mama akiwa ananyonyesha picha na maktaba
Na Woinde Shizza,Arusha
Wakinamama
wanaonyonyesha nchini wametakiwa kuwanyonyesha watoto wao kwa muda
uliopangwa kitaalamu ili kuweza kuepuka kupata magonjwa na saratani ya
titi,kuwa na msongo wa mawazo sambamba na ukuaji usiostahili hali
ambayo mtoto anakuwa na uelewa mdogo hasa darasani ambapo hali hiyo
isiposimamiwa na wazazi pindi wawanyonyeshaji itaathiri sana maisha ya
mtoto huyo.
Ambapo
aliongeza kuwa hivi sasa wakinamama wengi hawawanyonyeshi watoto wao
kipindi kilichopangwa kwa muda wa miaka miwili ambapo kutokana na hali
ngumu ya maisha na kuwa watu wamnekuwa wakijishughulisha sana ili kuweza
kutafuta riziki zao wamekuwa wakinyonyesha sichini ya miezi tisa tu
hali hiyo ama madhara yake hayaonekana mapema hasa kipindi mtoto akianza
shule nahasa katika matokeo yake ya kimasomo kushuka na hata kutoelewa
kwa haraka kama watoto wengine wakawaida.
Hayo
yameelezwa leo katika mahojiano maalumu wakati wa tathmini ya hali ya unyonyeshaji na Afisa lishe wa wilaya ya
Meru bi,Asia Ijumaa wakati akitoa somo kwa kinamama wakati wa clinik ya
kinamama na watoto katika hospitali ya Patandi iliyoko tengeru wilayan
Meru mkoani Arusha.
Hata
hivyo alisema kuwa mbali na jitihada zakutoa elimu kwa wakinamama hao
lakini bado wanakabiliwa na changamoto kubwa sana ikiwemo kushuka kwa
kwa hali ya unyonyeshaji ambapo kwa sasa ni asilimia 32 tu ambapo
ukilinganisha na na unyonyeshaji kwa nchi zilizoendelea ambapo ni
asilimia 39 hali ya unyonyeshaji sio nzuri ukilimnganisha na mahudhurio
ya kinamama kupata elimu yao.
Aidha
bi Asia amewashauri wakinamama wote kuweza kuzingatia elimu ya
kunyonyesha watoto ambapo mtoto kuanzia siku sifuri hadi miezi sita
hatakiwi kupewa kitu chochote kila ambapo baada ya muda huo anatakiwa
kuanza kupewa changanyiko wachakula na mlo kamili ili kuweza kumjenga
katika nlishe na kiakili pia.
Kwa
upande wake mmoja wakinamama bi,Sofia Boma alisema kuwa kuna hjaja sasa
watatalamu wa lishe waendelee kutoa elimu kwa kushirikiana na wizara ya
afya ili kuweza kusaidia malezi na makuzi ya watoto hao katika kulinda
maisha yao.
Pia
amewataka wataalamu walishe kuweza kuweka utaratibu wakuwafatilia
wakinamama wanaonyesha ili kuwaangalia mienendo yao ili kuweza
kuhakikisha wanatumia muda wao vizuri katika kunyonyesha watoto wao.