MBUNGE WA VITI MAALUM CATHERNINE MAGIGE (WAPILI KUTOKA KUSHOTO ) NA
MWENYEKITI WA UVCCM LENGAI OLE SABAYA (WANNE KUTOKA KUSHOTO) WAKITAZAMA
VIFAA VYA WANAFUNZI VILIVYOHARIBIWA KWA MOTO KATIKA BWENI LA WAVULANA WA
SHULE YA SEKONDARI MLANGARINI LILILOTEKETEA KWA MOTO JANA.PICHA NA
WOINDE SHIZZA,ARUSHA
Na Woinde Shizza ,Arusha.
Kufuatia Mfululizo wa Matukio ya Mabweni ya Shule tano mkoani Arusha
kuteketea kwa moto Umoja wa Vijana wa Chama Mapinduzi mkoani hapa
wameitaka serikali itoe majibu ya chanzo cha matukio hayo ikiwa ni pamoja
na kuwachulia hatua wanaohusika na vitendo hivyo ili kunusuru uharibifu wa
majengo na mali pamoja na maisha ya wanafunzi.
Mbunge wa Viti Maalumu mkoa wa Arusha Catherine Magige aliyeongozana na
Viongozi wa Uvccm kutembelea shule ya Sekondari Mlangarini ambapo bweni la
wavulana liliteketea kwa moto ,ameitaka serikali kuchukua hatua za kufanya
uchunguzi na kudhibiti matukio hayo kwani wasipofanya hivyo wanawaeza
kuhatarisha maiasha ya wanafunzi hao.
Catherine alisema kuwa umekua ni mtindo mpya umeibuka wa kuchoma mabweni ya
wavulana katika shule za bweni mtindo ambao usipotafutiwa ufumbuzi wa
kudumu unaweza kuwa janga kubwa litakalopelekea vifo vya watoto .
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya wamesema kuwa Kamati
ya Ulinzi na usalama inapaswa kutafuta mtandao huu unaohusika na uchomaji
wa mabweni ya wanafunzi ili kudhibiti vitendo hivyo hatarishi kwa usalama
wa wanafunzi.
Sabaya amezitaka Mamlaka husika zichukue hatua kukabiliana na tatizo hilo
ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi endelevu katika shule za Bweni.
Katibu Hamasa wa UVCCM Neema Kiusa amesema kuwa serikali inaingia hasara
kukarabati majengo yanayoungua na kujenga gharama ambazo zingetumika
kujenga majengo mapya ya shule hivyo wamesikitishwa na tukio hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya shule Mathias Manga amesema kuwa kwa sasa wanaendelea
na juhudi za kutafuta magodoro pamoja na kupata vifaa vya ujenzi ili
wanafunzi hao warudi katika masomo yao hivyo amewataka wadau wa maendeleo
kujitokeza kusaidia shule hiyo.
Baadhi ya Shule zilikubwa na janga la moto mkoani Arusha ni pamoja na Shule
ya Msingi Edward Lowassa ,Shule ya Sekondari Longido,Shule ya Sekondari
Nanja pamoja na Shule ya Sekondari Mlangarini.