Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha, akimkabidhi Chandarua kwa mtoto Mwasiti Abdallah(miezi 9) aliyebebwa na Mama yake Geni Elias,kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana na Malaria ujulikanaao kama Chandarua Kliniki,uliofanyika mkoani Mwanza kwa ushirikiano wa serikali na USAID.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mary Tesha,akimkabidhi chandarua mama mjamzito mkazi wa Mkolani jijini Mwanza Elizabeth Edward, kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana na Malaria iitwayo Chandarua Kliniki ulioganyika mkoani Mwanza.mradi huo wa chandarua kliniki unatekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks wakishirikiana na serikali.
Msanii wa muziki wa taarabu Khadija Kopa, akitumbuiza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana Malaria ujulikanao kama chandarua kliniki unaotekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks wakishirikiana na serikali, uzinduzi ulifanyika jijini Mwanza jana
Msanii wa muziki wa taarabu Khadija Kopa, akitumbuiza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana Malaria ujulikanao kama chandarua kliniki unaotekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks wakishirikiana na serikali, uzinduzi ulifanyika jijini Mwanza jana.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mo Music, akitumbuiza kwenye uzinduzi wa kampeni ya kupambana na Malaria Chandarua Kliniki unaotekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks wakishirikiana na serikali uliofanyika jijini Mwanza jana.
Mpango wa Chandarua Kliniki wagawa vyandarua mkoani Mwanza.
Malaria yapungua mkoani mwanza
Mpango wa ugawaji wa vyandarua unaojulikana kama CHANDARUA KILINIKI ulioanzishwa na serikali ya Marekani kupitia shirika la USAID umewafikia wananchi wa Mwanza mwishoni mwa wiki ikiwa lengo lake ni kuendeleza dhamira yake yakupambana na malaria nchini hasa kwa Mama wajawazito na watoto.
Akitoa taarifa, wakati wa utambulisho wa mpango na ugawaji vyandarua kupitia kliniki ya wajawazito na watoto,Mratibu wa Malaria mkoa wa Mwanza Dk Saula Baichumila alisema Jumla ya wagonjwa 235 wa Malaria katika Mkoa wa Mwanza wamepoteza maisha kwa kipindi cha miezi sita kuanzia Januari hadi Juni mwaka huu ambapo vifo 121 sawa na asilimia 51.5 ni vya watoto chini ya miaka mitano.
“Kutokana na vifo hivyo halmashauri ya Sengerema inaongoza kwa asilimia 27.6, Magu 20.4, Ukerwe 14.5, Nyamagana 11.9, Misungwi 11.1, Kwimba 8.5, Buchosa 3.4 na Ilemela 2.6,” alisema Dk Baichumila
Alisema mkoa umeendelea kupambana na ugonjwa huo kwa kushirikiana wadau mbalimbali ambapo kumekuwa na matokeo mazuri kwa ugonjwa huo kupungua hasa toka waliposhirikiana na USAID kupitia mpango wa CHANDARUA KLININKI mkoani Mwanza hadi sasa jumla ya vyandarua 142,360 tayari vimesambazwa kupitia vituo vya kutolea huduma za afya mkoani hapo.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Marry Onesmo, alisema maambukizi ya ugonjwa wa Malaria mkoani hapo yamepungua kutoka asilimia 19.1 ya mwaka 2011/12 hadi kufikia asilimia 15.1 mwaka2015/16.
Alisema lengo la mpango huo ni kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano vinavyosababishwa na malaria.Alisema takwimu za kitaifa za mwaka 2012 zinaonyesha kuwa kila vizazi hai 1000, watoto 54 hupoteza maisha huku malaria ikiongoza kuchangia vifo hivyo, huku kila vizazi hai 100,000 wajawazito 432 hupoteza maisha wakati wa kujifungua.
Mpango wa chandarua kliniki unatekelezwa na USAID chini ya mradi wa Vectorworks ambao ni mradi wa miaka mitano 2014-2019 ukiwa na dhumuni la kuongeza upatikanaji na matumizi ya vyandarua vyenye viatilifu vya muda mrefu kwa kushirikikiana na serikali ambapo wamejiweke lengo kuwa hadi kufikia mwaka 2016 kitaifa iwe imefikia asilimia 6 na mwaka 2020 iwe asilimia 1 kutoka asilimia 9 ya sasa.