Shule ya Mlangarini.iliyopo manispaa ya Arusha vijijini katika Wilaya ya Arumeru limeteketea kwa moto pamoja na vifaa mbalimbali vya wanafunzi yakiwemo madaftari pamoja na sare za wanafunzi hao.
Kwa mujibu wa mwalimu mkuu wa shule hiyo Elias John Pallakyo amesema kuwa yeye aliuona moto huo majira ya saa tatu na robo usiku lakini inasadikiwa moto huo ulianza mapema hadi walipofanikiwa kuuzima moto mwjira yasaasita usiku,hadi sasa hasara kamili haijafahamika kwani moto huo umeteketeza vitanda 42 ambavyo ni dabodeka ,sare za shule za wanafunzi hao,masanduku ya wanafunzi ya kuhifadhia vifaa vyao yameharibiwa vibaya na moto huo.
Aidha mkuu huyo amesema kuwa shule hiyo ni mchanganyiko wavulana na wasichana inajumla ya wanafunzi 1195,wanafunzi wanaolala shuleni hapo jumla yao ni 780 ,hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa ,kwani wakati moto huo ulipoanza wanafunzi walipokuwa wakijisomea wenyewe.
Jeshi la liliweza kufika katika eneo la tukio kuimarisha ulinzi,alikuwepo RCO Mkoa wa Arusha George Katabaze ,OCD Arusha Jumanne,OCID Augustino Damgoba pamoja na Inspekta wa zamu wilaya ya Arumeru Alan Mwita,Nae mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexander Mnyete alifika shuleni hapo,uchunguzi wa chanzo cha moto huo bado unaendelea pamoja na hayo walinzi wawili Robson Msuza,Mika Jeremia pamoja na mwalimu wa zamu na mwalimu wa bweni wapo mikononi mwa jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi.
Hii ni shule ya tano kuungua ndani ya mwezi mmoja ilianza kuungua shule ya Sekondari Lowassa iliyopo Halmashauri ya Monduli,Nanja sekondari,Longido sekondari iliyopo Halmashauri ya Longido,Sokoine sekondari iliyopo Halmashauri ya Monduli ,Na Mlangarini sekondari iliyopo Halmashauri ya Arumeru chakushangaza ni kwamba mabweni yote yanayoteketea kwa moto ni ya wavulana.