picha na maktaba aliyekuwa mkuu wa mkoa wa Arusha Filex Ntibenda ambaye uteuzi wake umefutwa
mkuu wa wilaya ya Arusha Mrisho Gambo aliyeteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha na anatarajiwa kuapishwa kesho ikulu jijini Dar es salaam
Na Woinde Shizza, Arusha
Hatimaye mkuu wa mkoa wa Arusha Filex Ntibenda
uteuzi wake umefutwa na
Rais John Magufuli ambapo mkuu wa wilaya ya Arusha
Mrisho Gambo
ataapishwa kesho kuwa mkuu mpya wa Mkoa huo
imefahamika.
Hata hivyo kuna ishara zote kuwa mvutano
uliojitokeza kati ya mkuu
wa zamani Ntebenda na UVCCM
mkoani hapa ndiyo ulioachangia kwa
kiasi kikubwa RC huyo kung'olewa.
Uchunguzi wa weti unebaini kuwa sakata la
wapangaji kulipa kiasi
kidogo cha fesha katika mradi wa maduka ya UVCCM ,
mikataba mibovu na
mkuu wa mkoa kumpigia simu katibu wa Uvccm Mkoa wa
Arusha Ezekiel
Mollel akimtaka ache kuwabughudhi
wapangaji kunatajwa ndiko
kulikoiudhi ikulu na kufukuzwa kazi.
Jambo jingine ambalo pia linatajwa na wadadisi wa
mambo yakisiasa
mkoajini hapa ni mfululzo wa matukio ya uchomaji
moto katika shule
tano za sekondari huku RC akionekana kutochukua
hatua muhimu za
kuyakabili masuala hayo.
Mapema wiki ya juzi katibu wa Uvccm Ezekiel Mollel
aliitisha mkutano
na waandishi wa habari na kumtaka aliyekuwa mkuu
wa mkoa wa Arusha
Ntibenda aaache mara moja kumpigia simu za vitisho
ili kuwalinda
wapangaji wasiotendea haki uvccm katika malipo ya
miradi yake badala
yake ampigie simu za kupambana na hujuma, ufisadi
aidha dhidi ya mradi
ya chama au ile ya serikali .
Kwa upande wake mwenyekiti w a UVCCM mkoa wa
Arusha Lengai Ole Sabaya
naye alisema kuwa wanamshukuru Rais Wa nchi hii
ambaye pia ni
mwenyekiti wa CCM taifa kwa kusikia kilio cha wana
arusha na kuamua
kumtoa mkuu huyo wa mkoa na kuleta mungine .
Napenda kuchukuwa nafasi hii kumpongeza rais wa
nchi hiii kwa kumuona
mkuu huyu wa mkoa kuwa ni jipu afai kwani
kuna mambo mengi ambayo
ameyafanya yasioyofaa tunamuhaidi kumuuunga
mkono na kumpa
ushirikiano wa kutosha mkuu mpya wa mkoa Mrisho
Gambo " Alisema
Sabaya.
Alitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kumpa
ushirikiano wa
kutosha mkuu huyu wa mkoa kwani ni mchapakazi na
pia ni mtenda haki .
Naye katibu hamasa wa
UVCCM mkoa wa Arusha Neema Emanueli Kiusa alisema kuwa wao vijana wa chama cha
mapinduzi hawatakuli kuwa na kiongozi mzigo ,fisadi na ambaye anapenda rushwa
na asiyesimamia haki na iwapo kama kunakiongozi wa namna hiyo ndani ya chama
ajitoe mapema maana UVCCM wakimgundua hawata muacha .
Alisema kuwa anaamini mkuu
mpya wa mkoa anatambua kazi aliotumwa kuwafanyia wananchi hivyo wananchi wasiwe
na wasiwasi huku akiwataka wananchi wa mkoa wa Arusha ,viongozi mbalimbali
pamoja na wafanyakazi wa serikali kumunga mkono kwa kumpa ushirikiano ili aweze
kufikisha mbali mkoa watu na kuwafanyia
watu wa Arusha mambo makubwa ya kimaendeleo .