhaa na mapenzi ya mume ikiwa mwanaume huyo hayuko tayari kutoa talaka, mwanamke hawezi kuachwa aendelee kuvumilia maumivu bila kupata dawa, Uislamu hauwi mtazamaji mkimya katika hali hizi,kuna baadhi ya watu wana fikra potofu kuwa kwa mtazamo wa Uislamu hali hizi hazitibiki,hali hii inayowatesa watu wenye bahati mbaya lakini haiwezi kutibika na hivyo mwanamke hana namna isipokuwa kustahamili hadi atakapokufa kwa maoni yetu fikra hii haikubaliki katika kanuni za Uislamu kwani Uislamu ni dini ambayo mara zote hutetea uadilifu. Kujenga jamii adilifu imekuwa ni lengo kuu la Mitume wote

 

Sasa hebu tuangalie nini kinapaswa kufanywa juu ya suala la talaka.

Ikiwa mume hataki maelewano na hatekelezi majukumu yake yote au baadhi ya kifedha (matunzo), kimaadili kuishi naye kwa wema na jimai (ngono) kama ilivyoamrishwa na Uislamu na wakati huo huo hayuko tayari kumtaliki mkewe, je ni hatua gani ichukuliwe? Je kuna sababu inayotosheleza hapa kuiruhusu mamlaka ya kisheria kuingilia kati?

 

MAONI YA SHEIKH


“Ndoa ni mkataba mtakatifu na wakati huo huo ni aina fulani ya ushirika (ubia) kati ya watu wawili ambao kila mmoja anawajibika kwa mwenzake, na ambao utekelezaji wa majukumu hayo huwasababishia furaha,Kwa kweli, mafanikio na furaha ya jamii nzima hutegemea mafanikio ya uhusiano wao.

Haki kuu za mke ni matunzo, unyumba na kuishi naye kwa wema ,ikiwa mume ataacha kutekeleza majukumu yake na pia atakataa kumtaliki mke wake, je mwanamke afanye nini na amwelekee vipi mume wake? Hapa kuna njia mbili, aidha mamlaka ya kisheria ya kiislamu iingilie kati na kuititangaza ndoa kuwa imevunjika au mke naye akatae kutekeleza majukumu yake


   

VIONGOZI WA DINI YA KIKRISTO  WALONGA

Niukweli kabisa tukizungumza kwa upande wa kidini  ,dini kama dini airuhusu utoaji wa talaka ,lakini kunasababu kamili zilizopo nje ya uwezo wa wakuu wa dini ambao zinafika mahali ambapo unakubali kwa ajili ya wale watu kila mmoja aweze akadai talaka.

Na tukizungumza hali halisi ya je mwanamke  anauwezo kudai talaka  jibu ni kweli ana uwezo wa kudai maana kwenye maswala ya ndoa kisheria  mwanamke au mwanaume wanahaki sawa katika swala la kisheria na tufahamu ya kwamba ndoa sio dini tu lakini ni jambo la kisheria na sababu unaweza ukaona ya kwamba watu wawili wanaweza wakawa na ndoa halali ya kisheria na kwa upande wa dini wakawa tofauti  katika madhehebu yao naniseme tu hakuna makosa yeyote ya mwanamke kudai talaka ila inategemea na mazingira  nanini kinampelekea adi.

askofu mkuu wa kanisa la Gombo la chuo lililopo ndani ya mji mdogo wa Ngaramtoni uliopo wilayani Arumeru mkoani Arusha Daniel Methew alipokuwa akiongea katika matukio ya kusimikwa kwakwe kuwa askofu

 

 

 “ninukuu katika kitabu cha  agano jipya Yesu mwenyewe alisema apendi kuona watu wakiachana lakini nini hasa kinachopelekea hata huyu mkristo  anadai talaka  ,niseme tu kanisa halina mamlaka wala halikubaliani swala la kutoa talaka lakini narudia kusema sheria pekee ndio yenye mamlaka ya kutenganisha ndoa ,pia kunasababu za msingi zinazoweza kupelekea mwanamke huyo akadai talaka mfano anatishiwa  kuuwawa na mwanamme wake basi iyo ikibainika hata kwa wakuu wa dini wanapokaa na kujadili hilo jambo na kuona ni kubwa na linashindikana kutengeneza basi watawaruhusu  hao wanandoa kwenda kwenye vyombo vya sheria na sheria ikaweze kutoa suluhu kama nikuwatenganisha  lakini hii ni baada ya kukaa vikao vya kujaribu kuwapatanisha na kushindikana

AELEZA SABABU HALISI ZINAZOPELEKEA MWANAMKE KUDAI TALAKA?

Nieleze tu baadhi ya sababu zinazopelekea mwanamke kudai talaka  ni pamoja na 

- Unakuta mwanamume amemuacha mke wake labda kwa miezi zaidi ya sita bila ya kuwa na sababu yeyote hii ni moja wapo ya sababu inayompekea yule mwanamke kuwa na haki ya kudai talaka 

-mwanamme kuoa mwanamke mwingine  bila mwanamke wa kwanza kujua  kama mumewake anataka kuoa

-kulingana na mazingira anayoishi  ,labda ananyanyaswa au anafanyiwa vitendo vya ukatili pamoja na unyanyasaji wa kijinsia ,

- kufanyiwa vitendo vya kudhalilishwa 

 

NINI KITAMPATA IWAPO  AKINYAMAZA

Alienda mbali zaidi na kudai kuwa  iwapo mwanamke atafanyiwa vitu hivyo na  kunyamaza uku akiofia labda dini yake anaweza akapata shida kubwa kwa sababu ya kunyamaza kwani linaweza kutokea tatizo kubwa ambalo iwapo angeongea mapema angeweza kusaidika kabla ya madhara na pia niseme kanisa likimnyima mwanamke kwenda kueleza matatizo yake litakuwa  linamgandamiza na pia litakuwa linavunja haki ya kibinadamu kwa mwanamke huyo  na ikumbukwe kuwa kule kuoana ni makubaliano ya watu wawili na kanisa linakuwa kama shahidi na serikali ikawapa wakuu wa dini leseni,  lakini cheti cha ndoa kikiwa kinatolewa na jamuhuri  ya muungano wa Tanzania  na kanisa alina haki ya kuvunja bali linahaki ya kupatanisha  huku serikali ikiwa na haki ya kutengua  baada ya kupitia mashauri mengi  na inapofikia mahali ya kwamba haifai tena kuunganisha basi wanaachana na kila mtu anapewa uhalali wake wa kufanya anachoitaji


kwenda kueleza matatizo yake litakuwa  linamgandamiza na pia litakuwa linavunja haki ya kibinadamu kwa mwanamke huyo  na ikumbukwe kuwa kule kuoana ni makubaliano ya watu wawili na kanisa linakuwa kama shahidi na serikali ikawapa wakuu wa dini leseni,  lakini cheti cha ndoa kikiwa kinatolewa na jamuhuri  ya muungano wa Tanzania  na kanisa alina haki ya kuvunja bali linahaki ya kupatanisha  huku serikali ikiwa na haki ya kutengua  baada ya kupitia mashauri mengi  na inapofikia mahali ya kwamba haifai tena kuunganisha basi wanaachana na kila mtu anapewa uhalali wake wa kufanya anachoitaji


Mwanasheria mwanamke Mary Mwita akiongelea maswala ya je mwanamke ana haki ya kudai talaka  ?alipotembelewa na mwandishi wa habair hizi ofisini kwake

MWANASHERIA  AFAFANUA ZAIDI KWA UPANDE WA SHERIA

Mery Mwita ni mwanasheria  mwanamke anaeleza kuwa mwanamke ana haki ya kudai talaka kwa sababu yeye ndio anajua maisha ayayaishi yeye na mume wake au mwenzi wake  akiona anapitia magumu kwa mfano manyanyaso ya kupigwa adi wakati mungine kuzimia ,mateso kuzidi adi kupitiliza  anauwezo wa kwenda kufungua madai ya talaka lakini pia lazima afate utaratibu kuanzia katika ngazi ya chini yaani baraza la usuluishi wa ndoa  la kata hadi nafasi zingine za juu hadi pale atakapo ona amepata suluhu na kama ndoa hio ikiwa inaviashiria vya kushindikana kupona basi sheria zifuatwe na watu hao watenganishwe 

Katiba yetu imetamka bayana katika ibara ya 14    kwamba kila mtu anahaki ya kuishi huku ibara ya 15 ikiongelea haki ya uhuru wa mtu binafsi, kupata haki kutoka katika jamii  hifadhi ya maisha yake Kwa mujibu wa sheria ,hivyo basi kama Kila mtu anahaki ya kuishi na katiba yetu inasema asijue akauliwa mtu yeyote akatolewa  kwa kung'ang'ania  ndoa .

 

KWA NINI TALAKA?

Moja wapo ya vitu ambavyo vinasababisha mtu akaomba talaka ni mwenendo na tabia mbaya zilizopo  miongoni mwa  wenzi katika swala la ukiukaji wa maadili mfano usaliti  mtu anafanya tabia za usaliti na anakwenda kinyume na  maadili ya ndoa   ,kinyume na makubaliano , mwanamume anakuwa na mahusiano mengine  na anatelekeza familia kwa hiyo mambo hayo yanampelekea mwanamke kuwa na haki ya kwenda mahakanani kudai talaka 

 

Kisheria ushaidi ukijitosheleza kuwa muhusuka alikuwa ananyanyasika  na nihaki yake kudai talaka basi  anapewa  kwakuwa ni haki yake kisheria ,kama pia anaona ndoa hiyo itampelekea kupoteza uhai wake   na anayofanyiwa na mwezi wake yeye ndio anayajua anayo haki ya kudai,dini inaweza ikawepo lakini hakuna mtu anaetamani ndoa ivunjike  maana ikivunjika  maana yake familia imesambaratika  ,watoto wanakosa muelekeo  kwa iyo viongozi wa dini  wakati mungine  wanafanya kwa nafasi zao kwa mujibu wa maandiko lakini pia na yeye mwanamke  anahaki kama ya mwanamume ya kudai talaka .

 


ANAMAONI GANI

-ni wakati wa  wanawake kujenga utamaduni  wa kusoma pamoja na kupenda kufata utamaduni wa kufuatilia wanasheria ili waweze  kuwapa  elimu  kuhusiana na maswala ambayo yanawatatiza na yanaitaji msaada wa  ki sheria 

-pia ndi vyema wanawake kuacha kutumia simu  katika maswala yasiofaa watumie simu kufuatilia maswala mbalimbali ya kisheria ili kuweza kupata uelewa na kutambua mambo mbalimbali ya kisheria kupitia simu zao ,pia kuna kunabaadhi ya wanawake wamekuwa wakifungiwa ndani na wanaume zao ,wakinyanyasika uku  wengine wakinyimwa ata kwenda kwa jirani  na wanaume zao na hii yote inatokana na wao kukosa elimu  hivyo nijukumu lao kutafuta msaada wa kisheria   utakao wasidia kuondokana na matatizo hayo

 

- Kwa kufanya hivyo itawasaidia kujua maswala ya sheria  na kujua sheria inasema nini  na wakiijua hakuna mtu ataweza kuwanyanyasa na watapata haki zao ikiwemo ya kudai talaka ,huku akiwasisitiza wanawake kuamka na kutokubali kunyanyaswa tena

 

-Aidha pia elimu itolewe kwa nguvu kubwa kama inavyoonekana katika karne hii  ambayo inaonekana kunauelewa mkubwa sana haswa katika vitendo vya ukatili ,watu wameamka na wanafichua vitendo vya ukatili ambavyo wanafanyiwa   tofauti na zamani hata mwanamke alikuwa akipigwa na mme wake  akienda katika vyombo vya sheria anakataa kuwa ajapigwa na kusema kitu tofauti na alichofanyiwa 

 

-Elimu kubwa iendelee kutolewa ili kuondoa mianya  ya wazee wa kimila wanaoona mtu ananyanyaswa  ameumizwa na wanataka wakayamalizie nyumbani badala ya sheria kufuata mkondo wake,Mila na desturi zimechangia sana watu kupoteza maisha kwakuwa wanasema wakayamalize nyumbani hivyo mwanamke asikubali ahamke  na akasake haki yake  , pia mwanamke  anahaki na apaswi kunyanyaswa na kufanyiwa ukatili ni vyema wanawake waamke wasake haki zao za msingi zikiweo za kudai talaka kama wameshidwa ndoa

habari hii imeandikwa na mwandishi wa habari  Woinde Shizza  wa libeneke la kaskazini blog

Post a Comment

unashauriwa kutoa maoni muda na wakati wowote na kama unahabari yeyote unaruhusiwa kututumia

Previous Post Next Post